Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Kumbe tuna uwezo mkubwa wa kukusanya kodi:
Na Nyakongo Manyama –MAELEZO-Dar es salaam
22.2.2016
Serikali imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwezi huu tofauti na zilizokuwa zikukusanya hapo awali za bilioni 850 kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuzielekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha mwezi Februari mwaka huu.
Amesema kuwa kati ya fedha hizo ,sekta ya elimu imepewa shilingi bilioni 18.7 kwa ajili ya utekelezaji wa utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali hadi kidato cha Nne ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya ada,chakula pamoja na ruzuku.
Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es salaam imeongezewa shilingi bilioni 2 ili kupanua uwezo wa udahili kama Rais alivyoahidi katika mkutano wake na Wazee wa Mkoa huo.
Aidha, Dkt. Likwelile amesema kuwa ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao ,Wizara imetoa shilingi Bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Kati ya fedha hizo wakufunzi wamepatiwa shilingi milioni 431.6 walimu walio masomoni wametengewa shilingi milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli.
Ameongeza kuwa fedha nyingine kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Umma , ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa shilingi bilioni 842.1 na Mifuko ya hifadhi za Jamii zimetolewa shilingi bilioni 81.13.
Fedha kwa ajili ya shughlui mbalimbali za maendeleo zimetolewa kiasi cha Shilingi Bilioni 166.2 ambapo chuo kipya cha Sayansi kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mlunganzi la kimepatiwa Shilingi Bilioni 18 na Kiasi cha Shilingi Bilioni 13.6 kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu.
Mamlaka ya Elimu (TEA) imepatiwa shilingi Bilioni 23.078, Mpango wa Maji vijijini Bilioni l7.1, maendeleo ya ujenzi wa barabara zimetolewa shilingi bilioni 58.8, miradi ya umeme vijijini zimetengwa shilingi bilioni 20.2, Reli shilingi bilioni 2.034, Serikali za mitaa zimepatiwa shilingi bilioni 4.5, na Mahakama zimepatiwa shilingi bilioni 12.3.
Naye Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amesema kuwa makusanyo yameongeza kutoka shilingi trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba hadi kufikia trilioni 1.79 kwa mwezi Januari