Serikali ya Kikwete Yajivunia Elimu

Jafar

JF-Expert Member
Nov 3, 2006
1,136
52
Na Salva Rweyemamu

SERIKALI imesema imepata mafanikio makubwa katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwagharimia wanafunzi 34,012 wanaotoka katika familia zenye kipato duni kwa ajili ya kupata elimu ya sekondari katika shule mbalimbali.

Katika mfanikio hayo serikali imesema ilipunguza ada kwa wanafunzi wa kutwa kutoka Sh 40,000 hadi Sh 20,000 na kuchukua jukumu la kutoa ruzuku ya fidia ya ada kwa wanafunzi 417, 712 mwaka 2006 na wanafunzi 755,079 mwaka 2007,Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu akitaja mafanikio ya elimu ya sekondari alisema kumekuwepo na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi kutoka 355,188 hadi wanafunzi 829,094 mwaka 2007.

Alisema ili kuchangia nguvu katika mkakati wa kuongeza nafasi kwenye shule za sekondari serikali ilitoa Sh bilioni 6.4 kati ya mwaka 2005 na 2007, madarasa 4065, nyumba za walimu 3,404, maabara 124, majengo ya utawala 19 vilijengwa kwa kutumia ruzuku hiyo.Aidha alisema kuwa serikali imeendelea kuongeza ubora wa elimu kwa kutoa fedha za ruzuku ya uendeshaji kwa lengo la kufikia Sh 30,000 kwa shule za serikali na Sh 15,000 kwa shule binafsi zilizofuzu vigezo.

Mkurugenzi huyo alisema serikali imetoa Sh bilioni 16.9 za kununulia vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule za sekondari za serkali katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2007.Aidha alisema kwamba serikali inaendelea kuimarisha ukaguzi wa shule kwa lengo la kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa inakidhi mahitaji na kuendelea kutoa mafunzo ya walimu wakiwa kazini ili kuongeza uwezo wa walimu hasa katika masomo ya sayansi hisabati na Lugha.

-------------------------------------------------------------------
Baada ya miaka 2 karibu na nusu hayo ndio mafanikio ya JK. Mimi hainiingii akilini wakati mtihani wa darasa la nne na kidato cha pili nasikia imefutwa, muungwana anataka Quantity na si Quality. Hivi ubora wa elimu unapimwa kwa kiasi gani cha fedha kimetolewa au kwa kupima elimu inayotolewa ?
 
Na Salva Rweyemamu

-------------------------------------------------------------------
Baada ya miaka 2 karibu na nusu hayo ndio mafanikio ya JK. Mimi hainiingii akilini wakati mtihani wa darasa la nne na kidato cha pili nasikia imefutwa, muungwana anataka Quantity na si Quality. Hivi ubora wa elimu unapimwa kwa kiasi gani cha fedha kimetolewa au kwa kupima elimu inayotolewa ?[/QUOTE]

Hawa jamaa hawajafanya lolote na hiyo plagiarisation wanayoitaka kuifanya ingeendana na uhalisia tungekubali. Enzi za Nyerere mtu alikuwa anapewa elimu ya ukweli sasa hivi ni kufaulu mtihani na namna utakavyofaulu utajua mwenyewe kama ni kwa kuibia,kudesa kuhonga wasimamizi au kihalali ilimradi wewe umefaulu na product yake ndiyo hiyo.
 
Hivi hapa hawa waungwana wanaposema wamepata mafanikio katika elimu wanamaanisha nini? Ubora wa Elimu ambayo inatolewa ama Uwingi wa watu wanaopata hiyo Elimu maana tunakuwa tunadanganyana sana.

Anaenda mwaka wa tatu akiwa madarakani na bila hata ya kuwa na soni wanadiriki kujisifu ati wamepata mafanikio. Mi nadhani one way ya kuangalia haya mafanikio ni kuangalia product zilizotokana na Elimu ya Kipindi cha Nyuma na Product zinazotoka kipindi cha Muungwana madarakani!
 
Huyu jamaa kwa mtaji huu akirudi tena baada ya 2010 basi watanzania tutakuwa tumelala sana.
 
Nivizuri jamani, tukajuwa hawa wanaojivunia wanatumia vigezo gani, kwa hakika kwenye mafanikio ya elimu kuna vigezo vingi, kabla ya kuingia kwenye mjadala huu, mimi nadhani ikiwa kila mmoja hapa atakuja na vigezo vyake basi tutakuwa na majawabu mengi ambayo mengine yanaweza kukatisha tamaa kwa wanafunzi, kama wao lengo lao lilikuwa ni kuengeza idadi ya wanafunzi basi hilo ndio lilikuwa lengo lao, mara nyingi mafanikio ya elimu huwezi kuyapata kwa miaka miwili hata kidogo ni process inayohitaji ushiriki mkubwa wa jamii, kila nchi inamikakati yake kwenye mambo ya elimu kutokana na pale walipo na wapi wanapotaka kwenda, kuna nchi wao wameamua elimu ya juu zaidi kupeleka watu nje kwa kiwango fulani na hawa nao wanapofika pahala pa kujadili mafaniko ya elimu kwa taifa lao wanasema wamefanikiwa kusomesha jamii yao.
 
Hivi hapa hawa waungwana wanaposema wamepata mafanikio katika elimu wanamaanisha nini? Ubora wa Elimu ambayo inatolewa ama Uwingi wa watu wanaopata hiyo Elimu maana tunakuwa tunadanganyana sana.

Anaenda mwaka wa tatu akiwa madarakani na bila hata ya kuwa na soni wanadiriki kujisifu ati wamepata mafanikio. Mi nadhani one way ya kuangalia haya mafanikio ni kuangalia product zilizotokana na Elimu ya Kipindi cha Nyuma na Product zinazotoka kipindi cha Muungwana madarakani!

Mzee mzima ni msanii BINGWA. Tizama alivyomleta Kocha wa mpira wa miguu ukitaka kujua objectives zake.

Jafar, sidhani kama ana hamu ya kugombea 2010; I might be wrong!.
 
I can say they are doing very little as far as the quality of education is concerned. Bear with me education is not only buildings and quantity of students but is quality teaching aids ( books, laboratories, classes,practicals, charts etc) teachers themselves, sports activities and the like. They better change the philosophy other wise our fellow will grab us as far as east African community is concerned. Real they are trying to bribe us that they are doing some thing, they are enrolling a lot of Division 4 graduates to teach our lovely kids where are we going.
 
Back
Top Bottom