Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,614
Kuna migogoro ya idadi kubwa ya chinichini kati ya Kiwanda cha Urafiki na makampuni binafsi, kati ya Kiwanda na wapangaji wa apartments zake na pia kati ya Kiwanda na serikali (Manispaa ya Ubungo).
Soko lisilo rasmi (soko bandia lisilokuwepo pale kisheria ya mipangomiji) la ndizi na mbogamboga almaarufu Mahakama ya Ndizi inaingiza faida ya Tsh.1bl kwa mwezi. Haya ni mapato haramu kwa sababu yanatoka sehemu isiyo rasmi kisheria na isiyo na miundombinu ya soko bora la kisasa.
Mapato haya yanagombewa na serikali, kiwanda na uongozi wa soko hadi dola kutumia nguvu kuyatwaa mapato haya 100% bila hata mgawo kwa wadau wengine hao 2 kikiwemo kiwanda ambacho ndicho mmiliki wa eneo.
Soko hilo bandi na haramu ndilo soko pekee ndani ya JMT linaloingiza mapato makubwa ya Tshs.1bl kwa mwezi.
Soko kuu JMT ambalo ni Shirika la Umma la KMC (Kariakoo Markets Corporation) linaingiza Tsh.56ml kwa mwezi na Tsh.678ml kwa mwaka (aibuuu...)
Kiwanda cha Urafiki kimekufa na sasa kinajiendesha kwa kodi za pango za fremu, apartments, soko la mitumba, Makanisa, maegesho ya bodaboda, bajaji na toyo, mamantilie, wafanyabiashara ndogondogo, waosha magari, bar, vibanda, maduka, gereji, bustani na sheli (japo hiyo ya mwisho taarifa zisizothibitishwa zinasema alimegewa mtoto wa kiongozi mmoja mwenye uchu mkali sana wa ardhi).
Kwa kuruhusu aina zote hizo za biashara eneo hilo, hakuna mwenye uhakika kama Kiwanda kimeenda serikalini kuomba kubadili matumizi ya ardhi hiyo au kimeamua kufanya hivyo kwa kuvunja sheria tu.
Makampuni ya usafirishaji mizigo na abiria yanagombana kila siku kuwania pango kwenye eneo hilo, mara 2 wafanyakazi wa makampuni hayo wamebadilishana viganja (wamepigana ngumi) kugombania maegesho hadi LATRA wamekuja kuweka beams kwenye mipaka ya barabara.
Kiwanda cha Urafiki ni masalia halisi ya mfumo wa Ukabaila nchini uliokosa kutibiwa na sera za Mwl. Nyerere aliyeishi kutokomeza mfumo huo kwa jamii za Ki-tz.
Serikali mkoa wa Dsm imemaliza ardhi yote (ardhi yote ya Dar imepangiwa matumizi) kiasi kwamba ikitaka kutekeleza mipango yake inayohitaji ardhi inabidi ama ijenge kwenda juu angani au ifidie watu binafsi kupata ardhi au ipeleke mpango/mradi mkoa jirani wa Pwani.
Mapendekezo ya ufumbuzi wa mgogoro huu mkongwe:-
1.Napendekeza kwa serikali namna salama ya kutokomeza masalia ya Ukabaila pale Urafiki ni kwa kutwaa ardhi hiyo yote 100% na kuipa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT kwa ajili ya upanuzi wake kufuatia kuongeza kozi nyingi za kubobea kwenye taaluma ya usafirishaji ikiwemo kozi ya urubani ili pia kiweze kudahili wanafunzi zaidi wanaokosa nafasi kwenye vyuo vingine.
2. Tanzania-China Textile Mills (Kiwanda cha Urafiki) kipewe ardhi Mkuranga. Chuo cha Taifa cha Uvuvi Mbegani kinahamishiwa Mkuranga ili kupisha Mwekezaji wa bandari pale Bagamoyo, hivyo hakuna madhara kwa Kiwanda cha Urafiki kuhamishiwa Mkuranga ambako ni eneo la kimkakati la viwanda na zoni ya kuchakata uchumi (EPZ).
3. Mapato ya soko bandia (soko haramu) lisilokuwepo kisheria la Mahakama ya Ndizi yagawanywe kwa haki baina ya wadau wote ambao ni Kiwanda, Manispaa ya Ubungo na uongozi wa soko.
4. Fumua Bodi ya Kiwanda kama ipo ili kuondoa uzembe, uvivu na mnyauko-wa-akili-wa-kufikiri-kimkakati kwa ajili ya kutafuta tija ya Kiwanda hicho.
NB.
1. Serikali kupitia PSRC na Mfilisi iliuza maeneo ya viwanda vya nyavu na zana za kilimo kwa Mwekezaji akajenga Business Park.
2. Serikali kupitia PSRC na Mfilisi iliuza maeneo ya Makampuni ya Usafirishaji Abiria Jijini ya:-
2.0 UDA Kurasini na Ubungo ambapo Ubungo palijengwa Kituo Kikuu cha Mabasi ya Mikoani na Shoroba za EAC, CA na SADC na baadaye kupewa Mwekezaji anayejenga soko kubwa la bidhaa toka ughaibuni.
2.1 KAMATA Kariakoo pamepewa Mwekezaji pia.
2.2 Maeneo kadhaa ya TRC yamepewa Wawekezaji pia.
Serikali haina faida na Kiwanda-tasa cha bidhaa za pamba cha Urafiki ambacho mapato yake yanafaidisha tu Makabaila-sugu.
The sooner the better.
Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app