Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kipindi kifupi tangu iingie madarakani, imefanya maamuzi ambayo yameshangiliwa na watu wengi. Baada ya muda mfupi serikali imekiri kwa vitendo kuwa maamuzi hayo yalikuwa na makosa. Baadhi ya makosa yaliyo dhahiri mpaka sasa ni pamoja na:
Kuna fikra zimejengeka kuwa kila kitu kilichofanya na Awamu ya 4, ilikuwa ni makosa matupu. Mimi nilitegemea kila kiongozi makini, hasa kiongozi mkuu hufanya tathmini ya kina kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule. Nchi ilikwishakuwepo na uongozi umekuwepo tangu enzi za utawala wa Mjerumani. Nchi haianzi leo. Hivyo ni muhimu kiongozi unapoliona jambo ambalo unadhani halipo sawa kujiuliza maswali kadhaa kabla ya kuchukua maamuzi. Maana kauli ya kiongozi mkuu ikiwa siyo sahihi, athari zake ni kubwa. Ninatarajia kabla ya kubadilisha kilichopo, Rais na wasaidizi wake inabidi wajiulize - kwa nini watangulizi wake waliruhusu au kuzuia jambo hilo kutendeka? Je, hawakuwa na utashi? Wahusika hawakutimiza wajibu wao? Hao waliamua hivyo walikosa uzalendo? Au uwezo wao ulikuwa mdogo? Mazingira ya wakati huo yalikuwa tofauti na ya sasa?, n.k.
Serikali ilitangaza kufuta uagizaji wa sukari toka nje kwa maelezo kuwa tunayo sukari ya kutosha inayozalishwa ndani. Na sisi wote tulishangilia kwa uamuzi wa kizalendo, tukiamini serikali iliyopita iliruhusu uagiza wa sukari toka nje kwa msukumo wa rushwa maana ilikuwa ni serikali ya rushwa. Sasa inadhihirika kuwa, uamuzi wa kuzuia uagizaji sukari toka nje ulikosa ni kosa, huenda kilichotakiwa ilikuwa ni kupitia utaratibu wa uagizaji sukari toka nje na kuufanyia maboresho ili sukari ya nje isifurike soko kiasi cha kuwafanya wazalishaji wa ndani kukosa soko.
Misaada
Moja ya mambo ambayo watu walishangilia sana ni kauli ya Rais kuwa nchi hii ni tajiri sana, hatustahili kulilia misaada bali tunastahili kuwa donor country. Wengine tulisema wazi kuwa nchi yoyote ina uwezo wa kujitegemea kama ina mipango thabiti lakini hilo haliwezi kutokea ghafla maana kujitegemea ni process.
Waimba vibwagizo vya kila wimbo wa serikali, akina Polepole na wenzake wakaja juu kweli kweli kwa kusema uwezo huo tunao kuanzia sasa maana makusanyo ya kodi yameongezeka sana. Wakaongeza kuwa misaada tumepewa miaka yote na ndiyo iliyotufanya tushindwe kujitegemea.
Tulimlaumu sana Rais Kikwete kwa kukaa angani wakati wote, akizunguka kutafuta misaada na mikopo. Na tulimlaumu sana pia kwa kutuaminisha kuwa huko nje kuna pesa nyingi, sisi kazi yetu ni kujieleza vizuri ili tuweze kusaidiwa.
Safari hii tukaambiwa bajeti yetu ya 2016/2017 itakuwa ni bajeti ya kujitegemea. Jambo la ajabu ni kuwa juzi Rais Magufuli akiongea na viongozi wa CCM toka mikoani aliwaambia, ' wana-CCM tembeeni vifua mbele kwa sababu serikali itatimiza ahadi zake, maana hata wahisani wamesema watatupatia misaada. European Union wamesema watatusaidia, Wamarekani watatusaidia, Wajapani watatusaidia, Wachina na Waingereza, wote wameahidi kutusaidia. Makusanyo ya kodi yameongezeka'. Kwa kauli hii ya Rais maana yake ni kuwa CCM itaweza kutekeleza ahadi zake kwa sababu wahisani wameahidi kutusaidia na makusanyo ya kodi yameongezeka.
Kwa hiyo wale waliosema kuwa tayari tunaweza kujitegemea, shangilieni pia kwa kauli hii mpya kuwa utekelezaji wa ahadi za serikali hii utategemea mambo mawili, moja ufadhili wa mataifa wahisani, na pili makusanyo yetu ya ndani. Lakini ikumbukwe kwamba hao wahisani walioahidi kuisaidia Tanzania, wapo kutokana na kazi kubwa ya kujenga mahusiano mazuri kati ya nchi yetu na mataifa wahisani yaliyofanywa na serikali ya Kikwete. Kauli ya kusema sasa hivi hatuna haja na ufadhili ilikuwa ni kauli iliyokosa umakini, kilichotakiwa ilikuwa ni kuboresha mahusiano ya Taifa letu na jamii ya kimataifa ili misaada yao ilete tija kwa Tanzania katika safari ya kuelekea kujitegemea.
Mwalimu aliwahi kusema, kila awamu kuna mazuri hufanya na kuna makosa hufanyika, awamu inayofuata huyachukua mazuri, huacha mabaya, na hata yale mazuri huyaboresha. Kama kila utawala ukiingia na kuamini uliotangulia haukufanya kitu, hatutaweza kusonga mbele maana kila mara tutakuwa tunaanza upya.
Ushauri kwa Rais Magufuli, kabla ya kufanya mabadiliko au kufuta kitu chochote ambacho kilikuwepo afanye uchunguzi makini sana ili kuweza kujua kitu hicho kinatakiwa kufutwa, kuboreshwa au kuendelezwa. Ni aibu kubwa kwa serikali kufanya maamuzi leo halafu baada ya mwezi mmoja inagundulika uamuzi ulikuwa na makosa.
Uamuzi wa kuzuia Bunge kuoneshwa ni wa hovyo kabisa. Awamu ya nne, ya Jakaya Kikwete ndiyo iliyoleta utaratibu wa taarifa ya CAG kujadiliwa Bungeni. Hongera sana Jakaya Kikwete kwa hilo. Tafadhali Magufuli usifute utaratibu wa taarifa ya CAG kujadiliwa Bungeni maana hii serikali yako kwenye demokrasia, tulio wengi tuna mashaka kuwa unaturudisha nyuma. Yaache mazuri ya mtangulizi wako, ongeza ya kwako mazuri mapya.
Rais kwenye hili jengo letu, rekebisha matofali yaliyokaa vibaya, ondoa yasiyofaa, ongeza matofali mazuri kwenye ukuta ili jengo likamilike, kuna sehemu tumeona unabomoa hata matofali yaliyojengwa vizuri na mafundi waliotangulia. Ukiendelea kufanya hivyo nyumba haitakamilika.
- Kuzuia uagizaji sukari toka nje
- Kutangaza kuwa tupo tayari kuanza kujitegemea, hatuhitaji misaada, tunatakiwa kuwa donors