Serikali ya awamu ya tano imetaharuki kujeruhiwa Lissu

Yaani hata mimi nilijiuliza, hivi kwa mfano baada ya Dr. Mashinji kuagiza wanachadema wakatoe Damu, tuseme Polepole naye, au Kinana, angesimama na kusema kwa kweli kutoa Damu ni jambo jema sana, na tunawatia moyo wanaccm na watanzania wote wajitokeze kutoa Damu kwa ajili ya wagonjwa wetu, mbona tungepata Damu nyingi tu? Maana tukumbuke kwamba huwezi kutembeza mchango kwa ajili ya maafa ya tetemeko, kama hakuna tetemeko. limetokea janga, ni nafasi ya kuchangisha damu, fedha, nk. maana watu wanakuwa wameguswa na hilo tukio. tumepoteza fursa nzuri sana kwa ajili ya cheap politics
You are very right!
 
Sirro pita usome bandiko hili acha kuendeshwa uko...
Ninavyojua Sirro ingawa anaitwa IGP hana tofauti na gari la mkokoteni linalosubiri kusukumwa tu ndio lisogee kutoka lilipo. Amri wanazopokea walio chini yake hazitoki kwake bali zinatoka kwa wenye mamlaka zaidi yake. Anaona tu polisi wake wakikamata wananchi na kuwasweka ndani bila kujua nani hasa anatoa amri hizo na kwa sababu zipi.

Hivyo hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu yupo kama hayupo na ameduwaa tu akisubiri maelekezo atoe kauli gani ambayo haitamuudhi bosi wake. Muda wote yuko karibu na simu akisubiri ruhusa ya kuongea. Ni kama vile serikali nzima imepigwa shoti ya umeme na hakuna anayejitambua, kiranja mkuu na mshikaji wake wamezishikilia akili zao.

Nina hakika wangekuwa na mamlaka hawangekubali ujinga unaoendelea kama huu wa kuwakamata waliotitikia wito wa kuchangia damu. Katika dunia ya leo kuna vitendo vinaweza kufanywa tu na watu wenye matatizo ya akili na katika awamu hii tumewashuhudia wengi. Yako yasiyoweza hata kufikirika kwa mtu mwenye akili timamu lakini yanafanyika.
 
Pingo ambalo Mungu amewapiga Lucifer bashite na baba yake hawatakaa wasahau wanatafutiza vitu vya kuwakeep busy ili wapunguze msongo wa mawazo kwa kweli ni hadhiti ya utukufu wa mwenyezi sikutegemea kuoona muujiza uliotokea ndani ya maisha ya Lissu ni malaika tu waliokuwa wakimlinda na kuziba damu zilizokuwa zinamagika,kuendesha moyo uliokuwa unatabu ya kusabaza damu kwenye maeneo yote risasi kumpata sehemu ambazo haziendani na akili yake yaani hata kama atakuja amelemaa lakini akili yake magu hawezi kuipata maana itaendelea kutambua na kuongoza harakati za ukombozi kwenye taifa la dictator
 
Tatizo ni kwamba Serikali inafikiria kwamba Mungu anafanya kazi yake kama Serikali. Kwa Mungu, ukikusudia kwenda kuiba, halafu ukakatisha mpango baada ya kuona kwamba kuna walinzi au usalama wako ni mdogo, au siri imefichuka, kwa Mungu wewe tayari umeiba na unapata adhabu ya Mwizi. kwa hiyo, mtu kama amekusudia kusali kumwombea Tundu Lissu, halafu akafurushwa na Polisi, ile nia ya mtu au kikundi kile, tayari ni sala na imefika kwa Mungu!!!! Polisi sijui kama wanalijua hilo.
Safi hapa umezungumzia nia....Mungu anaangalia nia mja ikoje na sio tendo stahiki
 
Huo si ukweli na hata kama ni ukweli damu ikitolewa wanaofaidika ni akina nani. Au unafikiri yote inahitajika kumsaidia TAML!
Kwanini hawakufanya hivyo kabla na kwa njia tofauti?
Kwani imeanza kuhitajika leo tu kwa ajili ya huyo TAML?
Ni kwanini msihamasishane kimya kimya bila kuchanganya na mambo ya kisiasa?
TAML anatibiwa kwenye hospitali ambayo gharama yake kwa siku tshs mil 10,hivi kwa akili yako ya kawaida bila kuweka hata ya kindergarten unadhani hiyo hospitali ina upungufu wa damu kiasi cha kiwango hicho?
Ikiwa mnatoa damu kwa ajili ya TAML kwanini msiende hukohuko aliko mkamtolee damu hukohuko?
 
Ninavyojua Sirro ingawa anaitwa IGP hana tofauti na gari la mkokoteni linalosubiri kusukumwa tu ndio lisogee kutoka lilipo. Amri wanazopokea walio chini yake hazitoki kwake bali zinatoka kwa wenye mamlaka zaidi yake. Anaona tu polisi wake wakikamata wananchi na kuwasweka ndani bila kujua nani hasa anatoa amri hizo na kwa sababu zipi.

Hivyo hivyo Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu yupo kama hayupo na ameduwaa tu akisubiri maelekezo atoe kauli gani ambayo haitamuudhi bosi wake. Muda wote yuko karibu na simu akisubiri ruhusa ya kuongea. Ni kama vile serikali nzima imepigwa shoti ya umeme na hakuna anayejitambua, kiranja mkuu na mshikaji wake wamezishikilia akili zao.

Nina hakika wangekuwa na mamlaka hawangekubali ujinga unaoendelea kama huu wa kuwakamata waliotitikia wito wa kuchangia damu. Katika dunia ya leo kuna vitendo vinaweza kufanywa tu na watu wenye matatizo ya akili na katika awamu hii tumewashuhudia wengi. Yako yasiyoweza hata kufikirika kwa mtu mwenye akili timamu lakini yanafanyika.
Nadhani sababu kubwa ya kumtoa Ernest Mangu nafasi ya IGP, na kumweka pale Sirro, ni kwamba Ernest ni askari Polisi kweli, mwenye weledi. huyu Sirro ni mtu ambaye anakubaliana na chochote. katika kada yoyote ile, wapo watu wanye kipaji cha kuwa kiongozi, tokea wa ngazi ya chini, ya kati, na ya juu. siyo kila Polisi anaweza kuwa IGP. Sirro hafai hata kuwa RPC. mwisho wake ni OCD tu.
 
Kwanini hawakufanya hivyo kabla na kwa njia tofauti?
Kwani imeanza kuhitajika leo tu kwa ajili ya huyo TAML?
Ni kwanini msihamasishane kimya kimya bila kuchanganya na mambo ya kisiasa?
TAML anatibiwa kwenye hospitali ambayo gharama yake kwa siku tshs mil 10,hivi kwa akili yako ya kawaida bila kuweka hata ya kindergarten unadhani hiyo hospitali ina upungufu wa damu kiasi cha kiwango hicho?
Ikiwa mnatoa damu kwa ajili ya TAML kwanini msiende hukohuko aliko mkamtolee damu hukohuko?
Kwa taarifa tu ni kwamba wito wa kutoa Damu ulikuwa ni kwa lengo la kusaidia wagonjwa popote nchini. Soma vizuri tangazo la Katibu Mkuu Dr. Mashinji. na kumbuka kwamba huyu ni Daktari wa binadamu, siyo daktari wa Kemia au mahesabu. kwa hiyo ana uelewa wa pekee kuhusu tatizo la Damu nchini. alihamasisha tu watu waende kuchangia Damu. watu siyo wehu kiasi hicho kwamba damu ichangwe nchi nzima kumpelekea Tundu Lissu
 
Kwanini sasa na si kabla na kwanini kichama?
 
