Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTARATIBU WA UHAKIKI WA ORODHA VA MALIPO HAUCHELEWESHI MSHAHARA
Kumekuwa na taarifa za kupotosha zikionyesha zinatoka Ofisi ya Rais - Utumishi kuwa kwa sababu ya zoezl Ia uhakiki, mishahara ya Watumishl wa Umma itachelewa. Taarifa hiyo ni ya uzushi na haina ukweli wowote .
Watumishi wa Umma watalipwa mshahara wa mwezi Machi 2016 kwa wakati, kama ilivyo ada. Hivyo, waendelee kufanya kazi na wasikatishwe tamaa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Ofisi ya Rais - Utumishi, moja ya majukumu yake ni kusimamia malipo ya mishahara ya Watumishi wa Umma, kazi hiyo kwa mwezi Machi 2016 ilishakamilika na kinachosubiriwa ni malipo kufanyika.
lmetolewa na Kitengo cha Mawasillano Serikalini Ofisi ya Rais-Utumishi