Serikali ya sherehe na maonesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya sherehe na maonesho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Congo, Nov 10, 2011.

 1. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Moja kati ya vitu ambavyo serikali yetu imefanikiwa miaka ya hivi karibuni ni kufanya sherehe na maonesho. Kila kukicha viwanja vya Mnazi Mmoja na kwingine kuna shughuli ya maonesho au sherehe inaendelea. Kasma ya sherehe na maonyesho hayo nadhani ni kubwa. Kama ni mashule ingeweza kujenga mengi tu. Nimetonywa kuwa wale maofisa wa serikali wanaokuwa kwenye maonesho hayo wanalipwa shs 100,000/= kwa siku. Mwasemaje?
   
 2. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Utasema nini wakati kila mtu anataka kula siku hizi na serikali yetu ya kifisadi inataka kila mtu abebe chake mapema?
  Hapo ni mwanzo tu maana tunafanya sherehe wakati pesa za kulipa mishahara tunakopa benki,ndio utajua kuwa tuna serikali mbovu na haifai.
   
 3. Platnam

  Platnam JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 208
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Hivi ni serkali ipi mnaizungumzia? mi ninachojua hakuna serkal ila ni kundi la wahuni wanaoitafuna hii nchi..
  Uliona wapi nchi yenye serkali halafu haiwezi kufanya chochote?

  Umeme shida,
  Sukari shida,
  Maji shida,
  Elimu ya kubabaisha,
  Kila siku bidhaa zina bei mpya,
  Matajri wababe kuliko hyo inayoitwa serkal,
  tukiwa mashoga ndo tupate misaada nk..

  tired of this shit.
   
 4. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  KAMA HATA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI ZAKE ZA WILAYA IMECHELEWA KULIPA YAWEZEKANA HAYA MAONESHO IKAWA NI NJIA YA KUJIKIMU KIUCHUMI WAFANYAKAZI WA TAASISI NA IDARA ZA SERIKALI HUSIKA......

  Taabu serikali yetu ikitoka AGIZO.....tafsiri yake nadhani ni CHANGANYA NA YAKO (kwako mkuu wa idara)....Pesa inayoendelea kutumika katika MAADHIMISHO HAYA (naona kila Wizara na Idara ina wiki yake) ingetosha kurekebisha mengi yanayotusibu kiuchumi na kijamii...

  Bahati mbaya VIONGOZI wetu PRIORITIES zao ni tofauti na zile za ukweli za WANANCHI na NCHI YENYEWE......
   
 5. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapa ni kuwa kila mtu anaitafuna kodi ya waTZ kwa urefu wa kamba yake
   
 6. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hatuna usemi.Tutapata presha za bure
   
Loading...