Serikali yaonya Shule binafsi kuhusu michango

Serikali yaonya Shule binafsi kuhusu michango

Nafikiri sasa mtaelewa alichokuwa anasema Kaunga jana..

Watu wanatakiwa kufatilia ili jambo kwa karibu si ku ngoja mpaka watu walalamike na huu ni udhaifu mkubwa wa kamishina wa elimu!

Yani baada ya kuona malalamiko jana ndio tunaona leo wanaibuka na matamko ...watu wanataka kuona mnafatilia kuhakikisha watu hawakiuki maagizo ya serikali!

Ni aibu kuona watu wana kiuka maagizo ya serikali na huku watendaji wamekaa tuu maofisi bila kifatilia utekelezaji mpaka waone malalamiko ndio wastuke!
Hakika watumishi wengi ni mizigo kabisa...

Reformation should touch every department of the government ministries and entities
 
Ada elekizi ni lazima. Ndiyo maana kuna board za kuratibu bei za bidhaa mbalimbali.

UKo sahihi kabisa! Tatizo watu wamefungwa macho muda mrefu na utaona baadhi kweli wanadhani Shule ni biashara. Ngongo na kandawe hapo juu wana mambo muhimu wanayoyaeleza. Kwamba hata wamiliki wa shule wanaelewa wazi kwamba ada hazistahili kuwa kubwa kiasi hicho na hawajalalamika, lakini kwa tamaa yao ya kupata zaidi, wanajidai kuweka michango ambayo kwa kawaida haikustahili kumuhusu mwanafunzi.

Utakuta mchango wa kompyuta, mchango wa kufuliwa nguo, mchango wa mlinzi, mchango wa graduation ya f. 4 au f. 6 hata kama mwanafunzi yuko f.1, mara mchango wa matibabu. Jana nilieleza shule inayolipisha matibabu ya laki 3 utadhani anakweda kufanyiwa upasuaji. mchango wa usafi, eti shuleni wanafunzi wanawekewa mfagiaji na mzazi anaumizwa au wengine wanakenua meno wakidhani ndo raha ya pesa. Wengine wanawalazimisha kuwashonea uniform. Michango yote hiyo ni ya juu na siyo bei halisi. Bado Asiyejijua anadhani ndo mambo ya pesa!

Kwa ujumla tukubali pia kwamba serikali iliyopita imetuponza sana! Viongozi hawakujijua na wamiliki wa shule wakadhani wao ndo wanaendesha elimu nchini. Pale Sinza iliwahi kuletwa shule inayoendeshwa kwa kilingala na kifaransa, ikafungwa kwa amri ya wizara. Sasa kuna watu hata hapa JF wakishatoa michango wakapewa like, wanaona sasa kumbe wanajua. Si umeona sasa kwa kutojua wanasema elimu ni biasahara kama zingine? Mtiu wa aina hiyo anadhani ana ufahamu, kumbe ni taabu kabisa!
 
Nakuunga mkono hundred percent ndugu yangu, usanii mkubwa sana wanafanya hawa ndugu zetu wakatoliki. Nina mtoto Bendel Memorial, ada ni shilingi 550,000 tu iliyoandikwa kwenye form. Lakini jumla ya pesa unazotakiwa kulipa, kwa mfano mimi binti yangu yuko form six. Anatakiwa kulipiwa shs 2,250,000!!! Na haijaishia hapo, kapewa na fomu ya kuchangisha yaani mzazi nichangishe kwa marafiki zangu!
Huwezi kuamini eti joho la kuvaa siku ya mahafari ya mtoto anaemaliza form six linalipiwa 100,000! Jamani huu sio wizi kweli!? Sawa ada iwepo na hawezi kuwa 550,000 lakini basi michango ifutwe iwekwe tu kwenye ada. Ada pamoja na michango tulikuwa tunalipa 1600,000.00 kwa term leo imepanda hadi 2,250,000( Plus michango) na wakati huo huo serikali ilitangaza ada zisipande!
Kwa hili serikali ilifanyie kazi, na kwa nini hiyo pesa tuliyolipa term iliyopita isiendelee tu na ki ukweli inatosha kabisa, 1600,000 kwa term ni reasonable na kama walikuwa na mpango wa kupandisha wangetutumia ujumbe toka wakati watoto wanenda kuanza term waliyomaliza ili tujipange. Kiukweli wakatoliki ni wababe sana katika shule zao. Serikali ilifanyie kazi hili ili tulipe ada kama term iliyopita kwa sababu hatukupewa notisi mapema. Mtoto kafunga tarehe 19/12 na anatakiwa 16/01/2016 hilo ongezeko mzazi atoe wapi au wanafikiri tunaziiba wapi, hata mishahara inayoweza kuongezeka kwa ghafla hivyo ni ya wapi?
Hivi wewe umelazimishwa kupeleka wako private schools? mbona kama una chuki na shule za kanisa? kama unaona huwezi acha asome za serikali,ni kama mtu anayeng'ang'ania kula vitu vitamu kama ice cream wakati ana serious problem ya kisukari,then analauumu watengenezaji wa Ice cream?
 
Form Ambayo haicost hata 200 shs kuuzwa elfu 50,000 ni wizi kuliko ule wa uomba viza American Embassy Stationery Charges
 
Ni wazi kwa hapa tulipofika tunahitaji mjadala wa wazi kuhusu viwango vya ada vinazotozwa na shule binafsi na mashirika na pengine tunahitaji tuwe na EWURA kabisa ya kusaidia kuhakikisha ada elekezi inafuatwa. Haiwezekani mambo yaende vululuvuluku hivi km hatuna serikali afu tunatamba kuwa sie wamoja.
 
Nina vijana wa3 wanasoma kimedium fulani. Usafiri tu tena ni ndani ya kilometa mbili kila mmoja namlipia 50,000 kwa mwezi!! Wote 150,000!! Gari wanayopanda sasa utachoka mwenyewe. Hawa wanahitaji uthibiti wazazi tunaumia sana we fikilia wanatuchangisha hadi majengo wkt majengo ni mali ya mwenye shule. Mtoto atamaliza shule lakini majengo yanaendelea kumwingizia pesa mwenye shule. Serikali imeanza vizuri ikaze hapohapo isirudi nyuma kwa sababu kiukweli wazazi tunaumia sana mtu unajibana hadi senti ya mwisho lakini wapi mara utaskia wanataka mchango wa maafali ya darasa la saba wakati mwanao yupo nursery!! Ni ujambawazi wa mchana kabisa.

Miezi michache ilopita nikitaka kuwahamisha nikaenda medium nyingine yule mwalim alitazama kwanza kisha akanitolea fomu lakini cha ajabu ada aliziandika yeye mwenyewe kwenye karatasi jingine tofauti na kiwango cha ada alichoandika ni tofauti na zilizo kwenye fomu!! Ndo tunakotaka kwenda huku? Hapana. Hapa uthibiti ni muhim.
 
Hakuna biashara isiyokuwa na kanuni.Sheria ni lazma zifuatwe,kwa mfano hebu chukulia kusingekuwa na TBS au TFDA kwenye soko la dawa ,vyakula na vipodozi....Acha wapate maelekezo toka tfda na tbs yao kama kulivyo na bei elekezi kwenye mafuta au nauli ktk vyombo vya usafiri.
 
Elimu ni sawa na biashara nyingine yeyote huwezi kunilazimisha kutoza ada wanayotaka watu wa serikalini. Huwezi kuniamria shule ya kupekeka mtoto wangu na pesa nilipayo ni jasho langu kama naona maumivu nitapeleka mtoto magufuli schools. Waache wenye hela waanzishe elite schools nasi tutapeleka watoto. Hatuwezi kuendesha nchi kwa matamko wakati kuna sheria.

Ama unazo za kuchota au umefanikiwa kumpeleka shule ambayo ni fair au we mmiliki ama hauko informed.

kuna shule zinazotoza kupitiliza. jna nimetolea mfano wa shule moja kuwa
Soksi za shule zinauzwa mtaani 1500, wanataka LAZIMA ununue shuleni kwa 5,000
Tracsuit inauzwa mtaani 18,000, wanakulazimisha ununue shuleni kwa 30,000
Basi la shule ukipiga mahesabu kwa term,unakuwa umelipia around 2,000 kwa siku
wana term 3, wanafunga AT LEAST 4 weeks each term, hivyo kwa mwaka wanafunga AT LEAST 3 months. na hizi term 3 ni kuigawa ada ili uone 1M sio nyiiiingi kumbe its 3M,

