Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,115
- 2,771
Kupitia NEMC walitoa tamko kwamba hakuna tena hoteli yoyote kutoza hela kuingia kwenye fukwe yoyote hapa Tanzania . Basi siku ya leo nikaanza na South Beach kule Kigamboni, pale wasomali wenyewe wanahakikisha umelipa kabla ya kuingia.
Mbalamwezi pale leo hii mida ya saa 9.45 nikapigwa 5,000 nilikaa dakika 39 nikaondoka. Kufika Giraffe pia nikalipishwa 5,000, hapa nilikunywa chai na kuondoka kuelekea Ramada Hotel ambaayo ni jamani, ambako pia nililipia 40,000 kwenda kula huko nyuma. Pale mbalamwezi nikauliza kwanini nilipe wakati serikali ilishakataza, baunsa akanijibu, kwamba nikiendelea na maswali hawataniruhusu kuingia na pia hawajui chochote kuhusu hilo tangazo.
South Beach nako niliambiwa kwamba hilo tangazo haliwahusu nikaulize serikalini kwamba lilimlenga nani, ila siyo wao
Nimefanya hivi makusudi kutaka kujua seriousness na ukweli wa hii serikali Ya kisanii ambayo inapenda maigizo hasa ikiona vyombo vya habari . Serikali Ya Magufuli ni usanii kuzidi wa kikwete, matamko kila siku, matamko yenyewe ili waonekane kwenye camera . Tusubiri mwaka uishe. Tamko la NEMC ni Changa la macho