Elections 2010 Serikali ya CCM na uonevu kwa walemavu...

Ngolinda

Senior Member
Apr 12, 2010
125
25
Hawa ni wapiga kura japo walemavu...nawafananisha wapiga kura hawa ktk kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi kama 'Mti mbichi' nikiwa na maana ndio wanaotegemewa kukiingiza chama chochote madarakani hapo October 31, kwa maneno mengine ndio mabosi wa nchi kwa sasa. Swali ni je, ikiwa watu hawa wananyanyaswa na kudhalilishwa namna hii tena katika kampeni za uchaguzi za CCM, itakuwaje pale ambapo uchaguzi utakuwa umepita na kuweka ukomo wa ubosi wao (wapiga kura) kwa kitambo?...hapo watakapogeuka kuwa 'Mti mkavu'. Kwa maelezo haya narudi katika swali langu la msingi;

Kama CCM wanautenda 'mti mbichi' namna hii, itakuwaje kwa 'mti mkavu'?

Jionee mwenyewe yaliyowakuta walemavu katika kampeni za CCM....see the attached document.

==================
Je...! ilihitajika Nguvu ya Namna Hii kwa Wadau Hawa..?
SONGOMBIGO+MLEMAVU+WA+KIKE-1.JPG

Mwanamke Mlemavu wa viungo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akizolewa msobe msobe na Askari kanzu wakike kwa kusaidiana na Geen Guard wa CCM baada ya kutaka kumwona Rais Jakaya Kikwete kwa nguvu bila kufuata utaratibu wakati Rais alipokuwa akiwahutubia wananchi mkutano wa hadhara wa kampeni , kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa mwishoni mwa wiki.

MLEMAVU+AKITHIBITIWA+%5B1%5D..JPG

Hapa akiondolewa kwa nguvu

MLEMAVU+NA+SONGOMBIGO+LA+KUTAKA+KUMWONA+JK-2.JPG

2.JPG

Juma Ramadhani (chini ya ulinzi) ambaye ni mkazi wa Nane Nane , Manispaa ya Morogoro , ambaye ni mlemavu wa viungo akizolewa msobe msobe na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia ( FFU) ambao wakisaidiana na Green Guard wa CCM . Sekeseke hilo lilianza mara baada ya Juma kudaiwa kutaka kumwona Mgombea Urais kwa Chama chama CCM,Mh Jakaya Kikwete kwa nguvu bila kufuata utaratibu , wakati huo Mh Jakaya alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni , kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini humo mwishoni mwa wiki.

Picha na maelezo kwa msaada wa Blog ya Haki Ngowi
 
Attachments

  • NGUVU KWENYE KAMPENI.pdf
    1.6 MB · Views: 124
Ccm watavuna wanachopanda.................wanawakokota wahuni kwa kutumia malori na kuwanunulkia pilau na miupombe ya kienyeji......wana dhambi ccm!!!!!
 
Mtu wa chini akiwatendea hata walemavu hivi, yule kiongozi wao atakuwa anafanya nini?
Hii inaonyesha picha halisi ya viongozi wetu, kutojali watu wake!
Je tuna haja ya kuendelea kuwapa mamlaka!
Faida za sera.JPG MLEMAVU AKITHIBITIWA [1]..JPG source: Food For Thought
 
View attachment 13357

Back
Top Bottom