Serikali Yamtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Achukue Hatua Stahiki Dhidi ya Aliyemtukana Rais

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,256
16,306

SERIKALI imemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuchukua hatua stahiki katika shauri la kesi ya jinai namba 100 ya Jamhuri dhidi ya Isaac Emily aliyeadhibiwa kulipa faini kwa kumtukana Rais John Magufuli mtandaoni.

Hayo yamesemwa jana bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe wakati akitoa kauli ya serikali baada ya mwongozo ulioombwa na wabunge wa CCM, Juma Nkamia wa Jimbo la Chemba na Livingstone Lusinde wa Mtera, baada ya hukumu hiyo kutolewa hivi karibuni. Hata hivyo, hatua stahiki hizo hazikuelezwa.

Alisema nia ya maagizo hayo kwa DPP ni kulinda dhana na dhamira ya adhabu katika mfumo wa haki jinai ambayo hutaka mhukumiwa kujutia kosa lake na wengine kujifunza kutoka kwake.

Katika maelezo yake, Waziri Mwakyembe alisema kwa hali ilivyo katika shauri hilo, dhana na dhamira ya adhabu haikuweza kufikiwa kwa mwenendo wa kuingiza siasa katika utekelezaji wa hukumu.

Alisema serikali imejiridhisha na kilichotokea katika shauri hilo na kauli za wabunge walioomba mwongozo kwamba masharti ya adhabu yalikuwa mepesi mno usiolingana na shauri lenyewe.

Alisema aliyehukumiwa analifanyia siasa suala hilo na kuigeuza adhabu rafiki aliyopewa kuwa burudani ya kisiasa katika mitandao ya kijamii.

“Mheshimiwa spika, nimejiridhisha na kilichotokea. Madhara ya mwelekeo huu mpya katika haki jinai, ni kuchochea vitendo zaidi vya ukaidi kwa mamlaka za nchi na hivyo kujenga msingi wa vurugu. Hili halikubaliki katika utawala wa sheria. Mdharau mwiba mguu huota tende,” alisema..

Alisema kosa kama hilo lilitokea Kenya mwaka jana ambapo mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini humo, Alan Okengo (25) alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kulipa faini ya dola 2,000 (Sh milioni 3.2) kwa kumtukana rais wa nchi hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema pamoja na umri wake na uwezo wake mdogo wa kulipa faini, adhabu ilibaki palepale ili mkosaji ajutie kosa lake asije akarudia na jamii ijisikie salama.

Alisema pamoja na kutokuingilia mhimili wa mahakama na taratibu zake kitendo cha kuwapo kwa adhabu ambayo haijutiwi inakiuka dhana na dhamira ya adhabu.

Alisema kwa shauri la Emily, pamoja na kutiwa hatiani wakili wake aliomba mtuhumiwa alipe faini kwa kuwa hakusumbua mahakama na pia ni kosa lake la kwanza na ana familia.

Alisema wakati hakimu anamuuliza wakili wa serikali aliiachia mahakama kutoa maamuzi ambayo ilimpatia wakili wa utetezi maombi yake.

Mwakyembe alisema pamoja na maagizo ya serikali kwa DPP amewakumbusha waendesha mashitaka nchini kuwa macho na waweke mbele weledi na maslahi mapana ya taifa na kamwe wasiyumbishwe na mihemko ya kisiasa katika jamii.
 
Mfano hapo utaanzia kwa huyo jamaa yenu!
Subirini hukumu! Hapo Ni kifungo Na faini nasio kifungo au faini!!
 
Chadema ndio kimekuwa chama cha kuendesha harambee ya kuchangia fedha watu wanaotukana mtandaoni.

Hili halikubariki kwa chama chetu kugeuzwa chama cha wahuni
 
Nchi ya ajabu sana hii,badala mjadili maendeleo mnajadili vitu vya kijinga,yule mtu aliyempiga kofi mzee mwinyi msikitini ingekuwa kipindi hiki naona mgesema anyongwe,maana kila kiongozi anamzuka wa RAIS si mnaona Magesa Mulongo alivyokuwa na mzuka
 
SERIKALI imemtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuchukua hatua stahiki katika shauri la kesi ya jinai namba 100 ya Jamhuri dhidi ya Isaac Emily aliyeadhibiwa kulipa faini kwa kumtukana Rais John Magufuli mtandaoni.

Hayo yamesemwa jana bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe wakati akitoa kauli ya serikali baada ya mwongozo ulioombwa na wabunge wa CCM, Juma Nkamia wa Jimbo la Chemba na Livingstone Lusinde wa Mtera, baada ya hukumu hiyo kutolewa hivi karibuni. Hata hivyo, hatua stahiki hizo hazikuelezwa.

Alisema nia ya maagizo hayo kwa DPP ni kulinda dhana na dhamira ya adhabu katika mfumo wa haki jinai ambayo hutaka mhukumiwa kujutia kosa lake na wengine kujifunza kutoka kwake.

