Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,140
- 1,982
Heshima Kwenu,
Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ametoa taarifa kuwa serikali imelipa deni la zaidi ya Tsh. Trilioni moja kwa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Kumekuwa na malalamiko kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii haina fedha za kutosha kulipa wanachama wake kwa kuwa nyingi ya fedha zake zimekopwa na serikali na hazijalipwa kwa wakati.
Jambo la kusikitisha ni kuwa serikali imelipa fedha hizo ili eti mifuko ya hifadhi ya jamii iweze kutimiza lengo/sera ya serikali ya Tanzania ya viwanda. Huu ni upotoshaji. Lengo kuu la kuanzisha mifuko ya hifadhi ya jamii si kufungua viwanda. Ni kutunza na kukuza fedha kwa minajili ya kulipa mafao.
Aina ya uwekezaji na mahali pa kuwekeza si kazi ya serikali. Ni jukumu la mifuko.