Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Lindi mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu ndogo wilayani Nachingwea. Waziri mkuu amewasili wilayani Nachingwea akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka
Oktoba 16. 2016 wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sokoine wilayani Nachingwea, mkoani Lindi, Waziri Mkuu alisema alishatoa maelekezo tangu Aprili, mwaka huu kwamba wanunuzi wa Korosho ni lazima watoe asilimia 25 ya malipo wanayotaka ili kuepuka tatizo la madalali kuingilia kati biashara hiyo
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi na Wakuu wote wa wilaya za mkoa huo wawahimize wakulima wapande miche mipya ya korosho kwa sababu mikorosho iliyopo imezeeka na haitoi mazao ya kutosha
Amesema kigezo kikuu cha ununuzi wa korosho hivi sasa ni idadi ya punje na kwa Ruangwa na Nachingwea, idadi inakuwa kubwa kwasababu punje zake ni ndogo
"Wenzetu wa Tandahimba walipanda miche mipya tangu miaka minne iliyopita kwa hiyo sasa hivi wanavuna korosho zenye ubora", ameongeza
Amempongeza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba kwa uamuzi wake wa kuvunja mfuko wa wakfu wa korosho (CIDTF) na akamtaka afute mifuko kama hiyo kwenye mazao mengine kama Katani, Chai na Kahawa kwani inafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na bodi za mazao hayo.
Chanzo : ITV channel