Katika maelezo yake, Waziri Mwakyembe alisema kwa hali ilivyo katika shauri hilo, dhana na dhamira ya adhabu haikuweza kufikiwa kwa mwenendo wa kuingiza siasa katika utekelezaji wa hukumu.

Alisema serikali imejiridhisha na kilichotokea katika shauri hilo na kauli za wabunge walioomba mwongozo kwamba masharti ya adhabu yalikuwa mepesi mno usiolingana na shauri lenyewe.

Alisema aliyehukumiwa analifanyia siasa suala hilo na kuigeuza adhabu rafiki aliyopewa kuwa burudani ya kisiasa katika mitandao ya kijamii.

“Mheshimiwa spika, nimejiridhisha na kilichotokea. Madhara ya mwelekeo huu mpya katika haki jinai, ni kuchochea vitendo zaidi vya ukaidi kwa mamlaka za nchi na hivyo kujenga msingi wa vurugu. Hili halikubaliki katika utawala wa sheria. Mdharau mwiba mguu huota tende,” alisema..

Alisema kosa kama hilo lilitokea Kenya mwaka jana ambapo mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini humo, Alan Okengo (25) alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kulipa faini ya dola 2,000 (Sh milioni 3.2) kwa kumtukana rais wa nchi hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema pamoja na umri wake na uwezo wake mdogo wa kulipa faini, adhabu ilibaki palepale ili mkosaji ajutie kosa lake asije akarudia na jamii ijisikie salama.

Alisema pamoja na kutokuingilia mhimili wa mahakama na taratibu zake kitendo cha kuwapo kwa adhabu ambayo haijutiwi inakiuka dhana na dhamira ya adhabu.

Alisema kwa shauri la Emily, pamoja na kutiwa hatiani wakili wake aliomba mtuhumiwa alipe faini kwa kuwa hakusumbua mahakama na pia ni kosa lake la kwanza na ana familia.

Alisema wakati hakimu anamuuliza wakili wa serikali aliiachia mahakama kutoa maamuzi ambayo ilimpatia wakili wa utetezi maombi yake.

Mwakyembe alisema pamoja na maagizo ya serikali kwa DPP amewakumbusha waendesha mashitaka nchini kuwa macho na waweke mbele weledi na maslahi mapana ya taifa na kamwe wasiyumbishwe na mihemko ya kisiasa katika jamii.
Napenda niseme kwanza kabisa kwamba siungi mkono kitendo cha kumtukana mtu. Ila naomba kumuuliza Mh. Mwakyembe maswali yafuatayo kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao au sheria yeyote:

1. "Rais" ni taasisi au mtu binafsi?
2. Kama Rais ni taasisi, nini maana ya maneno "kumtukana Rais"?
3. Kuna tofauti yoyote kati ya vitendo hivi viwili:
(i) "Kumtukana Doe" na
(ii) "Kumtukana Rais Doe"?
5. Mlalamikaji mbele ya mahakama katika (i) na (ii) hapa juu anapaswa kuwa nani?

6. Mtu akiniita mimi "lofa"; Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania itamshitaki mtu huyo mahakamani bila mimi mweyewe kulalamika au kuonekana mahakamani?

7. Katika kesi za aina hii ambapo mwendeshaji wa mashtaka ni mwanasheria wa Serikali na mlalamikaji wake akiwa ni 'JMT' maana yake ni wananchi wote wa JMT au kiongozi/viongozi tu?

8.Nauliza hivi kwasababu nilidhani sheria ya makosa ya mitandaoni ililenga kuzuia matumizi ya chombo hicho kwenye masuala ya ugaidi na ujangili. Badala yake sasa linaonekana lengo jingine lilikuwa kudhibiti uhuru wa wananchi kusema au kutoa maoni yao!

Mimi sio mwanasheria wala sio mjuzi wa masuala haya, naomba kuelimishwa.
 
Hizi thread mpaka naogopa kucomment siku hizi!! Daaahh Tanzania nakupenda nchi yangu.. Naamini Mwenyezi Mungu bado anatupenda!!
 
WANGESEMA HIVYO KUHUSU MADHAMBI MENGINE KAMA MAUAJI YA ALBINO NA UFISADI KATIKA TAASISI NYETI ZA SERIKALI NINGEWAELEWA KIDOGO.
 
Napenda niseme kwanza kabisa kwamba siungi mkono kitendo cha kumtukana mtu. Ila naomba kumuuliza Mh. Mwakyembe maswali yafuatayo kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao au sheria yeyote:

1. "Rais" ni taasisi au mtu binafsi?
2. Kama Rais ni taasisi, nini maana ya maneno "kumtukana Rais"?
3. Kuna tofauti yoyote kati ya vitendo hivi viwili:
(i) "Kumtukana Doe" na
(ii) "Kumtukana Rais Doe"?
5. Mlalamikaji mbele ya mahakama katika (i) na (ii) hapa juu anapaswa kuwa nani?

