Serikali ya Tanzania yaingia kwenye mazungumzo na Serikali ya Ujerumani ili kuona itakavyonufaika na Mjusi mkubwa 'Dinosaurs'

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
Serikali ya Tanzania imesema ipo kwenye hatua za awali za mazungumzo na Serikali ya Ujerumani kuona jinsi itakavyofaidika na mapato yatokanayo na utalii kupitia mabaki ya Mjusi mkubwa ‘’Dinosaurs " ambaye ni kivutio cha kikubwa cha utalii katika jumba la Makumbusho nchini Ujerumani.

Mjusi huyo kwa jina la kitaalamu anaitwa Dinosaur ambapo mabaki yake yalivumbuliwa miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi, yalikusanywa na kupelekwa nchini Ujerumani ambako wataalamu waliyaunda na kisha kuyaweka kwenye Makumbusho hiyo.

Amesema lengo la mazungumzo hayo ni kutaka kujua kiasi gani cha mapato yanayokusanywa na namna gani wanavyoweza kugawana mapato hayo yatokanayo na watalii kupitia mjusi huyo baina ya Serikali hizo mbili.

Pia soma
>Mjusi wa Tanzania nchini Ujerumani - Balozi wa utalii
>Germany Will Return 'Dinosaur' Remains To Tanzania
>Mnyama Mkubwa Zaidi Aliyewahi Kuishi Duniani aligundulika Tanzania mkoa wa Lindi
>Serikali: Hakuna tija kuwarudisha 'mijusi mikubwa' toka Ujerumani
>Serikali ingepata Sh3.2 Billion kama ingeliweza kurudisha mjusi wake!
 
Ni jambo jema. Kwakuwa mevumbuliwa nchini mwetu, Tanzania inapaswa kufaidika na utalii utokanao na mabaki ya mjusi huyo mkubwa.
 
Serikali ya Tanzania kupitia Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,.Japhet Hasunga imesema ipo kwenye hatua za awali za mazungumzo na Serikali ya Ujerumani kuona jinsi itakavyofaidika na mapato yatokanayo na utalii kupitia mabaki ya Mjusi mkubwa ‘’Dinosaurs " ambaye ni kivutio cha kikubwa cha utalii katika jumba la Makumbusho nchini Ujerumani Mjusi huyo kwa jina la kitaalamu anaitwa Dinosaur ambapo mabaki yake yalivumbuliwa miaka 100 iliyopita katika eneo la Tendaguru mkoani Lindi, yalikusanywa na kupelekwa nchini Ujerumani
ambako wataalamu waliyaunda na kisha kuyaweka kwenye Makumbusho hiyo.

Amesema lengo la mazungumzo hayo ni kutaka kujua kiasi gani cha mapato yanayokusanywa na namna gani wanavyoweza kugawana mapato hayo yatokanayo na watalii kupitia mjusi huyo baina ya Serikali hizo mbili

0 replies 0 retweets 2 likes
Yalio bakia hapa ni zaidi yahayo ya mewashida kujio gezea Utali .....ndomunaanza kutafuta kiki ujarumani duh cinema hizi zinachosha
 
kwa mfano wakatugawio sehemu ya mapato ya mjusi halafu waka discourage wajerumani kuja kutalii nchini mwetu tutapata hasara kubwa zaidi.
 
1540978336468.png
 
Ni kuwaomba arudi nyumbani tu maana nchi nyingi huwa zinarudishiwa vitu vyao.
Kuna mifano mingi kama Scotland, Egypt, India na hata nchi nyingi ambazo wazungu walichukuwa (wizi)

Wataalamu wetu hivi hawajawahi kufukua hata kobe?
Maana kila kitu mvumbuzi ni mzungu tu
Tujitahidi na sisi tufanye utafiti maana lazima mama yake na huyo dinosaur atakuwa kalala sehemu
 
Kwa hiyo zile harakati za kutaka kumrudisha Tanzania zimeshindikana now yamekuwa mazungumzo ya kujua tutafaidika vipi akiwa hukohuko Makumbusho ya Ujerumani. Labda Museum ya TZ haina uwezo wa kuhifadhi na kutunza
 
Hivi kweli huyu ni mjusi? au wajerumani wametulisha pumba ili tuone ni kitu kidogo tu
coz mjusi ni mdudu Na huyu ni jinyama kuubwa hawa wanatuenjoy Sana bhwana wamrudishe tu
 
Back
Top Bottom