Leo Waziri wa Uchumi na Mipango Mh.Dr Philipo Mpango,ametembelea makao makuu ya Bank ya Barclays na kuiomba kuisaidia serikali ya Tanzania mkopo wa riba nafuu ili iweze kutekeleza miradi yake ya miundombinu ya Reli ya kati ya "Standard Gauge" na mradi wa Umeme wa S.Gorge.
Waziri Mpango ameiomba bank hiyo kutenga kiasi cha fedha ili kuikopesha serikali ili iweze kujenga miradi yake ambayo inahitaji pesa nyingi na kuweza kufikia adhma ya nchi za viwanda.
Swali:Inakuwaje tena Serikali inaanza kwenda kukopa kwenye mabank binafsi na wakati tuliambiwa pesa inayojenga reli ya Standard Gauge na ule mradi wa Stiglers Gorge(?) ni pesa ya ndani ambayo ni kodi yetu?Je kiuchumi kuna athari gani kukopa bank binafsi kama Barclays?
Zile taarifa kuwa miradi inajengwa kwa pesa za ndani huwa ni siasa tu?Kwamba hakuna pesa ndiyo maana tunazunguka kukopa mpaka Barclays?