Serikali yakamata kiwanda bubu cha kufungashia sukari eneo la Soweto Mbeya

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Serikali mkoani Mbeya imekamata kiwanda bubu cha kufungasha sukari, kikiwa kwenye makazi ya watu katika eneo la Soweto jijini Mbeya ambacho kinatuhumiwa kufungasha sukari katika mifuko midogo yenye ujazo wa kati ya nusu kilo na kilo moja na kisha sehemu ya sukari hiyo kuiuza nje ya nchi na nyingine kusambazwa mitaani na kuwauzia wananchi kwa bei kubwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Mbeya,Nyerembe Munasa Sabi akiongozana na askari wa Jeshi la Polisi ameingia mitaani kutekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kuwasaka wafanyabiashara wanaoficha sukari, na ndipo akafanikiwa kubaini kiwanda bubu cha kufungasha sukari kinachodaiwa kufanya kazi hiyo kinyume cha sheria na ndipo akaingiwa na hofu kuwa huwenda kiwanda hicho kinafungasha sukari iliyokwisha muda wake na kuwauzia wananchi.

Baada ya kukamatwa,mmiliki wa kiwanda hicho ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa sukari jijini Mbeya, Bushir Sanga yakaibuka malumbano makali dhidi yake na Mkuu wa wilaya kuhusu aina na uhalali wa mifuko inamofungashiwa sukari hiyo.

Baada ya kujiridhisha kuwa mfanyabiashara huyo hana kibali cha kufungasha bidhaa hiyo kutoka kwenye viwanda vya sukari vya ndani ya nchi, Mkuu huyo wa Wilaya akaamuru mfanyabishara huyo akamatwe ili akatoe maelezo polisi.
 
Malawi wana Sukari ya kutosha na nyingi ilikua inatoka huko kwa njia za panya pamoja na Zambia Nchi gani tupeleke hii sukari guru mkuu..
 
Anasafirisha sukari kwenda nje ya nchi! Acheni kukurupuka! Zambia na Malawi sukari ni bei rahisi miaka yote! Tz haijawahi kuwa na bei ya chini ya sukari kuliko Zambia au Malawi, alichofanya ni kununua sukari malawai/ Zambia akaleta tz kwa kuwa mifuko ya kule tofauti akatafuta mifuko ya tz kosa lake kaingiza sukari kwa njia ya panya ambayo hata Mimi kama mfanyabiashara opportunity kama hiyo ningefanya ila mfute kauli za mizuka kusema sukari inatoka tz inaenda zambia!/Malawi!
 
hao ilovo Nchi za kusini huko hawajafanya ujanja ujanja kama hapa kwetu toka tunakua sukari Malawi..Zambia na Zimbabwe haizungumziwi ni bidhaa inayopatikana tena ina Ubora haswa hapa kwetu hii Sukari Guru kila siku hadith za uwongo uwongo tuu...
 
kama serikali inataka sukari iwepo wasitoe vibali kwa hao watu 12 pekee muruhusu kwa hiyo miezi mitatu yeyote alete muone kwa jinsi itavyojaa kama kuna watu wataweka store na kodi ipungue Zambia ni bei ndogo sana Zimbabwe ni usd 30...
 
acheni uongo!acheni uongo!mnafakiri mnasaidia mungu wenu wa ccm,kumbe ndio mnampunguzia credibility mbele ya wasomi...hizi propaganda wafenyieni semi-literates!
 
ahaaaaa ahaaaaaa nimecheka sana anapeleka nchi za nje?
ni nchi gani hiyo naomba mtutajie kama ni Zambia na Malawi sisi ndio tunaowategemea
 
wataelewa tu hakuna namna, serikali ya Magu hujanja ujanja hakuna
 
acheni uongo!acheni uongo!mnafakiri mnasaidia mungu wenu wa ccm,kumbe ndio mnampunguzia credibility mbele ya wasomi...hizi propaganda wafenyieni semi-literates!
Mkuu watu wanajitahidi kulinda vibarua vyao wanamuunga mkono bosi wao wasijekutumbuliwa, wewe huoni taarifa za kufichua sukari zimeongeza, kila pembe kuna matani ya sukari yalifichwa
 
Sukari za mia mia napeleka nje ya nchi??? Mbeya tushazoea hiyo mifuko midogo midogo haijaanza kufungwa leo,MIZUKA HII
 
Mbeya sukari ni kama maji baharini yani sukari ya kilombero sijui kagera hawaijui n sukari bora kabisa toka malawi na zambia huyo kufunga kawaida aende mwanjelwa pale stendi ya zamani atakuta jamaaa wanauza sukari ya paketi
 
Kuna watanzania wapo Dar hawajui uhalisia wa maisha sehemu nyingine, kuna wananchi wa mkoa wa mbeya tangu wazaliwe hawaijui sukari ya Tanzania wao ni ya zambia au Malawi kwa hiyo huwezi peleka sukari Zambia au malawi bali kuna watanzania wengi tu hufanya biashara hiyo kimagendo, huyo mfanyabiashara itakuwa alinunua Malawi ili auze huku kwa vifungashio vya huku, hapo atakuwa na kesi tofauti
 
DC amekurupuka na hajui wanatafuta nini mitaani! Wamedakia agizo bila kuelewa JPM alikuwa anajisafisha maana hii drama ameitengeneza mwenyewe! Sasa anahaha kujisafisha! Shortage ya sukari ameitengeneza yeye na anajua hilo! Inabidi azungukee weee lakini atuombe radhi watanzania! Hakuna namna
 
Back
Top Bottom