Linaweza kuwa ni jambo la kushangaza, kwamba wito wa Katibu Mkuu wa CHADEMA kwamba wanachadema wote nchini wafurike mahospitalini kujitolea Damu, umepokelewa visivyo na Serikali ya JPM, kiasi kwamba Polisi wanawafurusha wale wanaokwenda kuchangia Damu. nadhani mojawapo ya mambo magumu sasa hivi ni mtu kwenda Hospitali yoyote kusema unataka kuchangia Damu! watakuuliza mara mbilimbili kwa nini unachangia Damu. Ebo!

Pia linaweza kuwa jambo la kushangaza kwamba kukutana hadharani kumuombea Lissu ni jambo ambalo halitakiwi, wakati tumezoea mikutano mikubwa ya hadhara ya kuombea "Amani", au hata kuwaombea viongozi wetu, kuombea mvua, nk. Leo asubuhi nimewasikia Baby na Sam pale Clouds TV, kipindi cha 360, Baby alipendekeza kuwe na "Concert" kwa ajili ya kuchangia matibabu ya Lissu. Sam akatoa "ushauri wa bure" kwa wasanii ambao wangeshiriki hiyo Concert, wajipime kwanza kama wako vizuri katika masuala ya Kodi, wasijevamiwa na TRA! message sent! Pia Sam alitoa "ushauri wa bure" kama mtumishi wa umma anataka kumchangia Lissu, asitumie simu yake mwenyewe! Message sent!

Vilevile unaweza kushangaa kitendo cha Polisi kukamata watu wanaovaa Tshirt za "Pray for Lissu" kwamba inakuwaje tumezoea katika matukio mbalimbali "kumuombea fulani" ni kitu cha kawaida kabisa. lakini hii noma inatoka wapi?

Jibu ni rahisi tu. Matukio makubwa ya kisiasa hapa nchini: Ujio wa Vyama Vingi, mchakato wa Katiba mpya (wa Tume ya Warioba), yote haya yameletwa siyo na vuguvugu la wananchi, lakini yameanzishwa kutokana na msukumo wa watu fulani. Katika Vyama vingi ilikuwa ni msukumo hasa wa Nyerere. na aliona afadhali CCM ianzishe mfumo huo, ili iumiliki, kuliko isubiri mpaka vuguvugu au msukumo kutoka nje uiilazimishe serikali kuanzisha mfumo huo, bila kujitayarisha kuumiliki, ingekuwa hatari kwa CCM. na kweli, CCM ndiyo inamiliki mfumo wa Vyama vingi. inatunga sheria kwa ajili ya maonesho, lakini kinachofanyika ni tofauti kabisa.

Mchakato wa Katiba mpya, ambao pamoja na kugubikwa na sintofahamu nyingi, lakini wale wajumbe wa Tume waliamua kuacha tofauti zao pembeni na kuandaa kitu ambacho ni nadra sana kukiona kikitolewa katika nchi yetu. Katiba ambayo ingeweza kuleta suluhisho la kweli la matatizo yetu. Katiba ambayo ingeweza kuwa chombo cha kutumiwa na Rais mwenye nia njema ya "kuinyoosha nchi". lakini kwa kuwa mchakato huo haukuanzia kwa wananchi, ilikuwa rahisi kuupindua. namna nyingine wananchi wangekuja juu kudai katiba yao.

Sasa chini ya awamu ya Tano, ambayo inatumia "iron fist", imesababisha wale ambao ni "moderates" kama kina Mbowe, Mnyika, Baregu, nk. wapotee kwenye uwanja wa siasa au wapunguze kasi, na "hardliners, Hawks" kama kina Tundu Lissu, waanze kutamba zaidi. Magufuli amefunga platform ya siasa kwa vyama vya upinzani. wanaoweza kufanya siasa hizo sasa hivi ni wale ambao kwao ni "lolote na liwe", na hao siyo wengi sana. Kumbi za Mahakama na vituo vya polisi sasa hivi ndio viwanja vya siasa.

Lakini tukio la kushambuliwa Tundu Lissu, limemtoa Tundu Lissu kutoka umaarufu aliokuwa nao, mpaka kufikia hatua ya "ICON". Kwa mtu kama Tundu Lissu, hao waliompiga risasa wamefanya kitu ambacho hakikutarajiwa kabisa. CV ya Tundu Lissu imepaa sana. ni mtu wa aina hii ambaye anaweza kutumika kama cheche ambayo ikiangukia katika majani makavu, moto mkubwa utalipuka. na hii ndiyo hofu kubwa ya serikali ya JPM. Kwamba hatimaye kunaweza kutokea vuguvugu ambapo badala ya kupambana na kikundi cha wabunge wachache wa upinzani na viongozi wa vyama vyao, ambapo JPM aliwahi kuwatishia kwa kujiamini kabisa, alipomwambia Ndugai, washughulikie ndani ya Bunge, na mimi nitawashughulikia nje ya Bunge. Kwamba badala ya kupambana na kikundi kama hiki, sasa serikali italazimika kupambana na maelfu ya watanzania katika mikoa na wilaya mbalimbali. hicho ndio kinaitia hofu serikali ya JPM, inafikia kufanya vioja kama tunavyoona hivi sasa.

kwa bahati mbaya serikali hii haitambui kwamba ni yenyewe ndiyo imemtengeneza Tundu Lissu na kumpaisha kote huko. hata kama serikali ya JPM haihusiki kabisa na shambulio la Lissu, yaani siyo tu kwamba wale ma-gunmen hawakutumwa na serikali, lakini pia siyo watu wa serikali na pengine sababu hasa ni tofauti kabisa na mambo ya siasa, lakini kinachoiunganisha serikali katika kadhia hii ni ile behaviour yake muda wote huu, jinsi ambavyo imekuwa ikishughulika na Tundu Lissu na Upinzani kwa ujumla. Laiti serikali isingekuwa na taratibu kali namna hii, hadi kufikia JPM kuwadhibiti wabunge waliotamani kwenda kumuona Lema alipokuwa mahabusu kwa muda mrefu, wakati leo CCM inatoa barua ya kuwapongeza wanachama wake waliosaidia Lissu apelekwe Hospitali Nairobi.

Na licha ya kutotambua kuwa serikali ndiyo imekosea katika kushughulika na upinzani, pia hatua ambazo zinachukuliwa zinazidi kumpaisha Lissu. kuzuia maombi, kuzuia uvaaji wa Tshirt, kuzuia utoaji wa Damu. yote haya ni makosa makubwa ambayo yataigharimu sana serikali hii huko mbeleni. Nia ni kuzuia umaarufu wa Lissu usipae, lakini kinyume chake ndiyo atazidi kuwa maarufu. Hii mbona ni commonsense ya kawaida kabisa?
To every action there is an equal and opposite reaction.
 
Kwanini sasa na si kabla na kwanini kichama?
Hivi ingewezekana kuomba watanzania wachangie walioathirika na tetemeko bukoba, kabla ya tetemeko? kunapotokea tatizo, watu wanaweza kuhamasika kuchangia kitu fulani. unaweza kuona mwenyewe, vyombo vya habari duniani kote vinaongelea suala la Tundu Lissu. Mitandao ya Jamii hapa nchini imejaa mada hii. kwenye kumbi, vijiwe, sehemu mbalimbali mada hii inatawala. kwenye bunge pia. sasa katika mazingira kama hayo, ukiwaambia watu wachangie damu Tanzania nzima, watakuelewa.
Na kweli, hivi wewe umesikia mara ngapi watu wa hospitali wanaita watu wachangie damu, na watu hawaitiki sana? lakini katika wito huu, kutokana na kuguswa, watu wangemiminika kwa maelfu kuchangia damu wagonjwa wetu na benki ya damu ingejaa, kama siyo ujinga na upumbavu wa watala wetu. shida iko wapi?????
 
Hivi ingewezekana kuomba watanzania wachangie walioathirika na tetemeko bukoba, kabla ya tetemeko? kunapotokea tatizo, watu wanaweza kuhamasika kuchangia kitu fulani. unaweza kuona mwenyewe, vyombo vya habari duniani kote vinaongelea suala la Tundu Lissu. Mitandao ya Jamii hapa nchini imejaa mada hii. kwenye kumbi, vijiwe, sehemu mbalimbali mada hii inatawala. kwenye bunge pia. sasa katika mazingira kama hayo, ukiwaambia watu wachangie damu Tanzania nzima, watakuelewa.
Na kweli, hivi wewe umesikia mara ngapi watu wa hospitali wanaita watu wachangie damu, na watu hawaitiki sana? lakini katika wito huu, kutokana na kuguswa, watu wangemiminika kwa maelfu kuchangia damu wagonjwa wetu na benki ya damu ingejaa. shida iko wapi?????
Acha kujitoa ufahamu,tatizo la damu halikuanza Leo na usifananishe tetemeko na mambo ya kuchangia damu kwa hiari.Kama una damu ya kutoa nakushauri uende kimyakimya tu na utapokelewa utatoa damu na kuondoka kimyakimya.Tahadhari usivae nguo za chama.
 
Kwanini hawakufanya hivyo kabla na kwa njia tofauti?
Kwani imeanza kuhitajika leo tu kwa ajili ya huyo TAML?
Ni kwanini msihamasishane kimya kimya bila kuchanganya na mambo ya kisiasa?
TAML anatibiwa kwenye hospitali ambayo gharama yake kwa siku tshs mil 10,hivi kwa akili yako ya kawaida bila kuweka hata ya kindergarten unadhani hiyo hospitali ina upungufu wa damu kiasi cha kiwango hicho?
Ikiwa mnatoa damu kwa ajili ya TAML kwanini msiende hukohuko aliko mkamtolee damu hukohuko?
Kwa hiyo dami kwenye benki ya damu haihitajiki kwa sababu watoaji wanatoa kuonyesha mshikamano kwa madhila aliyopata TAML?
 
Acha kujitoa ufahamu,tatizo la damu halikuanza Leo na usifananishe tetemeko na mambo ya kuchangia damu kwa hiari.Kama una damu ya kutoa nakushauri uende kimyakimya tu na utapokelewa utatoa damu na kuondoka kimyakimya.Tahadhari usivae nguo za chama.
naona na wewe unaumwa ugonjwa unaoitwa UPINZANIOSIS. ingekuwa Pole pole ametoa wito kwa wanaccm kuchangia damu, wala isingekuwa ishu na hapa JF isingeingia. kwa nini mna insecurity kiasi hicho?
 
Kwa hiyo dami kwenye benki ya damu haihitajiki kwa sababu watoaji wanatoa kuonyesha mshikamano kwa madhila aliyopata TAML?
Affirmative,kwakua huo ni uanafiki.Ukitaka kutoa damu nenda kimya kimya kama siku nyingine za kawaida na si kama unaenda kwenye fiesta.
 
Acha kujitoa ufahamu,tatizo la damu halikuanza Leo na usifananishe tetemeko na mambo ya kuchangia damu kwa hiari.Kama una damu ya kutoa nakushauri uende kimyakimya tu na utapokelewa utatoa damu na kuondoka kimyakimya.Tahadhari usivae nguo za chama.
Nimekupa mfano wa tetemeko kwa sababu umeuliza kwa nini hawakutoa wito wa kuchangia damu kabla. kwa nini watoe kabla wakati wameamua kutoa sasa hivi? shida iko wapi? shida ni kuchangia damu?
 
naona na wewe unaumwa ugonjwa unaoitwa UPINZANIOSIS. ingekuwa Pole pole ametoa wito kwa wanaccm kuchangia damu, wala isingekuwa ishu na hapa JF isingeingia. kwa nini mna insecurity kiasi hicho?
Hayo ni mawazo yako ambayo yanadhihirisha kua utoaji wenu wa damu haukua genuine,ulikua fanatically,politically driven.
 
Back
Top Bottom