Serikali ya Misri yamkamata mwanahabari wa Al-Jazeera

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
Aljazeera.png


Serikali ya Misri imedhibitisha kwamba inamzuilia mwanahabari kutoka shirika la habari la AlJazeera aliyekamatwa Ijumaa.

Wizara ya usalama wa ndani inasema mwanahabari huyo, Mahmoud Hussein, atazuiliwa kwa kipindi cha siku 15 kwa tuhuma za kuchochea maasi na kusambaza habari za uongo.

Al Jazeera imepigwa marufuku ya kuendesha shughuli zake nchini Misri, na imelaani hatua hiyo.

Kulingana na Aljazeera, mwanahabari huyo raia wa Misri alikuwa nchini humo likizoni.

Aljazeera inahofia usalama wa mwanahabari huyo.

Chanzo: BBC
 
Ukiona nchi inapiga vita waandishi basi kuna tatizo kwenye Serikali

Sio kweli mkuu, Al Jazeera ni chombo kinacho tumiwa na MSM holders kueneza matakwa yao hawana tofauti yoyote na CNN,mfano mdogo taarifa za vita nchini Syria.
 
Kama ni kweli alisambaza habari za uongo nawaunga mkono Misri.

Nachowapendea Aljazeera habari zao hazipo biased.

kwakua sijajua aliripoti nini, ntasimama upande wa mwandishi.
Serikali nchi yoyote hazitaki kusemewa maovu yao, mfano si Tanzania, usiende mbali
 
Back
Top Bottom