Serikali ya awamu ya tano imetaharuki kujeruhiwa Lissu

Linaweza kuwa ni jambo la kushangaza, kwamba wito wa Katibu Mkuu wa CHADEMA kwamba wanachadema wote nchini wafurike mahospitalini kujitolea Damu, umepokelewa visivyo na Serikali ya JPM, kiasi kwamba Polisi wanawafurusha wale wanaokwenda kuchangia Damu. nadhani mojawapo ya mambo magumu sasa hivi ni mtu kwenda Hospitali yoyote kusema unataka kuchangia Damu! watakuuliza mara mbilimbili kwa nini unachangia Damu. Ebo!

Pia linaweza kuwa jambo la kushangaza kwamba kukutana hadharani kumuombea Lissu ni jambo ambalo halitakiwi, wakati tumezoea mikutano mikubwa ya hadhara ya kuombea "Amani", au hata kuwaombea viongozi wetu, kuombea mvua, nk. Leo asubuhi nimewasikia Baby na Sam pale Clouds TV, kipindi cha 360, Baby alipendekeza kuwe na "Concert" kwa ajili ya kuchangia matibabu ya Lissu. Sam akatoa "ushauri wa bure" kwa wasanii ambao wangeshiriki hiyo Concert, wajipime kwanza kama wako vizuri katika masuala ya Kodi, wasijevamiwa na TRA! message sent! Pia Sam alitoa "ushauri wa bure" kama mtumishi wa umma anataka kumchangia Lissu, asitumie simu yake mwenyewe! Message sent!

Vilevile unaweza kushangaa kitendo cha Polisi kukamata watu wanaovaa Tshirt za "Pray for Lissu" kwamba inakuwaje tumezoea katika matukio mbalimbali "kumuombea fulani" ni kitu cha kawaida kabisa. lakini hii noma inatoka wapi?

Jibu ni rahisi tu. Matukio makubwa ya kisiasa hapa nchini: Ujio wa Vyama Vingi, mchakato wa Katiba mpya (wa Tume ya Warioba), yote haya yameletwa siyo na vuguvugu la wananchi, lakini yameanzishwa kutokana na msukumo wa watu fulani. Katika Vyama vingi ilikuwa ni msukumo hasa wa Nyerere. na aliona afadhali CCM ianzishe mfumo huo, ili iumiliki, kuliko isubiri mpaka vuguvugu au msukumo kutoka nje uiilazimishe serikali kuanzisha mfumo huo, bila kujitayarisha kuumiliki, ingekuwa hatari kwa CCM. na kweli, CCM ndiyo inamiliki mfumo wa Vyama vingi. inatunga sheria kwa ajili ya maonesho, lakini kinachofanyika ni tofauti kabisa.

Mchakato wa Katiba mpya, ambao pamoja na kugubikwa na sintofahamu nyingi, lakini wale wajumbe wa Tume waliamua kuacha tofauti zao pembeni na kuandaa kitu ambacho ni nadra sana kukiona kikitolewa katika nchi yetu. Katiba ambayo ingeweza kuleta suluhisho la kweli la matatizo yetu. Katiba ambayo ingeweza kuwa chombo cha kutumiwa na Rais mwenye nia njema ya "kuinyoosha nchi". lakini kwa kuwa mchakato huo haukuanzia kwa wananchi, ilikuwa rahisi kuupindua. namna nyingine wananchi wangekuja juu kudai katiba yao.

Sasa chini ya awamu ya Tano, ambayo inatumia "iron fist", imesababisha wale ambao ni "moderates" kama kina Mbowe, Mnyika, Baregu, nk. wapotee kwenye uwanja wa siasa au wapunguze kasi, na "hardliners, Hawks" kama kina Tundu Lissu, waanze kutamba zaidi. Magufuli amefunga platform ya siasa kwa vyama vya upinzani. wanaoweza kufanya siasa hizo sasa hivi ni wale ambao kwao ni "lolote na liwe", na hao siyo wengi sana. Kumbi za Mahakama na vituo vya polisi sasa hivi ndio viwanja vya siasa.

Lakini tukio la kushambuliwa Tundu Lissu, limemtoa Tundu Lissu kutoka umaarufu aliokuwa nao, mpaka kufikia hatua ya "ICON". Kwa mtu kama Tundu Lissu, hao waliompiga risasa wamefanya kitu ambacho hakikutarajiwa kabisa. CV ya Tundu Lissu imepaa sana. ni mtu wa aina hii ambaye anaweza kutumika kama cheche ambayo ikiangukia katika majani makavu, moto mkubwa utalipuka. na hii ndiyo hofu kubwa ya serikali ya JPM. Kwamba hatimaye kunaweza kutokea vuguvugu ambapo badala ya kupambana na kikundi cha wabunge wachache wa upinzani na viongozi wa vyama vyao, ambapo JPM aliwahi kuwatishia kwa kujiamini kabisa, alipomwambia Ndugai, washughulikie ndani ya Bunge, na mimi nitawashughulikia nje ya Bunge. Kwamba badala ya kupambana na kikundi kama hiki, sasa serikali italazimika kupambana na maelfu ya watanzania katika mikoa na wilaya mbalimbali. hicho ndio kinaitia hofu serikali ya JPM, inafikia kufanya vioja kama tunavyoona hivi sasa.

kwa bahati mbaya serikali hii haitambui kwamba ni yenyewe ndiyo imemtengeneza Tundu Lissu na kumpaisha kote huko. hata kama serikali ya JPM haihusiki kabisa na shambulio la Lissu, yaani siyo tu kwamba wale ma-gunmen hawakutumwa na serikali, lakini pia siyo watu wa serikali na pengine sababu hasa ni tofauti kabisa na mambo ya siasa, lakini kinachoiunganisha serikali katika kadhia hii ni ile behaviour yake muda wote huu, jinsi ambavyo imekuwa ikishughulika na Tundu Lissu na Upinzani kwa ujumla. Laiti serikali isingekuwa na taratibu kali namna hii, hadi kufikia JPM kuwadhibiti wabunge waliotamani kwenda kumuona Lema alipokuwa mahabusu kwa muda mrefu, wakati leo CCM inatoa barua ya kuwapongeza wanachama wake waliosaidia Lissu apelekwe Hospitali Nairobi.

Na licha ya kutotambua kuwa serikali ndiyo imekosea katika kushughulika na upinzani, pia hatua ambazo zinachukuliwa zinazidi kumpaisha Lissu. kuzuia maombi, kuzuia uvaaji wa Tshirt, kuzuia utoaji wa Damu. yote haya ni makosa makubwa ambayo yataigharimu sana serikali hii huko mbeleni. Nia ni kuzuia umaarufu wa Lissu usipae, lakini kinyume chake ndiyo atazidi kuwa maarufu. Hii mbona ni commonsense ya kawaida kabisa?
Tatizo hapa ni moja tu... Hakuna shughuli yoyote kati ya ulizotaja hapo juu ambayo mlengo wake siyo wa kisiasa... Kama ni kuvaa t shirt ya pray 4 Lissu why usikae nyumbani kwako ukamuombea au mkaenda Nyumba za ibada kwani ni lazima utoke nayo Nje uungane na wengine ndo muonekane mmeguswa sana. Kuhusu kuchangia damu why ifanyike nw? Kwani siku zote si wapo wasiokua na damu wanaohitaji msaada mbona msijitokeze siku zote mjitokeze sasa. Hii inaitwa POLITICAL ADVANTAGE. Msitumie ugonjwa wa Lissu kutaka kupata umaarufu wa kisiasa.
 
Affirmative,kwakua huo ni uanafiki.Ukitaka kutoa damu nenda kimya kimya kama siku nyingine za kawaida na si kama unaenda kwenye fiesta.
Je, kuna dhambi au kosa lolote kuwa mshikamano hata kama ninkwa ajili ya tukio maalum; kuhamasisha utoaji wa damu? Waweza kuuita unafiki na utakuwa sahihi lakini je, damu hiyo haitahitajika kwa sababu waliotoa ni wanafiki? Je, damu inapoteza hb yake ( ubora wake kwa sababu imetolewakinafiki)?

