Serikali yamsaidia Sumaye

Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
10,381
4,355
Serikali imemsaidia Mh Sumaye kwa kuwaondoa wavamizi waliovamia shamba lake huko Mabwepande kwa kuwaamuru kuondoka mara moja na kuacha kuvamia maeneo ya watu wengine. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa DSM.

Chanzo: Mwananchi
 
Haijamsaidia ila ni jukumu la serikali kulinda amani na na kuzuia uonevu kwa mtu yeyote. haijalishi huyo mtu yuko chama gani lazima serikali imtetee.
 
Kwahiyo tunakubali kuwa serikali ya sasa inatekeleza wajibu wake bila kuangalia itikadi za vyama? Si ndio? Basi inastaili kupongezwa!....Kwa kuwa ingeamua ikanyamazia tu hilo suala sijui mzee Sumaye angekimbilia wapi!?

Hii iwe somo kuwa serikali ya CCM haina chuki na upinzani....Bali ipo kuhudumia wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.
 
Wasingefanya hivyo nasi tungeenda Kiwangwa kuvamia eka 300 za mfalme mstahafu.
 
Unaleta siasa kwenye utekelezaji wa sheria?! Hapo serikali imetekeleza majukumu yake na sio msaada.
 
Kwahiyo tunakubali kuwa serikali ya sasa inatekeleza wajibu wake bila kuangalia itikadi za vyama? Si ndio? Basi inastaili kupongezwa!....Kwa kuwa ingeamua ikanyamazia tu hilo suala sijui mzee Sumaye angekimbilia wapi!?

Hii iwe somo kuwa serikali ya CCM haina chuki na upinzani....Bali ipo kuhudumia wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.
Big up mkuu.
 
huyu sadiki naye ni jipu sumaye anamiliki mashamba kila kona ya nchi hii kwanini hao wananchi wafukuzwe hapo
 
Hizi sifa ndio zinaifanya serikali ionekane ya kijuha. Kwani kusimamia sheria kwa vile inamuhusu Sumaye ni MSAADA?
Tafsiri yake hapo ni kuwa haina utaratibu wa kutenda haki kwa baadhi ya makundi hasa yale yanayoikosoa
 
Ni jukumu lake kulinda usalama wa raia na mali zao!
ni haki yake kikatiba kulindwa!
 
Hizi sifa ndio zinaifanya serikali ionekane ya kijuha. Kwani kusimamia sheria kwa vile inamuhusu Sumaye ni MSAADA?
Tafsiri yake hapo ni kuwa haina utaratibu wa kutenda haki kwa baadhi ya makundi hasa yale yanayoikosoa
Waandishi wetu,waandishi wetu waandishi wetu lakini baadhi tu ndo wanaangusha hiyo tasnia...sidhani kuwa serikali ilienda kuwatoa wavamizi kwa kusema tunaenda kumsaidia Sumaye
 
Kwahiyo tunakubali kuwa serikali ya sasa inatekeleza wajibu wake bila kuangalia itikadi za vyama? Si ndio? Basi inastaili kupongezwa!....Kwa kuwa ingeamua ikanyamazia tu hilo suala sijui mzee Sumaye angekimbilia wapi!?

Hii iwe somo kuwa serikali ya CCM haina chuki na upinzani....Bali ipo kuhudumia wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama.
Serikali imeamua kuwasaidia wananchi wasiingie hasara ya kubomolewa. Maana wangetolewa tu hakuna namna. Sasa serikali Kuruhusu wavamie shamba la mtu ni sawa na kuona wananchi wanajenga mabondeni bila kuwazuia
 
Halafu na hata wananchi nao naona kuna tatizo sijui la elimu, sijui ni nini ? Sasa hivi tu watu wanabomolewa kujenga maeneo yasiyoruhusiwa halafu bado mtu anaenda kuvamia eneo lisiloruhusiwa ?! Basi kuna shida ya uelewa wa wananchi.
 
naona serikali iliposikia Sumaye akisema hana wasiwasi ana document zote halali..imeogopa kula faini zaidi mahakamani.
 
Niliisubiri siku kama hii hatimaye imewadia, asante mungu.Kwahiyo CCM wanamlipa fadhila Sumaye kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuijumu UKAWA,Mbowe aidha ni mshirika wa mpango huu au ni mchanga sana wa siasa za Africa kwa kumkubalia Sumaye kujiunga UKAWA tena bila vetting yoyote na kumpa majukumu ya kuongoza timu ya kampeni.
 
Back
Top Bottom