Moja ya sifa ambazo huitambulisha serikali iliyopo madarakani ni itikadi yake hasa kupitia chama ambacho kwayo imeundwa.
Sote tunafahamu, serikali ya awamu ya tano imeingizwa madarakani na chama cha mapinduzi ambacho kiitikadi kinafuata msingi wa UJAMAA na KUJITEGEMEA.
Imani ya Ujamaa na kujitegemea kwa kiasi kikuwa sana vijana wa ccm pamoja na wazee wao wa sasa huenda hawaijui ama wanafanya kuwa hawaijui.
Kwanini?
Kwasababu mkazo wa ccm katika kujiletea maendeleo kutokea TANU unasisitizwa kwenye;
1) Ardhi
2)Watu
3)Siasa safi
4) Uongozi bora.
Hayo yote yanakiukwa, nikisema nidadavue yanakiukwaje nahitaji muda wa kutosha sana! Lakini kwa mwenye akili akitafakari namna mambo yanavyoendeshwa kibabe ataelewa maana yangu kwanini nasema yote yanakiukwa.
Nirudi kwenye hoja ya msingi. Serikali ya awamu ya tano inajinadi na kusisitiza suala la viwanda, lakini kiuhalisia wazawa hawajajengwa vyema kimtaji, kiuwezo, kitaaluma au kiufundi n.k.
Serikali imekomaa tu viwanda, viwanda huku viongozi wakiamini kwamba maendeleo ni matokeo ya viwanda wakati kiuhalisia viwanda ndio matokeo ya maendeleo. Na ndio maana inafikia wakati viongozi tena mawaziri wanashindwa kuelezea na kudiriki kusema mtu akiwa na majagi ya kusagia juisi manne tayari anamiliki kiwanda, mtu akiwa na cherehani nne za kushonea tayari anamiliki kiwanda. Huu ni upuuzi.
Sasa imefika wakati kwamba wazawa hawapo wa kujenga viwanda, serikali inaalika msululu wa mabepari kuja kuhodhi sekta ya viwanda.
Imeonekana mara kadhaa Ikulu ikijitapa kuwa tumekuwa na ugeni kutoka nchi fulani wametuahidi kuja kujenga kiwanda flani, huku wakiwa wamesahau kabisa kwamba kwa kufanya hivyo wanaua msingi au imani yao ya siasa za ujamaa na kujitegemea.
Kwahiyo serikali ya ccm inajikaanga kwa mafuta yake yenyewe kwa kusahau kuwajengea uwezo wazawa waweze kumiliki viwanda ila inawakaribisha mabwenyenye waje kuhodhi sekta ya viwanda ili Wazawa wawe watumwa wa mabepari kwa kuajiriwa kwa ujira wa bora mkono uende kinywani.
Viongozi hawajui wanachosimamia, hawana dira, hawana misimamo ya kile wanachoamini. Kwa awamu ya tano, Ujamaa unajengwa na mabepari kwa maneno mengine ccm mpya yenye itikadi ya Ujamaa inaamini Ujamaa hauwezi kujengwa bila Ubepari!!!!!