Mimi nakuelewa vizuri tu lakini damu inahitajika na huwa hata makanisani wanahamasishwa wanatoa, tena kwa hamasa tu si kwa utashi wa kweli, lakini kwa kufanya hivyo maisha ya watu yanaokolewa. Je, huoni kuwa ni vema tu kuunga mkono utoaji wa damu bila kuhoji motive?
 
Hayo ni mawazo yako ambayo yanadhihirisha kua utoaji wenu wa damu haukua genuine,ulikua fanatically,politically driven.
Eti utoaji damu haukuwa genuine, my foot!!! hivi kuna utoaji damu ambao siyo genuine? kutoa damu ni kutoa damu tu. Lakini hebu nifupishe habari hii, woga wa serikali ya CCM ni mkubwa mno. inaogopa kivuli chake. CCM kwa nini inatumia sana Polisi kupambana na upinzani? pamabaneni wenyewe. aibu! yaani mna serikali, mna kodi, bado mnahangaishwa na upinzani mpaka muombe msaada wa polisi???
 
Je, kuna dhambi au kosa lolote kuwa mshikamano hata kama ninkwa ajili ya tukio maalum; kuhamasisha utoaji wa damu? Waweza kuuita unafiki na utakuwa sahihi lakini je, damu hiyo haitahitajika kwa sababu waliotoa ni wanafiki? Je, damu inapoteza hb yake ( ubora wake kwa sababu imetolewakinafiki)?

Mimi nakuelewa vizuri tu lakini damu inahitajika na huwa hata makanisani wanahamasishwa wanatoa, tena kwa hamasa tu si kwa utashi wa kweli, lakini kwa kufanya hivyo maisha ya watu yanaokolewa. Je, huoni kuwa ni vema tu kuunga mkono utoaji wa damu bila kuhoji motive?
Kwa hili ni unafiki tu na fahamu kwamba hujakatazwa kutoa damu kwa njia nyingine kwahiyo km nia ya kweli ipo ,achana na kukaa nyuma ya key board ,nenda hospitali ukatoe damu,long kwa jinsi unavyokomalia haya mambo yenu ya kifiesta fiesta ni dhahiri kua hamkua na nia ya kutoa damu bali kujipatia umaarufu wa kisiasa tu.
 
Eti utoaji damu haukuwa genuine, my foot!!! hivi kuna utoaji damu ambao siyo genuine? kutoa damu ni kutoa damu tu. Lakini hebu nifupishe habari hii, woga wa serikali ya CCM ni mkubwa mno. inaogopa kivuli chake. CCM kwa nini inatumia sana Polisi kupambana na upinzani? pamabaneni wenyewe. aibu! yaani mna serikali, mna kodi, bado mnahangaishwa na upinzani mpaka muombe msaada wa polisi???
Utoaji wenu wadamu ulikua wa kinafiki tu
 
Tatizo hapa ni moja tu... Hakuna shughuli yoyote kati ya ulizotaja hapo juu ambayo mlengo wake siyo wa kisiasa... Kama ni kuvaa t shirt ya pray 4 Lissu why usikae nyumbani kwako ukamuombea au mkaenda Nyumba za ibada kwani ni lazima utoke nayo Nje uungane na wengine ndo muonekane mmeguswa sana. Kuhusu kuchangia damu why ifanyike nw? Kwani siku zote si wapo wasiokua na damu wanaohitaji msaada mbona msijitokeze siku zote mjitokeze sasa. Hii inaitwa POLITICAL ADVANTAGE. Msitumie ugonjwa wa Lissu kutaka kupata umaarufu wa kisiasa.
Uvaaji wa Tshirt unazuiliwa kwa kifungu gani cha sheria? kama ni political advantage, mbona tshirt za "Magufuli Baki" hazikupigwa marufuku? mara ngapi kuna tshirt tunaona watu wanatengeneza kumuombea fulani na fulani. nongwa ni kwa Lissu tu?
 