6. Mtu akiniita mimi "lofa"; Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania itamshitaki mtu huyo mahakamani bila mimi mweyewe kulalamika au kuonekana mahakamani?

7. Katika kesi za aina hii ambapo mwendeshaji wa mashtaka ni mwanasheria wa Serikali na mlalamikaji wake akiwa ni 'JMT' maana yake ni wananchi wote wa JMT au kiongozi/viongozi tu?

8.Nauliza hivi kwasababu nilidhani sheria ya makosa ya mitandaoni ililenga kuzuia matumizi ya chombo hicho kwenye masuala ya ugaidi na ujangili. Badala yake sasa linaonekana lengo jingine lilikuwa kudhibiti uhuru wa wananchi kusema au kutoa maoni yao!

Mimi sio mwanasheria wala sio mjuzi wa masuala haya, naomba kuelimishwa.
Mkuu Shoctopus, maswali yako ni ya msingi sana. Lakini pia ukimsoma katika ya mistari waziri Mwakyembe, unaweza kuona kwamba sasa serikali yetu imechukua mwelekeo mpya kabisa, sina uhakika kama mwelekeo huu utatupeleka mahali pazuri au pabaya. Sina uhakika pia kama ni rais tuliyempigia kura atuongoze ndiye anatupeleka kwenye mwelekeo huo au ni matokeo ya wateule wake, wakiwemo akina Mwekyembe, kukosa kujiamini na kuanza kutenda kwa woga na kujipendekeza ili kujihalalisha katika ajira zao hizo za kuteuliwa.

Kuna watu walihoji iwapo kitendo cha muhimili wa bunge kuingilia uamuzi uliotolewa katika muhimili mwingine (mahakama) tena kupitia hukumu iliyotolewa mahakamani wakati inafahamika wazi kwamba, katika uamuzi wa shauri hilo mlalamikaji alitakiwa kukata rufaa kama alikuwa hakuridhishwa na hukumu hiyo! Mwakyembe anadai kwenye hukumu hiyo kulikuwa na influence ya kisiasa, lakini bunge nalo na yeye mwenyewe wameshughulika na kuligeuza suala hili kuwa mnyukano wa kisiasa kutaka kuonyeshana nani ni mwamba zaidi!

Kuna tafsiri kuwa Chadema/Ukawa wali-side na kijana aliyekutwa na hatia katika shauri hili. Sasa swali linaweza kuwa, Je, kitendo hicho cha Chadema (kama ni kweli) kuhakikisha kijana huyo ananusurika kwenda jela kwa kumchangia fedha kwa ajili ya kulipa faini hiyo ya Sh milioni 7 ndio kimesukuma bunge "kukengeuka" na kuingilia maamuzi ya mahakama wakati mlalamikaji, ambaye ni serikali, alikuwa ameridhika na uamuzi huo? Je, huu mwelekeo usipopigiwa kelele unawaweka katika mazingira gani mahakimu na majaji wanapotekeleza majukumu yao?

Mwanasheria msomi Dk Mwakyembe anasema adhabu inapotolewa kortini hulenga/hukusudia kumfanya mkosaji au watu wengine wasitende kosa kama hilo. Labda Mwakyembe na dhana hiyo ni sahihi, lakini wasomi wenzake waliishaanza kubaini kwamba adhabu kali anazozitamani hazijawa suluhisho la makosa ya jinai bali wanaona si adhabu peke yake zinazoweza kuwa suluhisho, isipokuwa ni pamoja na kujenga jamii zenye kufuata maadili mema pamoja na kuwa na hofu ya Mungu. Kwa bahati mbaya taifa letu linapungukiwa mno, tena kwa kasi kubwa, hazina ya maadili na hofu ya Mungu. Na hili la kugeuza suala la hukumu hii kuwa la kisiasa ni uthibitisho tu wa namna gani nchi yetu ina nakisi ya maadili na hofu ya Mungu!
 
Nimeshitushwa na habari hii kimsingi naona muhimili mmoja(bunge) unataka kupoka nguvu ya muhimili mwingine(mahakama) eti kwa matakwa ya kisiasa,naogopa kusema tunakoelekea kama taifa.
 
Shida ninayoiona katika watu wa Dunia yetu ya tatu ( Nchi masikini) ni kuwa watu wakipata nafasi za uongozi wanapoteza kabisa weledi wa kufikiria, kuamua na hatimaye kutenda. Badala ya kutenda kwa haki wao hutenda kwa namna ya kudhani kuwa wanampendeza aliyewateua/aliyewaweka madarakani matokeo yake wanawakosea wananchi na kurudisha maendeleo ya nchi nyuma. Wanatakiwa kufahamu kuwa chenye mwanzo mbaya mwisho wake huwa hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom