Serikali yafuta kodi ya Stoo

Billal Saadat

Senior Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
169
Reaction score
358
Kupitia muswada wa marekebisho ya sheria ya fedha na kodi.

Kodi na Tozo ambazo si rafiki katika mazingira ya kibiashara zimeondolewa na kufutwa kabisa.

Kodi ya Store ni miongoni mwa kodi zilizoleta mtafaruku hadi kusababisha mgomo kwa wafanyabiashara wa mkoa wa kikodi Kariakoo.

Tozo nyingine zilizopendekezwa kuondolewa ni pamoja na Tozo za miamala pamoja na ushuru wa vitenge kupunguzwa.

Tunampongeza Rais Samia na serikali yake ameonyesha usikivu zaidi katika kuijenga nchi. Mama yuko kazini.

Pia soma
  1. Mgomo mkubwa Soko la Kariakoo: Maduka yamefungwa, Mei 15, 2023
  2. UPDATE: Mgomo waendelea Kariakoo kwa Siku ya 3, Wafanyabiashara wataka Mkutano wa Wazi na Majaliwa
  3. Mgomo wa Kariakoo; Serikali Iwasikilize Wafanyabiashara
  4. Mwendelezo wa Mgomo, Kiongozi wa Wafanyabiashara Kariakoo adai kuna kikundi kina maslahi binafsi
  5. Waziri Mkuu Majaliwa aibukia Kariakoo, azungumza na wa fanyabiashara
  6. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afika Kariakoo. Aagiza task force za TRA kusitisha shughuli zake haraka

 
Hata hili la Bandari, litafutiliwa mbali.

Maandamano na spana ziendelee tafadhali.🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Yaani serikali iliyoweka tozo,tukapiga kelele Waziri wa fedha akatujibu tuamie Burundi, Leo hii anaifuta nasimama popote nilipo kumpigia makofi?

Yaani mtengeneze tatzo wenyewe alafu mlitatue alafu tuwasifie?
 
Yaani serikali iliyoweka tozo,tukapiga kelele Waziri wa fedha akatujibu tuamie Burundi, Leo hii anaifuta nasimama popote nilipo kumpigia makofi?

Yaani mtengeneze tatzo wenyewe alafu mlitatue alafu tuwasifie?
Alafu mbona taarifa za Tozo zimeachwa kutolewa au ndio kusema tushapigwa? 😢😢
 
Makato yarudi kama ilivyokuwa awamu ya 5

Bundle zirudi kama zamani, makampuni yasipangiwe yaachwe yashindane kupata wateja, kwa sasa hawashindani maana wamepangiwa bei
 
Mwingulu akikaa na kamishna wa TRA kwenye kitengo cha sera na kodi waje tena kodi nyingine ili elekezi ili kuongeza mapato ya V8
 
Hatuna waziri wa fedha. Ana fanya mambo kwa kubahatisha. Sasa tozo ime pelekwa kwenye mafuta ya magari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…