A
Anonymous
Guest
Habari wana Jamvi,
Leo nimekuja kuwasilisha kero yangu moja kubwa sana kuhusu hawa watu wanaotupangishia Nyumba au Frame za biashara. Naelewa ni zao na wana haki ila kitendo cha Mmiliki kuamua kupandisha kodi kila baada ya muda mfupi kwa kiwango anachojisikia sio sawa.
Je, Mamlaka husika au Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuna mwongozo au sheria yoyote ya kumlinda Mpangaji dhidi ya Mpangishaji kuhusu masuala mbalimbali likiwemo hili la kupandishiwa kodi? Wananchi tunaumia maana haiwezekani mtu unapandishiwa kodi kiholela kwa 120% ndani ya miaka miwili
Wafanyabiashara katika eneo Sinza Mori - Dar, Frame zinazotazamana na Kituo cha Mafuta cha Big Born wamepandishiwa kodi kwa asilimia 90% ndani ya mwaka mmoja. Kodi hiyo imepanda kutoka takribani TZS 700,000/- hadi TZS 1,500,000/- na mabadiliko haya yameanza Machi 2024.
Lakini kwenye frame hizo hizo naambiwa kwa mwaka jana 2023 kodi ilipanda kutoka TZS 400,000/- hadi kufikia 700,000/-. Naelewa hawa ni wafanya biashara na huenda kwamba anayeshindwa kulipa si lazima akae hapo lakini hii sio haki na sio sawa.
Najiuliza sana kama hawa wanafanyiwa hivi, si ajabu pia kuna wengine wanafanyiwa hivi lakini kwa taratibu tulizonazo hakuwa sehemu ya kufikisha malalamiko yao.
Serikali ni vema kuweka miongozo au kanuni kuhusu masuala ya kupangisha nyumba au frame; miongozo iseme wazi ni wakati kati kodi inaweza kupanda na kwa kwa kiasi gani na masuala mengine bila kumuumiza Mpangaji au Mpangishaji
Hali hii inaweza kusababaisha kuua bishara za wengi kwani kwa mfanyabiashara kuhama eneo huwa na impact kubwa sana lakini pia atawezaje kupata nguvu ya kupambana na biashara ili aweze kuishi na kuweza kuchangia mapato kikamilfu kwenye mamlaka za mapato Tanzania (TRA) kwaajili ya kuchangia pato la taifa kwaajili ya maendeleo ya wote?
Malalamiko mengine ni kuwa Mmiliki anataka fedha ya miezi 6 na hataki kupokea bank transfer bali anataka kiasi hiko kikubwa cha fedha takriban 9M kama fedha taslimu (mkononi), mbali na hayo Mmiliki anatoa mkataba wenye 1% ya pesa ilio lipwa yaani Mkataba kusoma Tsz 100,000/= tu
Je, Mamlaka husika inawasaidiaje Wafanyabiashara hawa? Mana hii ni kama case study ya tatizo hili nchini kwetu, wapo wanao miliki majengo na frame wengi sanaa wenye tabiaa hii.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi na Mamlaka ya Mapato (TRA) tunapaza sauti kwenu, tunaomba msikie sauti zetuu!