GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,006
Ninacho shangazwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hawa Mawaziri wake, kila mmoja kuja na matamshi yake huku serikali ikikana huku waziri wa utalii kupiga marufuku ndege yoyote kuja .
Waziri wa afya Hamad Rashid nae amekuwa akitoa matamko yake pamoja na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,kukana kuzuiya usafiri wa ndani na nje.
Wakati huo huo, wanasema wanaokuja lazima wakae karantini siku 14 kwa gharama zao? Mgeni gani atakae kuja akae karantini kwa siku hizo kwa gharama yake ? Pia hata sisi wazenji tutarudi vipi nyumbani kwa vitisho kwa gharama za karantini?
Kama mnazuia usafiri zuiyeni tu moja kwa moja Lkn sio kutoa vitisho vya karantini, huko ni kwenda kuambukizana, huku tuliko nchi za kigeni tupo karantini majumbani, si ruhusa kwenda hata hospital, unless una tatizo la kupumua.
Sisi kama wazenji watanzania tuna haki ya kurudi nyumbani, kama nchi nyengine zinavyo chukua hatua kuchukua raia wake.
Sent using Jamii Forums mobile app