Hiyo ni Martini Luther ipo kule Dodoma. halafu kafungua shule mbili in one, moja Martin Luther na ingine Martin Luther King. anachukua wanafunzi best 30 na kuwafanyisha mtihani na waliobaki mamia wanafanya kama martin Luther King... haya yote ni kujitangaza kwamba amefaulisha, shule imekuwa ya kwanza kiwilaya ama kimkoa, kumbe Kingi imetupwa mbali kule, hayo yoote ni trick ya biashara, kinachokwaza ni pale anapotumia mwanvuli wa DINI kwamba ameokoka na kajenga kanisa na msalaba mkubwa barabarani Dar road.

Mzazi niligundua dakika za mwisho natamani nipande ndege nikabebe watoto ila sasa wengine wapo darasa la 7 ambapo tunachangishwa 200,000 ya graduation sijui tunaenda kupewa na degree ya kununua!!

hivyo ndugu tusaidiane kufanya biashara halali sio wizi tena kwa kutumia Msalaba
 
Ndio maana unaitwa kapongosilo,nitakutumia vidonge vya kuongeza uwezo wa kufikiri
 
Elimu ni sawa na biashara nyingine yeyote huwezi kunilazimisha kutoza ada wanayotaka watu wa serikalini. Huwezi kuniamria shule ya kupekeka mtoto wangu na pesa nilipayo ni jasho langu kama naona maumivu nitapeleka mtoto magufuli schools. Waache wenye hela waanzishe elite schools nasi tutapeleka watoto. Hatuwezi kuendesha nchi kwa matamko wakati kuna sheria.

Mambo mengine yanafanyika huko tanzania ktk karne hii ya 21 hatoyasikia popote duniani haiingii akili pahala penye soko huru serikali iwe na uwezo wa kumpangia mtu tozo ya gharama za shule yake kama unapanga nauli ya daladala na cha ajabu wapo wanaoshangalia kuona ni sawa!
 
Hapana hakuna aliyetulazimisha lakini kama mzazi mara nyingi utapigana sana kuhakikisha mwanao anapata kilicho bora.Mimi naishi Njiro karibu na shule ya Naura sec naona jinsi wanafunzi wanavyopata shida ya usafiri asubuhi na jioni ukiwa na binti yako unayemjali na kumpenda kwa moyo wako wote kamwe hautopenda kumwona akining'inia kwenye dala dala,akichewa shule,akikosa mwelekeo mzuri wa masomo,akirejea nyumbani hakuna alichojifunza,akipachikwa mimba na madereva au makonda wa dala dala na nk.

Ni wajibu wa serekali kuweka mazingira mazuri ya elimu kwa wananchi wake bahati mbaya watawala wetu hasa awamu za 3 na 4 zilishindwa likatokea ombwe la elimu taasisi za dini zikachukua jukumu la kuziba ombwe hilo ambalo ni faida kwa taifa.

Ndugu yangu waTanzania wanashindwa kushindana katika soko la ajira ya EAC si kwa bahati mbaya ni kwasababu serekali yetu hajawekeza vyakutosha katika sekta ya elimu nchi nyingine zimetambua udhaifu wetu ndio maana zinataka soko la ajira lifunguliwe.Nadhani serekali ya Dr Magufuli inaweza kusaidiana na taasisi za dini katika sekta ya elimu kama serekali inavyofanya katika sekta ya afya.Jambo hili linawezekana kabisa wala si geni.

Nadhani kilicho bora ni serikali kuboresha shule zake zifikie kiwango cha shule binafsi.

Wahakikishe kuna walimu wa kutosha, chakula bora, vifaa vya kujifunzia kama madawati, maabara, vitabu vya kutosha.

Mabweni yawepo kwenye standard nzuri.

Kwa muktadha huu, serikali itakuwa imeongeza 'competition' na shule binafsi ambapo wazazi wataanza kuwapeleka wanao shule za serikali.

Shule za binafsi zinainua elimu kwa kiasi fulani, kuwaingilia na kuwafanyia fujo ni sawa na kuua elimu.
 
Kwa mbaaali naona wamiliki wa shule nyingi wakifikiria kubadili biashara,naona walimu wa Uganda,Kenya na India wakirudi makwao,naona Zahanati binafsi na maduka ya dawa yakifunga biashara.Taswira inatoa picha!
 
