Serikali ya Tanzania isitangaze case za Corona virus hata kama zikipatikana

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,434
5,094
Kwenu wenye mamlaka
Baada ya kufatilia kwa kina suala la Corona , binafsi nashauri serikali isiingie mkenge wa wengine kutangaza case za Corona Tanzania hata kama zikipatikana.

SABABU
kwanza maambukizi ya Corona maeneo ya tropical Afrika ni kwa wale waliotoka nje tu, hakuna alietoka nje akamuambukiza local person, hivyo ni wazi kua virusi hizi vinakosa nguvu pindi mazingira ya joto , na ndio maana hata Raisi wa marekani anamatumaini kua joto litakalo anza mwezi wa nne litapunguza kama si kupoteza kabisa kwa ugonjwa wa Corona.

Ndio maana nchi kama Nigeria Cameroon na nchi nyingine za kiafrika, waliogundulika na ugonjwa ni wale waliosafiri, lakini hata baada ya kugundulika kwao. Hakuna kesi ya watu wandani kuambukizwa

Pili hali ya kiuchumi ya watanzania, wengi wetu chakula tunachokula leo tunakitafuta leo.
Ukitangaza kesi ya Corona , watu watapani na hawana hela ya kuingia sokoni kujaza stock nyumban. Wengi watakufa zaidi kwa njaa, uizi utaongezeka na wagonjwa watakosa huduma, badala yake itakua vifo vinavyosababiswa na makatazo na mazuio zaidi kuliko Corona,
Imani yangu ni kua Corona ni ugonjwa wa mlipuko kama ilivyo magonjwa ya macho mekundu kipindi funi na kisha hupotea,

Cha msingi mgonjwa yoyote atakae kutwa na Corona atibiwe kwa tahadhari lakni awe kama anatibiwa magonjwa mengine.

Najua kuna madaktari wasiotunza siri watatangaza mitandao ya kijamii, hao achananeni nao.

Watu wawe na aman na kazi ziendelee, wanaoumwa watibiwe kama normal cases

Narudia tena serikali isitangaze case za ugonjwa wa Corona kwa kufata mkumbo wa kimataifa kisha kuzuia shughuri za kijamii na kiuchumi.

Mambo yaendelee, ni mwezi huu tu na wanne mwanzoni. Corona itakua historia
 
Uyu amesha fowadiwa ile post ya wasapu kutoka kwa mwanafunzi wa china akaitumia kutengeneza uzi huu

Akuelewa ule msemo za kuambiwa changanya na zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini Unasema ni Mwezi huu tuu na wa NNE? Kuwa ugonjwa utakuwa historia?
Au unataka Kumaanusha Joto?
Unajuaje kama hiyo ndo Miezi ya Joto?
Hiyo ni Miezi ya Masika Mvua ,je Unamaanusha Nchi Nzima au Dar tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom