Serikali ya awamu ya 5 imetambua hatujiwezi

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,829
2,387
Mwanzoni tulijifanya nchi yetu ni tajiri. Hatuhitaji msaada. Asilimia 40 ya bajeti itaenda kwenye miradi ya maendeleo. Mifuko ya hifadhi ya jamii kujenga viwanda.
Leo hii, misaada ina masharti magumu. Mikopo ni ghali kutokana na hali ya soko la dunia, (sijui soko lipi hilo). Mtikisiko wa kibenki upo na nchi nyingine. Biashara zinafungwa kwa sababu ya kubadili biashara lakini hawasemi ngapi zimefunguliwa.
Baada ya hapo, tumeomba mikopo na tunasaka mikopo sehem.kadhaa, tumeomba serikali ya China itusaidie kujenga viwanda. Tumeomba, tunaomba na tutaendelea kuomba.
Tujipange, tutayumba zaidi.
 
Unapo yumba wewe wengine ndo wanafaidika
 
Nchi sasa imefilisika rasmi.

Bajeti iliyosomwa bungeni ni makaratasi matupu..

Hakuna pesa za Miradi ya Maendeleo.

Mwanzoni pale alisema hapendi vi misaada misaada.

Sasa hata wa kumuomba amkope hayupo.

Serikali ya awamu ya 5 ipo hoi bin taabani.

Na bado.
 
Tuombeni jamani, viongozi wa dini ombeeni Taifa mambo yaende sawa. Tumuombe Rais wetu kipenzi mambo yatakaa sawa hiki ni kipindi cha mpito tu.
 
walioko halmashauri za wilaya, manispaa na majiji watufahamishe wamepata fedha za miradi ya maendeleo na kwa asilimia ngapi ya bajeti yao?
 
Tuombeni jamani, viongozi wa dini ombeeni Taifa mambo yaende sawa. Tumuombe Rais wetu kipenzi mambo yatakaa sawa hiki ni kipindi cha mpito tu.
Siafiki maombi haya kutoka viongozi wa dini. Labda tuanze na toba. Katiba Bible kuna jamaa mmoja alipokutana na Yesu akatubu kwa kusema "wote niliowadhulumu nawarudishia mara nne" kama nakumbuka vizuri anaitwa Zakayo. Mapadri na Mashehe waombee serikali hii baada ya kurudisha michango ya wahanga wa Kagera. Bila hivyo maombi mengine ni ya kujifurahisha tu!!
 
Back
Top Bottom