Hivi wewe umelazimishwa kupeleka wako private schools? mbona kama una chuki na shule za kanisa? kama unaona huwezi acha asome za serikali,ni kama mtu anayeng'ang'ania kula vitu vitamu kama ice cream wakati ana serious problem ya kisukari,then analauumu watengenezaji wa Ice cream?

Kanisa, kanisa! Hata kama ni kanisa limesemwa, usimchukie aliyelisema maana wamezidi. Aliyeandika anasema ukweli. Mtu anajidai ni kanisa ndo aweke gharama ya joho laki 1! Kanisa gani hilo? That amounts to nonsense!

Hapa hakuna cha kusema hutaki acha, ni swala la kufuata sheria. Ndo maana tunalaani hata anayekunywa pombe kuliko kipimo hata kama pesa ni zako, bar ni yako, tumbo ni lako, etc. Unaleta mfano wa ice cream ili iweje? Hujasikia wavuta sigara wakishitaki mashirika ya utengenezaji sigara na wakalipwa? Acha ushabiki and let ua be seriour in thinking.
 
Hili nalo neno.

Ama unazo za kuchota au umefanikiwa kumpeleka shule ambayo ni fair au we mmiliki ama hauko informed.

kuna shule zinazotoza kupitiliza. jna nimetolea mfano wa shule moja kuwa
Soksi za shule zinauzwa mtaani 1500, wanataka LAZIMA ununue shuleni kwa 5,000
Tracsuit inauzwa mtaani 18,000, wanakulazimisha ununue shuleni kwa 30,000
Basi la shule ukipiga mahesabu kwa term,unakuwa umelipia around 2,000 kwa siku
wana term 3, wanafunga AT LEAST 4 weeks each term, hivyo kwa mwaka wanafunga AT LEAST 3 months. na hizi term 3 ni kuigawa ada ili uone 1M sio nyiiiingi kumbe its 3M,

Hiyo ni Martini Luther ipo kule Dodoma. halafu kafungua shule mbili in one, moja Martin Luther na ingine Martin Luther King. anachukua wanafunzi best 30 na kuwafanyisha mtihani na waliobaki mamia wanafanya kama martin Luther King... haya yote ni kujitangaza kwamba amefaulisha, shule imekuwa ya kwanza kiwilaya ama kimkoa, kumbe Kingi imetupwa mbali kule, hayo yoote ni trick ya biashara, kinachokwaza ni pale anapotumia mwanvuli wa DINI kwamba ameokoka na kajenga kanisa na msalaba mkubwa barabarani Dar road.

Mzazi niligundua dakika za mwisho natamani nipande ndege nikabebe watoto ila sasa wengine wapo darasa la 7 ambapo tunachangishwa 200,000 ya graduation sijui tunaenda kupewa na degree ya kununua!!

hivyo ndugu tusaidiane kufanya biashara halali sio wizi tena kwa kutumia Msalaba
 
Nahisi unaishi kwenye ile himaya ya 'Wapumbavu'. Hakuna serikali ya aina hiyo Dunia hii.
btw. Wewe mwenyewe una elimu ya kiwango kipi? Ni ajabu kuona mtu wa JF anasema elimu ni biashara!

Watu wasio na elimu kama wewe mchunguzi ndio wanaishi kwa kuhisi na at most kupiga ramli. Kwani wale watoto wanaopelekwa kusoma ulaya na marekani hakuna serikali huko? Elite schools ni education system yenye ubora wa hali ya juu na ni very expensive. Thank God Mqagufuli amekuja na shule za bure ambazo watu wapumbavu kama wewe wanatakiwa kupeleka watoto wao ili wanapomaliza hawajui kusoma, kuhesabu na kuandika.
 
Dah! Sasa yaonekana wote tunadhalauliana. Lakini nina hakika niko mbele yako. Hata unavyopanga hoja zako, bado hujafika mwisho wa mikono ya waalimu.

Hebu nidokeze, una elimu ya kiwango gani. Nitakusaidia kujua ni asilimia ngapi umepungukiwa.
 
Serikali ni refa jamani, kama huduma ni ya kinyonyaji ni lazima iingilie kati kuweka mambo sawa
 
Back
Top Bottom