Zakaria kasalimu amri, bado kesi ya kuuwa na kujerui mfanyakazi wa TISS.View attachment 1004119
SERIKALI imerejesha mali zote 10 za Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Mwanza (Nyanza), zilizokuwa zimeporwa na kuhujumiwa na baadhi ya watu binafsi pamoja na wafanyabiashara kwa kujiuzia kwa bei ya kutupa.
Mali iliyokuwa imebaki ni jengo la zamani la Kampuni ya Uchukuzi Mwanza (Kauma), lililopo Barabara ya Stesheni kiwanja namba 242, kitalu T, lenye eneo la gereji pamoja na kituo cha mafuta. Mali hiyo imerejeshwa kwenye chama hicho kutoka kwa mfanyabiashara Antonia Zakaria na Timothy Kilumile, ambao walikuwa wakimiliki kinyume na taratibu tangu mwaka 2002.
Hatua hiyo imefuatia Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, kutoa kibali cha kuruhusu kesi hiyo ya uhujumu uchumi ya mwaka 2018, kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa Mwanza badala ya Mahakama ya Mafisadi. Baada ya DPP kutoa ruhusu hiyo, watuhumiwa walisomewa mashtaka mbele ya hakimu Gwae Sumaye na kutiwa hatiani kwa
makosa matatu ya kula njama na kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia hasara serikali na kuamuriwa kulipa gharama ya Sh. milioni 54 baada ya kukiri makosa yao.
Aidha, DPP alimwagiza Meneja wa ushirika huo kuhakikisha mikataba yote ya wapangaji walioko katika majengo hayo ambayo serikali imeyataifisha waiangalie kama walikuwa wanalipa shilingi ngapi na ni ya muda gani na kuanzia muda ule wapangaji wote hawatamlipa tena Antonia, badala yake watalipa fedha hizo kwa serikali. Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Chama Kikuu Cha Ushirika Nyanza, Juma Mokiri, Alisema agizo la Rais John Magufuli la kutaka mali mbalimbali za chama hicho kurejeshwa limerejesha