Serikali ya CCM Yashindwa Hoja na Halima Mdee

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
6,346
Reaction score
1,873
Ule mgogoro wa ardhi uliokuwa ukiwahusisha wananchi na kiwanda cha Cement cha wazo hatimaye umekwisha rasmi.

Na hii imetokana na juhudi binafsi zilizofanywa na mbunge matata Halima Mdee kwa kushirikiana na madiwani makini.
Wa chadema Janeth Rithe, Deus Mtiro na Esther Samany ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilaumu serikali kwa kuendelea kumkumbatia mwekezaji wa kiwanda hicho bila kuwajali wananchi ambao ni watanzania.

Hatimaye leo saa 7:00 mchana waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi pamoja na naibu wake walifika eneo la Chasimba wakiwa sambamba na timu nzima ya wizara hiyo iliyoongozwa na katibu mkuu wa wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi na hatimaye wamekubali kuwa wananchi wa chasimba,chachui na chatembo wataendelea kuwepo hapo maisha yao yote.

Hongera Halima Mdee, Janeth Rithe, Samanya waziri kwa kusikia kilio cha wananchi
 
Match Summary
Aggregate:Mdee 3-0 Gama
Ball Possession :70% vs 30%
Assists :Bill Lukuvi
Full time
 
Mkuu Chademakwanza naamini ujuzi wa Uanasheria wa Mhe.Mdee hautaishia kwenye kauli hizo za Lukuvi na timu yake.
Mhe.awaoganaze wananchi wote wa eneo hilo ililipimwe na liwe kwenye eneo liliopangwa (Michoro) kwa gharama yao hao wananchi bila kupoteza eneo sipokuwa yale yatakayopitiwa na Miundobinu kama Barabara za mitaa,eneo kwa ajili ya Dispensary ,shule etc.
Bila hivyo ni ulaghai ule ule wa Kisiasa baada ya Uchaguzi mambo ya bomoa bomaa yanarudi kama kawaida.

Last edited by a moderator:

Chini ya Kamanda Mdee Mambo yanafanyika kiumakini
 
Last edited by a moderator:

Nilini serikali ilishindana na cdm ikashinda?
 
Kamanda Mdee amefanya kazi kubwa sana na ya kupigiwa mfano.
Sasa tunamuongezea miaka mingine mitano ili afanye makubwa zaidi ya haya aliyofanya awamu hii ya 2010-2015!
 
Ndiyo kazi ya mbunge makini kama mdee
 
Last edited by a moderator:
Kamanda Mdee amefanya kazi kubwa sana na ya kupigiwa mfano.
Sasa tunamuongezea miaka mingine mitano ili afanye makubwa zaidi ya haya aliyofanya awamu hii ya 2010-2015!
Hakika kamanda Mwita Maranya
 
Kama halima anauwezo wa kumaliza mgogoro kwaini hajamaliza yeye mpaka amekuja Lukuvu ndiyo mgogoro ukaisha kwahiyo ujue kuwa bila serikali ya ccm kutia miguu hapo mgogoro usingeisha.
 
Kama halima anauwezo wa kumaliza mgogoro kwaini hajamaliza yeye mpaka amekuja Lukuvu ndiyo mgogoro ukaisha kwahiyo ujue kuwa bila serikali ya ccm kutia miguu hapo mgogoro usingeisha.
Lukuvu =Lukuvi
 
Tuacheni uchama jamani, MTU anapopiga kazi lazima tumsifie. Tangu Magamba yameanza hayajawahi kutoa kifaa kizito kama Lukuvi. Namkubali sana LUKUVi anajituma. Magamba igeni huo mfano. Hongera sana waziri, timu yako, Mbunge na Madiwani. Ndo tunachokitaka hiki.
 
Hongera sana kamanda Halima mdee
 
Kamanda Mdee amefanya kazi kubwa sana na ya kupigiwa mfano.
Sasa tunamuongezea miaka mingine mitano ili afanye makubwa zaidi ya haya aliyofanya awamu hii ya 2010-2015!
Kafanya nini sasa mbona amekaa na huo mgogoro zaidi ya miaka minne mpaka waziri lukuvi kaja ndiyo umeisha kwanini hajamaliza bila lukuvu kufika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…