Mkuu sijui kama unaelewa maana ya serikali kivuli, hayo majina na wizara yanaendana na wizara alozitangaza kikwete kila waziri anakuwa na waziri kivuli wala si kwamba wakiingia madarakani watafanya hivyo. Fuatilia kama kuna wizara ambayo ni tofauti na ile ya kikwete!
Ni kweli ni kubwa lakini ni kwa sababu mbili
1. Ya kwanza ni kwasababu unatakiwa kuchagua watu wakusimamia kila wizara. hivyo kama wizara kubwa vilevile serikali kivuli itakuwa kubwa.
2. Haina Gharama: Hawa jamaa ni wabunge hivyo hawalipwi kwa kuwa Mawaziri vivuli!! hivyo haiongezei gharama serikali hata shillingi moja.
Wasi wasi wangu na hasa kama Mbowe anaruhusiwa kuunda serikali kivuli aitakayo yeye kikatiba;je isingekuwa vyema kuunda serikali ndogo kivuli ili mwaka 2015 watumie kama case study kuwaeleza wa Tanzania ni jinsi gani wapo serious kwenye kuokoa fedha za umma?
Mkuu sijui kama unaelewa maana ya serikali kivuli, hayo majina na wizara yanaendana na wizara alozitangaza kikwete kila waziri anakuwa na waziri kivuli wala si kwamba wakiingia madarakani watafanya hivyo. Fuatilia kama kuna wizara ambayo ni tofauti na ile ya kikwete!
Gazeti la tanzania daima limeandika hivi
"Akitumia kanuni ya 14 (2) toleo la mwaka 2007 Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alitangaza baraza dogo kivuli lenye Mawaziri na Manaibu 26 na kusema wametekeleza ahadi ya kuundwa kwa baraza dogo kama ilivyo kwenye ilani ya chama chao".
"Kanuni hiyo inaeleza kwamba ‘Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni atateua wabunge wa chama chake au wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ambao watakua wasemaji wakuu wa kambi ya upinzani kwa wizara zilizopo za serikali"
"Idadi ya Mawaziri na Manaibu Mawziri wa serikali ni 50 uteuzi wangu umezingatia hilo na kuwateua wasemaji wakuu na manaibu wao wasiozidi 29 ili kuishi kivitendo; kilio chetu cha muda mrefu cha kuwa na baraza dogo la mawaziri… natambua uwezo mzuri wa waheshimiwa wabunge wetu lakini ni vema kutenda tunayohubiri," alisema Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai"(mwisho wa kunukuu)
kikatiba kiongozi Mkuu wa Upinzani Bungeni anaweza kuunda serikali kivuli kwa jinsi anavyoona yeye na chama chake inafaa;kwa hiyo madai kuwa Serikali kivuli lzm i-reflect ilivyo serikali halisi hazina msingi wowote!
ingawaje Mbowe kasisitiza kuwa kaunda serikali ndogo lkn kwangu bado watu 26 ni wengi sana,angepunguza hadi at least 15-20!
Wengine uwezo wao wa analysis of issues ni questionable and leaves a lot to be explained. Mtoa mada ni mmoja wao!
If so,mbona hamna serikali kivuli ya wizara nyingi tu nikianzia ya jumuia ya africa mashariki inayoongozwa na mzee samwel sitta?
Kwani ni nini maana ya kivuli? Je, Unaweza kuwa na kivuli bila object?
Afrika Mashariki nayo ipo. Wewe umeorodhesha wizara 26 wakati wao wana wizara 29 ina maana umeacha wizara 3
CHADEMA itajengwa kwa kukosolewa wala siyo kwa siasa za "ndiyo mzee"