Losambo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 2,612
- 864
WABUNGE wameitaka Serikali kutoa maelezo ya vurugu za Machinga zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Mbeya na hatua ya askari wa JKT kambi ya Masange, kuvamia Soko Kuu la Tabora, kuwapiga na kuwajeruhi wafanyabiashara. Ombi hilo lilitolewa jana asubuhi na Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), Godfrey Zambi, muda mfupi baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Kwa habari yote Serikali yabanwa vurugu za Mbeya
My take;
Ngoja tusubiri majibu ya serikali hii leo tuone nini itasema, je itagusa kiini cha tatizo au itaendeleza propaganda tena?
Nilishabandika post fulani kuhusiana na tatizo hili kwa ufupi, kiini cha tatizo la Wamachinga Mbeya na kwingineko ni ukosefu wa ajira. Hivyo nitafurahi kama serikali itajikita katika kutoa njia mbadala ilizojipanga za kuwaandalia mazingira mbadala yanayokidhi haja badala ya kukimbilia kuwafukuza kama mbwa tena kwa kutumia maguvu yaliyopitiliza