Serikali ya Zanzibar haijazuia mchakato wa Katiba

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijazuia mchakato wa upigaji kura wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano na iko tayari kutekeleza zoezi hilo litakapokuwa tayari.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari vya Zanzibar Waziri wa katiba,sheria,utumishi wa umma na utawala bora Mhe Haroun Ali Suleiman amesema wao SMZ hawahusiki na mchakato huo kwa vile mamauzi yote yako ndani ya uwezo wa serikali ya muungano ndio wenye mamlaka ya kupanga na kupangua.

Mhe Haroun pia amezungmzia utendaji wa Wizara yake katika maeneo mbalimbali na kueleza hatua zinazochukuliwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la Mahakama kuu ya Zanzibar huko Tunguu ingawa amekiri kuwepo udhaifu katika baadhi ya watendaji ikwiemo ofisi za nyaraka za serikali na hatua zimeanza kuchukuliwa.


Waziri Haroun anakuwa Waziri wa pili wa SMZ kukutana na vyombo vya habari vya Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa Rais Ali Shein kuzitaka wizara zote zikutane na vyombo vya habari na kusikiliza kero za wananchi.

Chanzo ITV
 
Back
Top Bottom