Serikali ya Che Che Me inahusika na vifo vya watoto wachanga Ngara

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Serikali ya Chama cha mapinduzi (Che Che Me) inahusika kwa kiasi kikubwa na vifo vya watoto wachanga na wengine wanaopata ulemavu unaotokana na magonjwa yanayozuilika kama kupooza na kifua kikuu.
Uchunguzi nilioufanya mimi binafsi katika wilaya ya Ngara (jana na leo) kati ya vituo vya afya vitatu (Mrusagamba, Bukiriro na Mabawe) vilivyopo wilayani humo na zahanati 13 hakuna dawa ya chanjo kwa watoto wachanga ya kuzuia polio na pepopunda katika wilaya nzima.

Mtoto anayekosa chanjo hii anaweza kupooza na kuwa na ulemavu wa kudumu (endapo atapata matibabu) na asipopata matibabu anaweza kupoteza maisha. Tanzania ni moja ya nchi duniani ambazo kiwango cha watoto wanaokufa wakiwa na umri wa chini ya miaka mitano ni kikubwa duniani. Pia kiwango cha wanawake wanaokufa kwa sababu zinazohusiana na uzazi kiko juu.

Ukosefu wa madawa na vifaa tiba katika zahanati, vituo vya afya na hospitali kadhaa nchini vinaweka maisha ya watanzania walio wengi mashakani hasa maskini. Kama bado ahadi za Che Che Me za kuwahadaa watanzania juu ya kupata maisha kwa kila mtanzania zinaendelea, hatutaweza kuyafikia wala kuyakaribia mpaka hapo serikali inayojali watawala badala ya wananchi itapoondolewa madarakani.

Ndugu wananchi wa Ngara na Mbunge wetu tuungane kupinga udhalimu huu. Leo hapa Ngara serikali inatumia mamilioni ya fedha kusherehekea sikikuu ya mfanyakazi ambaye yuko hoi, dawa hospitalini hakuna, barabara hazipitiki na mambo mengine mengi kama hayo. Kwanini zisielekezwe kwenye kupata madawa ya chanjo? Na mbunge yuko wapi? India au dar maana jimboni hayupo muda wote.

Kazi kwetu wanangara

Nawasilisha

Quality
 
Back
Top Bottom