Serikali yakamilisha upembuzi wa reli ya SGR Mtwara–Bamba Bay

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC), imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kutoka Mtwara-Mbambabay pamoja na matawi yake ya Liganga na Mchuchuma yenye jumla ya urefu wa kilometa 1,000.

Taarifa hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, Bungeni jijini Dodoma, aliyetaka kujua kama Serikali haioni haja ya kuanza upembuzi wa ujenzi wa reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Kusini, hususan ikizingatiwa maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Gesi Asilia (LNG).

Akijibu swali hilo, Kihenzile amesema kuwa kwa sasa Serikali inaendelea na juhudi za kutafuta rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa, ikiwemo kutumia utaratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP).

Aidha, amesema kwa upande wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Mtwara, Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia mpango kabambe wa East Africa Railway Master Plan imetambua umuhimu wa kipande hicho cha reli kitakachounganisha Bandari ya Dar es Salaam na Bandari ya Mtwara, kutokana na mchango wake katika kukuza uchumi, maendeleo ya kijamii na kuimarisha mtangamano wa kikanda.

Hata hivyo, Naibu Waziri huyo amesema reli hiyo bado haijaingizwa katika mpango wa utekelezaji kwa kutumia fedha za Serikali kwa sasa, kutokana na Serikali kuendelea na ujenzi wa reli ya SGR pamoja na utekelezaji wa miradi mingine ya kimkakati inayohitaji rasilimali kubwa za kifedha kwa wakati mmoja.

Kutokana na hali hiyo, Kihenzile ametoa wito kwa wawekezaji wa sekta binafsi na taasisi za kifedha kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya reli, ikiwemo reli ya kusini, ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuboresha miundombinu ya usafirishaji nchini.

Ningekuwa Mimi ndo Rais wa nchi hii - Chuma cha Liganga ndo kingezalisha mataluma ya hii Reli! Yaani nisingeweza kununua chuma toka nje- ili niweze kusafirisha Chuma nje ya nchi😁 Tuna Kila kitu cha kuwezesha jambo hili 100%
 
Siku nyingi Wachina wametaka kuwekeza kwenye hiyo reli ili wapate malighafi chuma.
 
Mradi wa bongo aifatagi watu ila watu ndo tunafata mradi kwel hela kwa hela hapo mjenzi mchina na mchimbaji atakua mchina na mteja ni mchina na atapanga bei lkn mkataba utakua wa miaka mia kwa malipo ya mradi na mia kwa uwekezaji yani tunamaliza deni na mradi umekufa chuma kimeondoka chote tunaenda kubuni mradi wa kufanya kwenye maeneo na rais anaenda tena kuzindua mradi mpya kutokana na maeneo hayo na kusema tumechezewa sana na uongozi uliopita sasa maendeleo yetu sote wana mbamba bay wanashangilia sana wananchi vizazi vya wakandarasi wa kichina kibao wakina lin ping haule na dong fen mapunda
 
Back
Top Bottom