GAZA: Israel yatoa masaa 24 kwa raia wote waliishio kaskazini mwa Gaza kuhamia upande wa Kusini

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,769
Wizara ya ulinzi ya Israel imetoa masaa 24 kwa raia wote waishio upande wa Gaza Kaskazini kuondoka mara moja. Raia hao wameamriwa kuelekea upande wa kusini mwa Gaza haraka iwezekanavyo. Taarifa hiyo inasema, atakayebaki baada ya masaa 24 atakuwa amechelewa.

Kaskazini mwa jiji la ukanda wa Gaza kuna wakazi takribani Milioni 1. Msemaji wa Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR amesema ni kitu kisichowezekana kwa watu milioni 1 kuhamishwa ndani ya masaa 24. Pia amesema kuhamisha watu kiasi hicho kunahitaji maandalizi ya zaidi ya siku 180 za kuanda mahali wanapofikia, chakula, madawa na mahitaji mengine.

Wachambuzi wa masuala ya kiusalama wanadai kuwamba huenda hayo ni maandalizi ya jeshi la ardhini la Israel kuingia ukanda wa GAZA ili kuwasaka wanamgambo wa HAMAS. Ili kufanikisha hilo lazima raia waondolewe lasivyo mauaji ya raia yatakuwa mengi kuliko kawaida.

Msemaji wa HAMAS aliyeko uhamishoni nchini Jordan amewataka raia wa GAZA kupuuza wito huo akiuita ni windo wa Propaganda wa Israel wa kutaka kuinyakua Ardhi hiyo endapo Watahama.

Wakati hayo yakijiri, Israel imerundika zaidi ya wanajeshi elfu 30 na vifaru 600 kwenye mpaka wa GAZA kwa kile kinachosemekana ni maandalizi ya Uvamizi wa Ardhini kuelekea upande wa Gaza.

Bora wamewapa gracing period raia waondoke kuepusha mazara zaidi maana Israel when they talk they mean ,sasa huyo kiongozi anasema raia wapuuzie wito huo wakati yeye amekimbia hayo ni maisha yao hatima yao wanayo wenyewe, zakuambia changanya na zako.
 
Maisha haya!! Cha ajabu wanaweza kumsikiliza jamaa aliyoko Jordan anakula maisha tu, hapa ni kuchanganya na zako.
 
Bora wamewapa gracing period raia waondoke kuepusha mazara zaidi maana Israel when they talk they mean ,sasa huyo kiongozi anasema raia wapuuzie wito huo wakati yeye amekimbia hayo ni maisha yao hatima yao wanayo wenyewe, zakuambia changanya na zako.
Tena uko alipokimbilia anashinda na baibui na ushungi wa kike. Aende akapuuze pamoja na raia
 
Back
Top Bottom