Tabora: Serikali yamsaka muuguzi aliyebaka mgonjwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wizara ya Afya inafuatilia sakata la muuguzi anayedaiwa kumbaka msichana mgonjwa na kisha kukimbia kusikojulikana.

Akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Igunga na viongozi wa sekta ya afya mkoa wa Tabora, Naibu katibu mkuu (Tamisemi-Afya), Dk Dorothy Gwajima alisema lengo ni kuona haki inatendeka.

“Pia lazima kurudisha heshima ya sekta hiyo na hospitali ya wilaya ya Igunga,” amesema.

Ameeleza kuwa anayedaiwa kufanya tukio hilo ni mtu mmoja na hawezi kuchafua sifa ya sekta nzima ya afya na kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya mhusika.
Akimzungumzia mtumishi mwingine wa hospitali hiyo, anayedaiwa kuomba rushwa ya Sh200,000 na kukamatwa na Takukuru ambapo ana kesi mahakamani,alisema hilo liwe funzo kwa watumishi wa sekta ya afya akisema hospitali sio pango la kuomba rushwa.

Ameonya kuwa watumishi wanapokabiliwa na mkono wa sheria kwa kufikishwa mahakamani inakuwa si mwisho kwani watakumbana na mabaraza yao ya kitaaluma pamoja na kiutawala.

Naye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, alisema tayari amemsimamisha kazi muuguzi anayekabiliwa na kesi ya rushwa mahakamani, akisubiri sheria ichukue mkondo wake.

Kuhusu mtumishi anayedaiwa kumbaka msichana mgonjwa alisema kuna hatua zinaendelea na kwamba hawezi kuzisema ni hatua gani kwa sasa. Naye Katibu tawala mkoa wa Tabora, Msalika Makungu aliwataka watumishi wa sekta ya afya kutambua dhamana waliyo nayo katika kuwahudumia wananchi na kuwataka kuwa mfano mzuri kwa jamii.

Chanzo: Mwananchi

Imeelezwa kuwa muuguzi mmoja wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Anatuhumiwa kumbaka msichana wa miaka 16 (Jina linahifadhiwa), mkazi wa Mtaa wa Buyumba, Kata ya Igunga Mjini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mganga Mkuu Wilaya ya Igunga, Dkt. Ruta Deus amesema binti huyo alikuwa akimuuguza mama yake aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo.

Ni kweli tukio hilo lipo na hiyo si mara ya kwanza kwani siku za nyuma muuguzi huyo (jina tunalo) akiwa Kituo cha Afya Tarafa ya Igurubi alifanya tukio kama hilo, hivyo hii ni mara ya pilli na huo ni ukiukwaji wa taratibu na kanuni za kiutumishi,” alisema Dkt. Deus.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo, Mamamzazi wa msichana huyo, Wande Salum (42) aliyekuwa amelazwa wodi no. 3, alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 10, mwaka huu, saa 4 usiku.

Wande alidai kuwa muuguzi huyo alifika katika wodi hiyo kuangalia hali yake na baada ya kumuona alimwambia ambadilishe dawa na alimuomba aondoke na mwanae aliyekuwa akimuuguza na walipofika ofisini alimchoma sindano ya usingizi kisha kumbaka kuanzia saa 4 usiku hadi saa 8.

Bi. Wande amesema baada ya kuona muda unaenda pasipo mwanawe kurudi wodini, Aliomba msaada kwa baadhi ya wagonjwa wenzake wenye hali nzuri wamsaidie kumtafuta.

Alidai kuwa baadhi ya manesi waliokuwa zamu walipopata taarifa hiyo, waliungana na baadhi ya wagonjwa kumtafuta mwanawe na walimkuta eneo la nyasi wanakofulia nguo kina mama akiwa hajitambui, huku akivuja damu sehemu za siri kutokana na kubakwa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.

Aidha mama huyo alisema kitendo alichofanyiwa mwanawe ni cha kinyama na hakipaswi kufumbiwa macho, huku akiomba vyombo vya dola kumsaka muuguzi huyo apatikane na kufikishwa mahakamani.

Baadhi ya kina mama wanaokwenda kutibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Rehema Julias na Sada Mwinamila, walisema hivi sasa wameingiwa na hofu kutokana na kitendo hicho na kuiomba Serikali kutofumbia macho suala hilo.

Mganga Mkuu amesema kuwa tayari suala hilo liko polisi na wao wanaendelea kuchukua hatua dhidi ya muuguzi huyo ambaye mpaka sasa hapatikani kwa njia ya simu na hajulikani yupo wapi.

Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Barnabas Mwakalukwa, Walipoulizwa kuhusu tuhuma hizo dhidi ya muuguzi huyo, walisema bado hawajapokea taarifa hizo.

CHANZO: Mtanzania

Baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania, (TNMC) limeisimamisha kwa muda wa miezi mitatu leseni ya muuguzi, aliyemchoma sindano ya usingizi na kisha kumbaka kuanzia saa nne usiku hadi saa nane msichana mwenye umri wa miaka 16, aliyekuwa akimuuguza mama yake, katika hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania limeviomba vyombo vya ulinzi na usalama nchini kumkamata popote alipo muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, Damian Mgaya (41) aliyetoroka Hospitalini hapo kufuatia tuhuma za kumbaka binti huyo wa miaka 16 ili afikishwe kwenye vyombo vya Sheria

Inaelezwa kuwa mara baada ya kumaliza kumbaka binti huyo aliamua kumtupa eneo la kufulia nguo kwenye nyasi akiwa hajitambui na kumwagia maji mwili mzima.


Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 18, 2019, na Msajili wa Baraza hilo Agnes Mtawa na kusema kuwa baada ya mtumishi huyo kurejeshwa kazini, alihamishwa kutoka kituo cha Afya cha Igurubi na kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Inaelezwa kuwa muuguzi huyo Damiani Samson Mgaya, mnamo mwaka 2017, akiwa katika kituo cha Afya cha Igurubi , wilayani humo alishawahi kufanya tukio kama hilo, ambapo alipelekwa polisi na kisha mahakamani na hatimae aliachiwa huru na kurejeshwa kazini mwaka 2018.

Kufuatia mtiririko wa matukio hayo kufanywa na muuguzi huyo, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, (TNMC) limeamua kumchukulia hatua ya kusimamisha leseni yake ya kutoa huduma za ukunga na uuguzi popote nchini Tanzania kwa muda wa miezi mitatu.

Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo amethibitisha tuhuma hizo na kusema kesi imefikishwa katika kituo cha polisi.

“Ni kweli tukio lipo na sio mara ya kwanza siku za nyuma Mgaya akiwa kituo cha afya cha Tarafa ya Igurubi alifanya tukio kama hilo, hii ni mara ya pili na huu ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kanuni za kiutumishi”- Dkt.Ruta Deus, Mganga Mkuu wa Wilaya.
 
Pole kwa mgonjwa alifanyiwa unyama, ila naona jamaa uvumilivu ulimshinda igunga kuna watoto wazuri balaa!!
 
Wizara ya Afya inafuatilia sakata la muuguzi anayedaiwa kumbaka msichana mgonjwa na kisha kukimbia kusikojulikana.

Akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Igunga na viongozi wa sekta ya afya mkoa wa Tabora, Naibu katibu mkuu (Tamisemi-Afya), Dk Dorothy Gwajima alisema lengo ni kuona haki inatendeka.

Msichana alikuwa mgonjwa au mama yake ndiye alikuwa mgonjwa? Hizi habari umiza kichwa
 
Back
Top Bottom