Serikali ya mkoa wa Kibaha angalieni uwezekano wa Traffic lights kwenye barabara za kuingia Kibaha stand

fitonenendefu

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
428
866
Leo mida hii ya usiku natoka zangu mjini Dar es Salaam kwenda Kibaha kupumzisha mbavu zangu. Sasa ni lazima magari ya abiria na daladala yaingie kukata ushuru stand ya mkoa Kibaha.

Hii stand mpya (zao la Hayati Magufuli), ila sasa hizi barabara za kuingia na kutoka hapo stand ya Kibaha huu upande kama unatoka mjini na ule upande kama unaelekea picha ya ndege zimekaa kimtego sana wa ajali.

Kwa kweli serikali iliangalie hilo. Kwa maana mida hasa ya usiku huwa kuna gari kubwa zinamiminika kwa kasi sana kutokea upande wa picha ya ndege. Sasa hapo ni hatari sana maana kwa usiku traffic police hakuna na traffic lights hakuna.

Dereva wa daladala wanafanya kama kuvizia tu. Zingatieni hilo kuokoa yajayo yasiyofurahisha. Taarifa hizi zimfikie mama tunajua anaupiga mwingi sana na hili wakalitazame.
Kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom