Serikali yangu imelala ama imesinzia katika haya?

Serikali yangu imelala ama imesinzia katika haya?

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,324
Reaction score
2,494
Ni swali tu najiuliza na nadhani wapo wengine pia wanajiuliza wakati wapo wengine wanalalamika lakini pia wapo wengine hawana la kufanya.

1. Wizi wa airtime kupitia promotion za kitapeli katika mitandao ya simu mfano JAYMILIONARE, ni wizi mtupu kwani unakuta mtu hata hujajiunga nao ila ukiweka salio tu unakatwa pesa yako! Serikali imeruhusu biashara hii ambayo ni zaidi ya upatu. Mh. January Makamba hili limekushinda kupitia wizara yako, uraisi unatafuta wa nini?

2. Mauaji ya Albino; ni kweli kabisa serikali yangu sikivu haina cha kufanya kuthibiti mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi? Amani yetu mbona inabagua albino?

3. Utapeli wa fedha kupitia vyombo vya habari na mitandao kwa kutumia majina ya viongozi, ni kweli viongozi hao wameshindwa kushirikiana na mamlaka husika kuwabaini?

4. Malipo ya Service charge ya kila mwezi katika bill za umeme hata kama hufikishi units 70 zilizopo kwenye sheria, na upandaji holela wa gharama hizo bila sababu za msingi.

5. Mafuta kushuka bei wakati nauli haishuki na madereva kukiri bei inapaswa ishuke ila wanasubiri kauli ya SUMATRA

Ni maswali tu najiuliza, na hadi ifike october nadhani yatakuwa yametimia 20. Naona mpo busy na maandalizi ya uchaguzi mnasahau mambo ya msingi!!

Niongezeeni mengine wadau ambayo nimeyasahau.
 
Back
Top Bottom