Makini
Senior Member
- Dec 23, 2014
- 154
- 59
Serikali imeonya wadau wa elimu wanaoendelea kutoza ada ya kujiandikisha na michango mingine kuacha mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Eng. Stella Manyanya, amesema wakuu wote wa Wilaya na Wakurugenzi wa Miji na Manispaa watahusika katika kufuatilia kwa karibu na kuhakikisha kuwa agizo la Rais linatekelezwa. Rais Magufuli aliagiza kufutwa kwa michango yote shule ya msingi na Sekondari.
Manyanya pia amewasihi Watanzania kushirikiana na utawala kwa kuripoti aina yoyote ya ukiukwaji wa agizo hilo.
Kuhusu ada elekezi, Kamishna wa Elimu, Prof. Eustella Bhalalusesa amesema Serikali itakuwa na kikao na wamiliki wa shule ili kujadiliana ni kiwango gani kitakachofaa na kisichowaumiza wananchi.
Wakati hayo yakiendelea, Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya juu, Jonathan S. Mbwamba, ameendelea kusisitiza kuwa wanafunzi wote waliokidhi vigezo vya kupata mikopo watapatiwa mikopo hiyo. Idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo imeongezeka kutoka 13,582 hadi 53,032.