Serikali yafikiria kuitanua barabara ya Morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yafikiria kuitanua barabara ya Morogoro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Mar 29, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,367
  Likes Received: 22,227
  Trophy Points: 280
  SERIKALI ipo katika mazungumzo na wahisani ili kuweza kupanua barabara ya Morogoro kuanzia Dar es Salaam hadi Chalinze, kwa kiwango cha njia mbili zitakazosaidia kurahisisha usafiri na kuondokana na ajali zisizo za lazima.

  Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari Ruvu mkoani Pwani, kabla ya Rais Jakaya Kikwete kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa machinjio ya kisasa ya Ruvu iliyopo Ruvu Darajani.

  Alisema ajali nyingi zinazotokea katika eneo hilo hazitokani na wembamba wa barabara hiyo kama inavyofikiriwa, bali zinatokana na uzembe wa madereva ambapo wengi wao wameonekana wakiendesha kwa kukiuka kanuni za usalama barabarani ikiwemo kwenda mwendo kasi kupita kiasi, kulewa na madereva wengine hupitiwa na usingizi wakiwa waneendesha magari.

  Dk Kawambwa amezungumza hayo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea ajali mbaya katika eneo la Kibamba Darajani jijini Dar es Salaam, ambako watu 10 akiwamo mama mjamzito aliyepasuka tumbo, walifariki dunia papo hapo baada ya lori la mafuta kuiangukia daladala.

  “Wembamba wa eneo ilipotokea ajali ya juzi na kuua watu wote kwenye daladala ni changamoto kwa serikali kutanua barabara hiyo, lakini ajali zinazotokea katika eneo hilo hazitokani na wembbama wa barabara, kwani ajali zinazotokea katika eneo hilo zinatokana na uzembe wa madereva,’’ alisema Dk Kawambwa.

  Akizungumzia kuhusiana na mradi wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo, Dk Kawambwa alisema mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka huu na utaanzia kutanua eneo la Mwenge hadi Tegeta kwa ngazi ya njia mbili za kuingia na kutoka ili kusaidia kuondokana na msongamano wa magari katika barabara hiyo.

  “Tunajua tutapata changamoto kubwa kwa wananchi waliojenga kandokando ya barabara hizo tunazotaka kuzitanua, lakini tutajitahidi kwenda na wakati kwa kuendelea na ujenzi huo huku mazungumzo na wananchi hao katika maeneo mengine ambayo yatakuwa bado hatujayafikia yakiendelea ili kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa kwa kiwango cha njia mbili,’’ alisema Dk Kawambwa.

  Pia Dk Kawambwa alisema ili kuondokana na tatizo kubwa la msongamano wa magari ndani ya jiji la Dar es Salaam, kupitia mradi wa kutanua barabara 10 za jiji hilo la Dar es Salaam utafanyika kwa lengo la kurahisisha usafiri katikati ya jiji hilo.

  Alisema mradi huo utafanya kazi kwa kutumia barabara tofauti na zilizo zoeleka katika usafiri wa daladala kama barabara ya Morogoro na Mandela.

  “Tunatarajia kutumia njia nyingine na hazitamlazimisha dereva kutumia barabara moja ya Morogoro ili afike Posta ama Ubungo bali ataweza kupita ya kutokea Kigogo na kumuwezesha kufika ubungo ama Posta hiyo ikiwa ni malengo ya kuondokana na msongamano wa foleni katika barabara hizo.
  Aliongeza kuwa mradi huo pia utasaidia kuondoa mrundikano wa malori kuwa katika foleni moja na magari madogo hasa katika barabara ya Jangwani, ambapo imeonekana malori yakiitumia pamoja na magari mengine madogo ambapo mradi huo ukianza malori na magari mengine hayatakuwa katika barabara moja.

  SOURCE: GAZETI LA MWANANCHI
   
 2. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Let 's wait and see
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Thats the best thing we can do! at least for now!
   
Loading...