Serikali yaidhamini TANESCO mkopo wa Sh408 bilioni

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862
Wadau,
Katika kuhakikisha tatizo la umeme linakuwa ndoto serikali yetu sikivu imevunja ukimwa kwa kuwazawadia Tanesco Fungu.


SERIKALI imekubali kulidhamini Shirika la Umeme nchini(Tanesco) ili liweze kupata mkopo wa Sh408 bilioni utakaosaidia shirika hilo kujiendesha.

Kufikiwa kwa uamuzi huo wa serikali kutamaliza mvutano uliokuwapo kati ya Bodi ya Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini ambao ulisababisha Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Jenerali Mstaafu Robert Mboma kumwandikia aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja akihoji sababu za kutokutekelezwa kwa agizo la Rais Jakaya Kikwete la kulipatia shirika hilo Sh408 bilioni kwa ajili ya kujiendesha.

Barua ya Mboma ya Machi 20, mwaka huu kwenda kwa Ngeleja, ambayo gazeti hili ilifanikiwa kuiona, ilisema mnamo Machi 8, mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza Tanesco ipewe haraka mkopo wa Sh408 bilioni lakini akasema hadi sasa amri hiyo ya Amiri Jeshi Mkuu haijatimizwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, William Mhando alisema , sasa mkopo huo uko mbioni kupatikana.

Mhando alisema mpaka sasa bado hawajapata mkopo huo lakini wako kwenye mazungumzo ya mwisho ya kuupata baada ya serikali kukubali kutoa dhamana yake.

"Ndiyo tunamalizia mazungumzo ili tuweze kupata mkopo na serikali imeshakubali kutudhamini kilichopo sasa ni kubadilishana nyaraka na Citi bank," alisema Mhando.

Kuhusu hali ya umeme nchini Mhando alisema, maji yaliyopo hivi sasa yanaweza kusaidia umeme upatikane hadi Agosti mwaka huu.

Alisema kutokana na mvua kutonyesha kwa wingi katika bwawa kama la Mtera lina maji kidogo na limebakia mita 1.36 kufikia mwisho.

"Bwawa la Mtera linatakiwa liwe na mita za ujazo 698.5 na sisi tunaruhusiwa kutumia hadi kufikia mita 690.0 hivi sasa liko na mita za ujazo 691.36 hivyo tumebakiwa na mita 1.36 ambazo ni kidogo," alisema Mhando.

Mhando alisema shirika hivi limeweza kukusanya kiasi cha Sh60 bilioni kutoka serikalini kati ya Sh86 bilioni walizokuwa wakizidai.

Wakati huohuo mtambo wenye uwezo wa kufua umeme wa megawati 50 wa kampuni ya Symbion Power uliofungwa mkoani Arusha unatarajiwa kuanza kazi katika wiki mbili zijazo katika mpango wa ubia katika ya sekta za umma na binafsi wenye lengo la kulinasua taifa kutokana na upungufu wa nishati ya umeme.

Akithibitisha taarifa hizi jana, Ofisa mtendaji mkuu wa Symbion Power, Paul Hinks alisema kwamba, ujenzi wa mtambo huo wa kuzalisha megawati 50 mjini Arusha umeshakamilika na kwamba kampuni yake ilikuwa inamalizia tu maunganisho katika gridi ya taifa kabla mtambo haujaanza kazi.

“Mtambo utaanza kufanya kazi katika wiki mbili zijazo au mapema zaidi …….hivyo ndivyo nionavyo kwa sasa,” mkuu huyo wa Symbion alisema.

Na Boniface Meena
sosi: Serikali yaidhamini Tanesco mkopo wa Sh408 bilioni
 
Wasiwasi wangu ni matumizi ya hizo hela, zinaweza kuishia kulipa posho nk na tatizo la umeme likabaki palepale. Mbona Tanesco wanakusanya zaidi ya 70 bil kwa mwezi zinaenda wapi? Hivi matumizi yao kwa mwezi ni kiasi gani? Ni wakati sasa kwa Tanesco kubebwa na kubebeka, vinginevyo wataendelea kuwa mzigo kwa Serikali na walipa kodi licha ya kupandishiwa bei ya umeme hivi karibuni.



 
This is the familiar and typical scenario:

Wata-default huo mkopo with their crazy & stupid unproductive 'investment' na mwisho wa siku wavuja-jasho kupitia serikali, tutaishia kulipishwa hilo deni.
 
subiri sasa tuone nyumba zikatavyonunuliwa kwa bei mbaya dar

hizi pesa hizi sijui.....
 
Wasiwasi wangu ni matumizi ya hizo hela, zinaweza kuishia kulipa posho nk na tatizo la umeme likabaki palepale. Mbona Tanesco wanakusanya zaidi ya 70 bil kwa mwezi zinaenda wapi? Hivi matumizi yao kwa mwezi ni kiasi gani? Ni wakati sasa kwa Tanesco kubebwa na kubebeka, vinginevyo wataendelea kuwa mzigo kwa Serikali na walipa kodi licha ya kupandishiwa bei ya umeme hivi karibuni.


Zinaenda kwa EL na washirika wake. Kwani umesahau malipo ya Dowans/Richmond?
 
Symbion power in Arusha...!!!??? Hahaaaaaa i got the point now..... wtz mtaliwa na kuzungushwa hadi mkome....
Hivi hiiiiiiii TAnesKO ina tatizo gani? hivi hiii TAnesKO kila mwezi Capacity charges pekee monthly ni Tshs 3500 hivi tena za bure ss tupo kimya bado wanashindwa kujiendesha, juzi juzi Feb wamepandisha gharama za umeme na umeme bado unakatwa as usual na bado wanashindwa kujiendesha... Leo serikali inaidhamini Tshs 408 billions... na hizi tutalipa ss kupitia gharama za umeme... na bado shirika litashindwa kujiendesha.... Na huu huu umeme ndio umepandisha gharama za maisha....
TAnesKO ni JANGA LA TAIFA i declare kuliko mashirika yote combined yaliotutia hasara kubwa kubwa....
 
watajiendesha vipi wakati viwavi wa magamba wamejaa kula kila kiasi chochote kiingiacho TANESCO? Walikuwa wanne IPTL, SONGAS, AGGRECO, na DOWANS/Si-mbioni. Sasa wameongezwa unadhani fedha hizo zitapona?
 
yaani hapo namuona MD wa tanesco anavyokenua... Kama kuna hekalu yake ambayo hajaimalizia basi huu ndio wakati wenyewe hela ndio hiyoo....bahati mbaya ngeleja hayupo maana lazima jamaa angekata na ya kwake
 
Kwa miezi miwili sasa, wakazi wengi wa Dar tunafurahia umeme bila matatizo wala mgao, kama kuna sehemu za dar zina matatizo basi ni mambo ya kiufundi zaidi na si uzembe wa mgao.
 
Kwa miezi miwili sasa, wakazi wengi wa Dar tunafurahia umeme bila matatizo wala mgao, kama kuna sehemu za dar zina matatizo basi ni mambo ya kiufundi zaidi na si uzembe wa mgao.

Hata sisis PEMBA katika maeneo yenye umeme ni wa uhakika, natumai mabilioni haya yataongeza ufanisi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom