Serikali ya Zanzibar kuvunja shule ya kihistoria, kujenga soko

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,569
9,429
Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema inakusudia kulivunja jengo la Shule ya Sekondari ya Vikokoni lililopo Darajani Mjini Zanzibar na badala yake eneo hilo linatarajiwa kujengwa soko kubwa la kisasa litakalotumika kwa ajili ya biashara mbalimbali.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema hayo leo Ijumaa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi, wakati akiwasilisha taarifa maalumu ya Serikali juu ya uvunjaji wa shule hiyo yenye zaidi ya miaka 50 tangu kujengwa kwake.

Amesema kuwa Serikali wameamua kuivunja shule hiyo ili kupatikana kwa fursa nzuri ya kulipanua eneo hilo kibiashara kwa kujenga jengo kubwa la soko ambalo litabadilisha mwonekano wa mji wa Zanzibar.

Amesema kuwa taratibu kwa ajili ya ujenzi huo tayari zimeanza kufanyika ikiwemo kuandaa mchoro maalumu na kuupeleka kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) kwa ajili ya kupata baraka zao juu ya ujenzi kwenye eneo hilo ambalo lipo chini ya miji ya urithi duniani.

Alisema ni matarajio yao kuwa ujenzi huo utaanza baada ya kupokea ushauri wa kitaalamu kutoka Unesco jinsi gani ujenzi huo ufanyike ili kutoondosha haiba ya mji huo ambao ni tegemeo kubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla kibiashara.


Chanzo; mwananchi
 
Imani ile na makumbusho ni kama paka na panya! Huwa nawaona CNN na aljazeera wakifanya vurugu zao kosa wafike museum hahaha! Vitabu vya kale na masanamu yote wanapurua, na miongoni mwao wapo wanaopiga selfie wakivunja huku wengine wakificha kwenye mikoba yao na kujipatia pesa si haba.
 
Sawa kabisa. Unavunja shule ili ujenge soko kisha uuze vitu vya watu waliovunja soko kwao wakajenga shule!
 
Back
Top Bottom