Serikali ya Tanzania yakubali ndoa ya jinsia moja

GIB

JF-Expert Member
Mar 2, 2012
336
92
Kuna mjadala uliokuwa hapa jf ukihusisha Tanzania kunyimwa misaada kutoka kwa cammeron (PM ), pia leo huo mjadala unaendelea.

Lakini Nipashe ya leo tar 22/3 yaonesha Tanzania imepewa msaada wa mabilioni ya pesa je kulikoni?
soma hii habari kisha ,utafakari

Uingereza yaipa Tanzania Sh. bil. 69.5 kusaidia huduma ya maji vijijini




Na Mwandishi wetu

22nd March 2012

Tanzania imepokea Sh. bilioni 69.5 kutoka Serikali ya Uingereza kwa ajili ya kusaidia kuimarisa huduma ya maji vijijini pamoja na utunzaji wa mazingira bora katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Msaada huo utawanufaisha zaidi wa wakazi 650,000 watakaopata huduma ya maji safi, na zaidi ya wakazi 160,000 katika kuimarisha huduma ya vyoo hasa kwa wakazi wanaoishi vijijini.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa asasi ya DFID Tanzania, Marshall Elliot, alisema upatikanaji wa huduma ya maji ni muhimu katika maisha ya mwanadamu hasa katika afya, elimu na kipato.


CHANZO: NIPASHE
 
Hivi mnadhani hawa wanatoa pesa zote hizi kwa lengo gani? wanatupenda sana, wana moyo safi sana? Hapana! huwa tunapay in kind,ndo matokeo ya mikataba ya uchimbaji madini and the like inayosainiwa mahotelini
 
Nikafikiri Nipashe ndo wameandika hivyo, kumbe heading yako wala haimo kwenye habari ya Nipashe! Ni hisia zako tu, manake juzi Waziri Chikawe alitutangazia kupitia vyombo vya habari kuwa Tz pamoja na mambo mengine imekataa ndoa hizo. Au ndo unazipigia promo kiaina ili ziruhusiwe? Weka wazi basi, usisingizie Nipashe.
 
Heading kero kama zile za gzeti la Alasiri na Dar Leo na unapoingia kurasa za ndani ya gazeti unakuta habari inayotajwa haimo. Bure kabisa!!
 
Unajua watanzania wananishangaza sana..hivi unategemea kuwa kwa hii serikali ya kuombaomba tunaweza kwepa hayo? Mimi nachojua ni kuwa muda si mrefu tutatepeta tu,na kwa aina ya hawa watawala wetu.Sijui!!
 
Unajua watanzania wananishangaza sana..hivi unategemea kuwa kwa hii serikali ya kuombaomba tunaweza kwepa hayo? Mimi nachojua ni kuwa muda si mrefu tutatepeta tu,na kwa aina ya hawa watawala wetu.Sijui!!


Mwigulu alisema CHADEMA hawana pesa maana Uingereza wamegoma kuwasaidia baada ya kukataa sera ya Cameroon. Sasa serikali ya CCM imepataje huu msaada? wamekubaliana Cameroon au?
 
Mwigulu alisema CHADEMA hawana pesa maana Uingereza wamegoma kuwasaidia baada ya kukataa sera ya Cameroon. Sasa serikali ya CCM imepataje huu msaada? wamekubaliana Cameroon au?

kuna mtu alisema hili uwaelewe CCM inabidi uwe na akili ya mwendawazimu sasa naanza kuamini.
 
Back
Top Bottom