Na Salva Rweyemamu
SERIKALI imesema imepata mafanikio makubwa katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwagharimia wanafunzi 34,012 wanaotoka katika familia zenye kipato duni kwa ajili ya kupata elimu ya sekondari katika shule mbalimbali.
Katika mfanikio hayo serikali imesema ilipunguza ada kwa wanafunzi wa kutwa kutoka Sh 40,000 hadi Sh 20,000 na kuchukua jukumu la kutoa ruzuku ya fidia ya ada kwa wanafunzi 417, 712 mwaka 2006 na wanafunzi 755,079 mwaka 2007,Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu akitaja mafanikio ya elimu ya sekondari alisema kumekuwepo na ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi kutoka 355,188 hadi wanafunzi 829,094 mwaka 2007.
Alisema ili kuchangia nguvu katika mkakati wa kuongeza nafasi kwenye shule za sekondari serikali ilitoa Sh bilioni 6.4 kati ya mwaka 2005 na 2007, madarasa 4065, nyumba za walimu 3,404, maabara 124, majengo ya utawala 19 vilijengwa kwa kutumia ruzuku hiyo.Aidha alisema kuwa serikali imeendelea kuongeza ubora wa elimu kwa kutoa fedha za ruzuku ya uendeshaji kwa lengo la kufikia Sh 30,000 kwa shule za serikali na Sh 15,000 kwa shule binafsi zilizofuzu vigezo.
Mkurugenzi huyo alisema serikali imetoa Sh bilioni 16.9 za kununulia vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule za sekondari za serkali katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2007.Aidha alisema kwamba serikali inaendelea kuimarisha ukaguzi wa shule kwa lengo la kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa inakidhi mahitaji na kuendelea kutoa mafunzo ya walimu wakiwa kazini ili kuongeza uwezo wa walimu hasa katika masomo ya sayansi hisabati na Lugha.
-------------------------------------------------------------------
Baada ya miaka 2 karibu na nusu hayo ndio mafanikio ya JK. Mimi hainiingii akilini wakati mtihani wa darasa la nne na kidato cha pili nasikia imefutwa, muungwana anataka Quantity na si Quality. Hivi ubora wa elimu unapimwa kwa kiasi gani cha fedha kimetolewa au kwa kupima elimu inayotolewa ?