Serikali ya Zimbabwe yateuwa wakuu wa tume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Zimbabwe yateuwa wakuu wa tume

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Feb 12, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,913
  Trophy Points: 280
  [​IMG] ZimbabweWazimbabwe wawili wanaoheshimika nchini humo wameteuliwa kuongoza tume mbili mpya - za haki za binadamu na tume ya uchaguzi. Uteuzi huo umefanyika baada ya miezi kadha ya mashauriano magumu na kufanikiwa kwake ni dalili ya maendeleo katika siasa za mvutano nchini humo.
  Sehemu muhimu ya mkataba wa Septemba 2008 uliounda serikali ya umoja wa taifa Zimbabwe mwaka mmoja uliopita ni kuteuliwa kwa kiongozi mpya wa tume ya uchaguzi na kuunda kwa tume ya haki za binadamu. Serikali sasa imeamua nani wataongoza tume hizo mbili.
  Mwenyekiti mpya wa tume ya uchaguzi ni Jaji Simpson Mtambanengwe, raia wa Zimbabwe aliyekuwa akifanya kazi na mahakama za Nambia tangu 1994 ambako aliwahi kuwa Jaji Mkuu na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Windhoek. anachukua nafasi ya George Chiweshe aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi uliopita.
  Professa Reg Austin atakuwa mwenyekiti wa kwanza wa Tume ya Haki za Binadamu, Zimbabwe. Alikuwa mshauri wa maswala ya sheria wa kiongozi wa zamani Joshua Nkomo wakati wa mazungumzo ya uhuru London mwaka 1979.


  http://www.voanews.com/swahili/2010-02-08-voa4.cfm?CFID=376164956&CFTOKEN=55014355&jsessionid=0030b05b82d1963de82cb263721c7345297f
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...