Unampongeza mtu aliyetengeneza tatizo akaja kuliondoa mwenyewe? MF mtu anakulisha sumu, baada ya kuzidiwa anakupeleka hospitali unatibiwa je, ukipona unatakiwa umshukuru kwa kukupeleka hospitali au umsitaki kwa kukulisha sumu? Pili kama wataondoa hizo tozo za miamala ya kielektroniki pia watuonyeshe walizozikusanya kwa miaka miwili zilifanya kazi gani maana walitwambia ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati lakini mpaka sasa shule nyingi zina upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa mpaka watoto wanasomea chini ya miti.