Serikali ya DRC yasema kundi la waasi wa FDLR-FOCA, limetekeleza mauaji ya Balozi wa Italia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,878
Serikali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewashtumu waasi wa FDLR wenye asili ya Rwanda, kwa kumshambulia na kumuua balozi wa Italia nchini humo Luca Attanasio hapo jana karibu na mji wa Goma, mashariki mwa nchi hiyo.

Balozi Attanasio alikuwa katika msafara wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP wakati gari lao liliposhambuliwa.
Hata hivyo, kundi la FDLR limekanusha kuhusika na shambulizi hilo, kwa kile inachosema vikosi vyake viko mbali na eneo la shambulizi hilo.

Maafisa katika mbuga ya wanyamapori ya Virunga wanasema shambulio hilo lilikuwa jaribio la utekaji nyara lililoshindikana, pale walipoingilia kati mara moja.

Makundi mengi ya wapiganaji wenye silaha yameendelea kujiimarisha ndani na pembezoni mwa mbuga hiyo inayopakana na nchi jirani za Rwanda na Uganda.

Waziri wa mambo ya nje wa jamhuri wa DRC Marie Ntumba Nzeza amefahamisha kuwa serikali yake imeanzisha uchunguzi kubaini wahusika wa mauaji hayo na kwamba mpaka sasa hawajakamatwa.

Mbali na balozi huyo wa Italia kuuawa, dereva wa gari raia wa Congo pia aliuawa katika tukio hilo.

Pia soma

- Balozi wa Italia nchini Congo DRC auawa katika shambulizi
 
Nachukizwa na mauaji yaliyotokea LAKINI hayo mauaji yamekuwa yakifanyika sana na jitihada za kuyakomesha hazikuwa zinafanikiwa. LABDA KWAVILE KAUAWA MZUNGU TENA BALOZI WA NCHI basi ngoja tuone waasi wakitoweshwa na AMANI KUREJEA DRC MASHARIKI
 
Ngoja tuone maana hata miaka ya tisini nadhani 97 balozi wa Ufaransa nchini Zaire/DRC aliuwawa.

Ile mbuga ni hatari sana na ina vikundi vya kigaidi mbalimbali kutoka nchi zaidi ya tatu. Kwa hivyo lazima nchi "zinazowalea" na kuwafadhili lazima zishirikishwe katika mpango wa amani.
 
Ikitokea mim ndo nmekuwa raisi wa Congo sasa hivi

Ndani ya saa 48 za mwanzo nitakuwa nishaichapa Rwanda.

Congo hakutatulia as long as watutsi wako hai.
 
Nachukizwa na mauaji yaliyotokea LAKINI hayo mauaji yamekuwa yakifanyika sana na jitihada za kuyakomesha hazikuwa zinafanikiwa. LABDA KWAVILE KAUAWA MZUNGU TENA BALOZI WA NCHI basi ngoja tuone waasi wakitoweshwa na AMANI KUREJEA DRC MASHARIKI
Hiyo si rahisi, kuuawa kwake hakuwezi kuyafanya mataifa yanayofaidika na uporaji yaanze kujishughulisha na kurejesha amani
 
Back
Top Bottom