Serikali yakipa Kiwanda cha Dangote siku 7 kuwasilisha taarifa zake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali ya Tanzania imetoa siku saba kwa kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote kilichopo Msijute, Mtwara kuwasilisha taarifa ya utendaji wake katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili kwenda na matakwa ya sheria na taratibu za nchi.

Hayo yameelezwa jana Ijumaa Septemba 27, 2019 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji, Angellah Kairuki wakati akizungumza na wafanyabiashara mkoani Lindi baada ya kubaini uongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Aliko Dangote kutowasilisha taarifa hizo katika kipindi cha miaka mitatu.

"Nimesikitishwa sana na suala hili la kutopeleka taarifa zenu TIC na mnajua kuwa jambo hili ni la kisheria, kuanzia sasa nawapa wiki moja hakikisheni taarifa hizo zinawasilishwa haraka," amesema Angellah.

Waziri huyo alieleza hayo akiwa ameambatana na naibu Waziri wa Ardhi, Angela Mabula ambao kwa pamoja walitembelea mgodi wa madini ya uno uliopo kijiji cha Matambalale kusini mwa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Meneja wa kampuni ya Lindi Jumbo inayochimba madini hayo, Paul Shauri amesema mgodi utajengwa kwa miezi tisa na wanatarajia kuwekeza zaidi ya dola milioni 30 za Marekani, sawa na Sh69 bilioni.

Akifafanua zaidi Angela ameziagiza Halmashauri zote kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi katika vijiji vyenye maeneo ya uwekezaji.

"Hakuna sababu ya mwekezaji kuanza kuhangaika na mambo madogo kama hayo ambayo yanampotezea wakati, ni lazima halmashauri zijipange ili kumwekea mwekezaji mazingira mazuri avutiwe kuwekeza" amesema Angela.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa ameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara za wilaya hiyo ili kuchochea mazingira ya uwekezaji wa kampuni zilizoonyesha dhamira ya kuwekeza.
 
E
Serikali ya awamu ya tano mmeanza tena kumfuatafuata huyo mwekezaji, ataondoka, mlianza kukamata magari yake yote kila yanapopita, hamjatosheka mpaka muwapotezee ajira watanzania hapo kama mlivyofanya kwa kampuni ya tumbaku ya Tltc.
 
Hi nchi neema tupu Sasa madini ya UNO ndo yakoje? Mliosoma kemia hebu tuwekeeni periodic table ya kiswahili
 
Serikali ya awamu ya tano mmeanza tena kumfuatafuata huyo mwekezaji, ataondoka, mlianza kukamata magari yake yote kila yanapopita, hamjatosheka mpaka muwapotezee ajira watanzania hapo kama mlivyofanya kwa kampuni ya tumbaku ya Tltc.
Nakuambiaje uwekezaji wa kiwanda hiki ni juhudi za enzi ya JK. Magu lazime "amjambishe" mwekezaji hadi na yeye "alambe unga" kupitia uwekezaji huu.
 
Serikali ya awamu ya tano mmeanza tena kumfuatafuata huyo mwekezaji, ataondoka, mlianza kukamata magari yake yote kila yanapopita, hamjatosheka mpaka muwapotezee ajira watanzania hapo kama mlivyofanya kwa kampuni ya tumbaku ya Tltc.
Watu bana kama aliwekeza kimaangumashi lazima afuate sheria za nchi hili sio shamba la bibi
 
Serikali ya awamu ya tano mmeanza tena kumfuatafuata huyo mwekezaji, ataondoka, mlianza kukamata magari yake yote kila yanapopita, hamjatosheka mpaka muwapotezee ajira watanzania hapo kama mlivyofanya kwa kampuni ya tumbaku ya Tltc.
Hajotoa taarifa kwa miaka 3 kinyume cha sheria, ametakiwa afanye hivyo. Tatizo nini hapo ?!
 
Yeye mbona hanaga wizara maalum?
Serikali ya Tanzania imetoa siku saba kwa kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote kilichopo Msijute, Mtwara kuwasilisha taarifa ya utendaji wake katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili kwenda na matakwa ya sheria na taratibu za nchi.

Hayo yameelezwa jana Ijumaa Septemba 27, 2019 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji, Angellah Kairuki wakati akizungumza na wafanyabiashara mkoani Lindi baada ya kubaini uongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Aliko Dangote kutowasilisha taarifa hizo katika kipindi cha miaka mitatu.

"Nimesikitishwa sana na suala hili la kutopeleka taarifa zenu TIC na mnajua kuwa jambo hili ni la kisheria, kuanzia sasa nawapa wiki moja hakikisheni taarifa hizo zinawasilishwa haraka," amesema Angellah.

Waziri huyo alieleza hayo akiwa ameambatana na naibu Waziri wa Ardhi, Angela Mabula ambao kwa pamoja walitembelea mgodi wa madini ya uno uliopo kijiji cha Matambalale kusini mwa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Meneja wa kampuni ya Lindi Jumbo inayochimba madini hayo, Paul Shauri amesema mgodi utajengwa kwa miezi tisa na wanatarajia kuwekeza zaidi ya dola milioni 30 za Marekani, sawa na Sh69 bilioni.

Akifafanua zaidi Angela ameziagiza Halmashauri zote kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi katika vijiji vyenye maeneo ya uwekezaji.

"Hakuna sababu ya mwekezaji kuanza kuhangaika na mambo madogo kama hayo ambayo yanampotezea wakati, ni lazima halmashauri zijipange ili kumwekea mwekezaji mazingira mazuri avutiwe kuwekeza" amesema Angela.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa ameiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara za wilaya hiyo ili kuchochea mazingira ya uwekezaji wa kampuni zilizoonyesha dhamira ya kuwekeza.
 
Yaani hii nchi sijui kupau mbele chake ni kipi?

Back
Top Bottom