Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,154
- 137,162
Let’s talk about it!
Serikali ya Magufuli ni nini? Ni nani?
Kuna kila aina ya ‘excuses’ ambazo Rais Samia anapewa na baadhi ya watu.
Watu hawa wanadai kuwa Rais wetu huyu anahujumiwa na watu waliokuwepo kwenye serikali ya Magufuli.
Sasa labda ni mimi tu ambaye ndo sielewi. Hivyo nataka/ naomba nieleweshwe.
Hiyo serikali ya Magufuli ni nini? Ni mashine? Ni watu? Ni mbuzi? Ni nguchiro?
Nijuavyo mimi hiyo serikali ya Magufuli ilimhusisha Magufuli mwenyewe pamoja na Samia.
Samia naye ni sehemu muhimu kabisa ya hiyo serikali ya Magufuli.
Rais Samia kuivunja serikali ya Magufuli ni kujivunja na yeye mwenyewe maana hatenganishiki na Magufuli.
Hatenganishiki kwa sababu waligombea wote mwaka 2015 na kugombea tena mwaka 2020.
Samia angeweza kabisa kuamua kutogombea tena baada ya kumaliza muhula wake wa kwanza kama makamu wa Magufuli.
Lakini aliamua kugombea tena na huyo huyo Magufuli mwaka 2020.
Sasa mtu huyo anajitengaje na serikali ya Magufuli?
Help me make sense of this ‘vunja serikali ya Magufuli’ nonsense’.