Serikali yaondoa Muswada wa Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalamu wa Afya Shirikishi bungeni

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Mbunge wa Siha Mhe.Dr.Godwin Mollel amefanikiwa kuidhibiti serikali na kuzuia muswada wa sheria ya madaktari kuwasilishwa bungeni kwa kuwa ulikuwa na mapungufu mengi.

Mbunge huyo ambaye ndiye Waziri kivuli wa Afya, aliongoza Timu kubwa yenye umoja wabunge wa UKAWA na CCM akiwa kama kocha mkuu wa jopo hilo akiwashauri kusimamia misimamo miwili ambayo ni:

1. TATIZO LA AFYA TANZANIA NI ZAIDI YA SHERIA. Hapa aliitaka serikali kuwekeza kwenye Technologia ya Vifaa tiba na utafiti wa SAYANSI ya afya. Dr.Mollel ambaye ni daktari kitaaluma (MD, Muhimbili), alikosoa pia uchumi wa nchi kuendeshwa kwa mawazo binafsi ya viongozi, hali inayoathiri sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya afya.

2. SHERIA YA MADAKTARI IWATAMBUE MADAKTARI WASAIDIZI. Hapa Dr.Mollel alijikita katika kuwashauri wabunge kuukataa muswada huo kwani hauwatambui madaktari wasio na shahada yani Maafisa Tabibu (COs) na Madaktari wasaidizi (AMOs).

Dr.Mollel aliwatetea madaktari hao wenye Diploma na Advanced Diploma yaani CO, AMO, na ADO, na kusisitiza kuwa wanastahili kuheshimiwa na kutambuliwa na sheria hiyo kwani wanafanya kazi kubwa sana ya kuokoa maisha ya watu hasa vijijini.

Muswada huo ulikua ukiwaweka CO na AMO kwenye kundi la wataalamu wa afya shirikishi, lakini Dr.Mollel alisisitiza kuwaweka kwenye kundi la madaktari kwa kuzingatia taaluma yao na kiwango cha elimu.

Kutokana na hoja hizi za kitaalamu, Dr.Mollel alifanikiwa kushawishi wabunge wa CCM na Upinzani na kwa kauli moja wakakubaliana nae kuwa wataukataa muswada huo. Kufuatia hali hiyo Serikali iliamua kuondoa muswada huo bungeni kwenda kuufanyia marekebisho.!

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Nitumie fursa hii kumpongeza sana rafuki yangu Dr.Mollel kwa ujasiri huu wa kupigania maslahi ya taifa. Pia niwapongeze wabunge wa CCM waliomuunga mkono Dr.Mollel kwenye hoja hii. Kimsingi muswada huo ulilenga kukwepa tatizo la msingi la sekta ya afya, lakini pia ulilenga kuwanyanyapaa madaktari wasaidizi (AMO) na maafisa tabibu (CO).

Lakini watu hawa wana tija kubwa kwa taifa. Wanahudumia mamilioni ya watanzania, wanaokoa roho za mama zetu na baba zetu huko vijijini. Kuna watu wanazaliwa mpaka wanazeeka hawajawahi kumuona daktari wa degree (MD). Wametibiwa na hao AMOs na COs amvao leo mnataka sheria isiwatambue. Hivi mnajua kazi kubwa wanayofanya hao COs na AMOs? Hivi mnajua COs wanahudumia tarafa nzima huko vijijini yuko peke yake??

Pongezi Dr.Mollel kwa kazi kubwa na nzuri uliyoifanya leo. Lakini pia nishauri serikali ifanye marekebisho ya muswada huo kama ilivyodhamiria. Muswada huo utakaporudishwa bungeni uwe umeincorporate hoja zote zilizosababisha uondolewe.!

Malisa GJ

========

SERIKALI imeondoa bungeni Muswada wa Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalamu wa Afya Shirikishi wa Mwaka 2016, ambao jana uliotarajiwa kusomwa kwa mara ya pili.

Akiahirisha shughuli za bunge jana, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alisema shughuli hizo zimeahirishwa hadi leo kutokana na serikali kuondoa muswada huo.

Akizungumza nje ya Bunge, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala, alisema muswada huo umeondolewa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo madaktari wasaidizi kuulalamikia.

Alisema serikali itaendelea kuwatambua madaktari wasaidizi nchini kutokana na umuhimu wao katika sekta ya afya, hata hivyo.

Alisema madaktari wasaidizi hao wameonyesha wasiwasi kwamba muswada huo ukipitishwa na kuwa sheria, watakuwa hawatambuliki, "jambo ambalo si kweli".

Dk. Kigwangala alisema muswada huo haulengi kuwafuta madaktari wasaidizi kama wanavyohisi bali kinachofanyika ni kuwatofautisha na madaktari wengine wenye elimu tofauti na wao.

“Serikali imeona ni busara kuuondoa bungeni muswada husika ili baadaye tupate muda wa kuwaelewesha vizuri kabla haujawasilishwa bungeni (tena),” alisema Dk. Kingwangala.

Kwa upande wake, Waziri Kivuli wa Afya ambaye pia ni Mbunge wa Siha (Chadema), Dk. Godwin Mollel, alisema muswada huo unaonyesha kutowatambua madaktari wasaidizi, jambo ambalo alisema halijakaa vizuri.

“Unaonekana kutowatambua vizuri wale madaktari wasaidizi, ndiyo maana wanalalamika, kimsingi wale madaktari ambao wana elimu ya diploma na diploma ya juu, wana umuhimu katika sekta ya afya na ni wengi zaidi kuliko madaktari kamili,” alisema Dk. Mollel.

Alisema ni lazima Serikali iwatambue kisheria kwa sababu baadhi ya kazi wanazozifanya, madaktari wengine hawazifanyi.

Naye Mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk. Faustine Ndugulile, ambaye kitaaluma ni daktari, alisema kinachowafanya watu wavutane ni juu ya tafsiri ya nani awe daktari na nani awe daktari msaidizi.

“Lakini kwa ujumla muswada ni mzuri na unalenga kuimarisha sekta ya afya nchini,” alisema Dk. Ndugulile.

Chanzo: ITV
 
Hao ndio aina ya wabunge wanao hitajika nchini tanzania
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Kawaida yetu kuandika na kusifu.

Kitu kikikataliwa si kwa sababu ya ushawishi wa mtu ila kwa masilahi ya taifa. Siku zote maslahi ya vyama ndio yanaua uzalendo wetu.
 
Amezuiaje yaani zile sauti za wanaoafiki waseme ndiyo wasioafiki waseme hapana sauti yake ulikua kubwa? Usitudanganye.
 
Mbunge wa Siha Mhe.Dr.Godwin Mollel amefanikiwa kuidhibiti serikali na kuzuia muswada wa sheria ya madaktari kuwasilishwa bungeni kwa kuwa ulikuwa na mapungufu mengi.

Mbunge huyo ambaye ndiye Waziri kivuli wa Afya, aliongoza Timu kubwa yenye umoja wabunge wa UKAWA na CCM akiwa kama kocha mkuu wa jopo hilo akiwashauri kusimamia misimamo miwili ambayo ni:

1. TATIZO LA AFYA TANZANIA NI ZAIDI YA SHERIA. Hapa aliitaka serikali kuwekeza kwenye Technologia ya Vifaa tiba na utafiti wa SAYANSI ya afya. Dr.Mollel ambaye ni daktari kitaaluma (MD, Muhimbili), alikosoa pia uchumi wa nchi kuendeshwa kwa mawazo binafsi ya viongozi, hali inayoathiri sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya afya.

2. SHERIA YA MADAKTARI IWATAMBUE MADAKTARI WASAIDIZI. Hapa Dr.Mollel alijikita katika kuwashauri wabunge kuukataa muswada huo kwani hauwatambui madaktari wasio na shahada yani Maafisa Tabibu (COs) na Madaktari wasaidizi (AMOs).

Dr.Mollel aliwatetea madaktari hao wenye Diploma na Advanced Diploma yaani CO, AMO, na ADO, na kusisitiza kuwa wanastahili kuheshimiwa na kutambuliwa na sheria hiyo kwani wanafanya kazi kubwa sana ya kuokoa maisha ya watu hasa vijijini.

Muswada huo ulikua ukiwaweka CO na AMO kwenye kundi la wataalamu wa afya shirikishi, lakini Dr.Mollel alisisitiza kuwaweka kwenye kundi la madaktari kwa kuzingatia taaluma yao na kiwango cha elimu.

Kutokana na hoja hizi za kitaalamu, Dr.Mollel alifanikiwa kushawishi wabunge wa CCM na Upinzani na kwa kauli moja wakakubaliana nae kuwa wataukataa muswada huo. Kufuatia hali hiyo Serikali iliamua kuondoa muswada huo bungeni kwenda kuufanyia marekebisho.!

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Nitumie fursa hii kumpongeza sana rafuki yangu Dr.Mollel kwa ujasiri huu wa kupigania maslahi ya taifa. Pia niwapongeze wabunge wa CCM waliomuunga mkono Dr.Mollel kwenye hoja hii. Kimsingi muswada huo ulilenga kukwepa tatizo la msingi la sekta ya afya, lakini pia ulilenga kuwanyanyapaa madaktari wasaidizi (AMO) na maafisa tabibu (CO).

Lakini watu hawa wana tija kubwa kwa taifa. Wanahudumia mamilioni ya watanzania, wanaokoa roho za mama zetu na baba zetu huko vijijini. Kuna watu wanazaliwa mpaka wanazeeka hawajawahi kumuona daktari wa degree (MD). Wametibiwa na hao AMOs na COs amvao leo mnataka sheria isiwatambue. Hivi mnajua kazi kubwa wanayofanya hao COs na AMOs? Hivi mnajua COs wanahudumia tarafa nzima huko vijijini yuko peke yake??

Pongezi Dr.Mollel kwa kazi kubwa na nzuri uliyoifanya leo. Lakini pia nishauri serikali ifanye marekebisho ya muswada huo kama ilivyodhamiria. Muswada huo utakaporudishwa bungeni uwe umeincorporate hoja zote zilizosababisha uondolewe.!

Malisa GJ
Malisa mtani wangu piga ua utadanganya kama utaniambia waliounga mkono hoja Dr Mollel ama yule mbunge aliyetaka kuwekwa makumbusho ya kupiga push up na kibajaji wamo. Lol
 
Back
Top Bottom