Eti utoaji damu haukuwa genuine, my foot!!! hivi kuna utoaji damu ambao siyo genuine? kutoa damu ni kutoa damu tu. Lakini hebu nifupishe habari hii, woga wa serikali ya CCM ni mkubwa mno. inaogopa kivuli chake. CCM kwa nini inatumia sana Polisi kupambana na upinzani? pamabaneni wenyewe. aibu! yaani mna serikali, mna kodi, bado mnahangaishwa na upinzani mpaka muombe msaada wa polisi???
Hakuna cha uoga hapo ni unafiki ndiyo unaopigwa vita katoe damu kimya kimya uone kama Kuna mtu atakugusa
 
Kwa hili ni unafiki tu na fahamu kwamba hujakatazwa kutoa damu kwa njia nyingine kwahiyo km nia ya kweli ipo ,achana na kukaa nyuma ya key board ,nenda hospitali ukatoe damu,long kwa jinsi unavyokomalia haya mambo yenu ya kifiesta fiesta ni dhahiri kua hamkua na nia ya kutoa damu bali kujipatia umaarufu wa kisiasa tu.
Kwa hiyo damu iliyotolewa kinafiki haifai kwa matumizi ya kuokoa uhai au una maana gani mkuu?
 
Kwa hiyo damu iliyotolewa kinafiki haifai kwa matumizi ya kuokoa uhai au una maana gani mkuu?
Hatutaki vitu vinavyofanyika kinafiki basi.Kama una damu ya kutoa match hadi pahala husika kimyakimya, kivyakovyako,toa damu kimyakimya,ondoka kimyakimya.Hakuna atakaekugusa na si kuvaa sare na kuonyesha ishara za chama
 
Nadhani roho inamuuma sana maana Lisu hajawambia wamwombee watu kwa kujua umuhimu wa Lisu ndio maombi yanakuja automatic lakini wewe kila hatua naomba mniombee. na hakuna dalili ya wewe kuombewa lazima roho ikuume... kumbuka sala ya watu ina nguvu haswa.. Asante Mungu kwa kuisikia sala zetu. endelea kumponya Tundu Lisu kwa kweli na umefanya maajabu
AMEN
 
Hakika Nguvu ya Mungu imeonekana< Hakika pia Lissu amelipigania Taifa hili mpaka Damu yake kumwagika kwa ajili ya Taifa hili, nionavyo binafsi huyu ndie afaaye kuungwa mkono na daima tumwombee kwani ndie raisi ajae !!!!!!!

TL anasifa nyingi sana lakini hii inampambanua na wengi. Na yaliyotokea (Mola amrehemu) yanaonyesha anaishi yale asemayo. Na kwa kuwa Mungu hajawahi kushindwa bado titasikia na kuona mengi kuhusiana na huyu jabali. Uchambuzi wakokiapande hiki nimeupenda sana. Tunapopanga na kutekeleza mambo tufikirie matokeo yake hasa yale ambayo hatukuyategemea kara ya kwanza. Serikali inaonekana ina react na haina mkakati wa kuhandle hili tukio matokeo yake inafanya mambo yanayo ipa twasira mbaya mbele ya wananchi. Askari hao hao kwa gharama hizo hizo au chache zaidi ingeweza kufanikisha watu kuoa damu zaidi sio kwa ajili ya Lisu bali kwa watanzania wengine. Sala pia zingefanyika kwa amani. Watu wakikusanyika na kuoma wakiwa na ulinzi kuna ubaya gani?

Mungu huwa ana mikakati ambayo ipo nje ya uwezo wa binadamu.Kupitia Lisu Mungu anataka kuonesha ukuu wake dhidi ya Mfalme Zero.
 
Kuna watu wana roho mbaya sijawaona hivi mtu ukiwambia tu watu wafanye mikutano wanakuiaje kufanya Maendeleo manake sidhani km vyama vya siasa vitafanya kila siku hiyo mikutano...Au wataandamana kila siku
 
Back
Top Bottom