Serikali tupeni majibu kuhusu haya ya Mh. Lissu!

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
mheshimiwa Tundu Lissu amekuwa akichachafya serikali kwa hoja moja mbali mbali hasa zinazohusiana na katiba na mambo ya sheria,yafuatayo ni mifano michache
1.serikali ya zanzibar kuanzisha majeshi kinyume cha katiba
2.serikali ya Zanzibar kujitangazia uhuru bila kutaja neno uhuru
3.Muungano sio halali kwa kuwa bunge la zanzibar wakati wa kuungana halikutunga sheria ya kuridhia muungano
4. Mambo yaliyoongezwa kwenye article 11 za muungano ni batili kwa kuwa hayakufata sheria ya muungano
5.wakuu wa mikoa na wilaya ni watumishi wa umma hivo kuwa wabunge ni kinyume na katiba
6. Wanajeshi ambao sio wastaafu kuwa wakuu wa wilaya ni kinyume cha katiba
7. Mahakama ya Rufani iliingizwa kuwa jambo la muungano kinyemela
8.Rais wa muungano kukaa kimya wakati kuna uvunjifu mkubwa wa katiba hasa upande wa Zanzibar ni kosa na anatakiwa kushitakiwa bungeni kwa kushindwa kulinda katiba aliyoapa kuilinda?

Hayo ni machache sana ila serikali ya ccm imekuwa inataoa majibu ya jumla au kumshambulia Lissu binafsi na sio hoja zake! Swali langu ni lini serikali hii itapitia kifungu hadi kifungu hoja za kamanda Lissu na kuzitolea majibu ya kisheria na sui ya kisiasa, huu ni wajibu mkubwa sana wa mwanasheria mkuu(AG) na waziri wa sheria na katiba!!Kuna mkanganyiko mkubwa sana wa kikatiba i.e katiba ya zanzibar, katiba ya JMT NA Sheria ya muungano! tupeni majibu sio porojo na siasa!
 
Mkuu serikali yote kwa sasa iko bize kuhusu ishu ya Dr. Ulimboka...
 
kwa kweli hata nyerere mwenyewe angekuwepo angeshindwa kujibu hoja za Lissu, hoja zake ni ngumu wala AG hana jibu. Jana umeona alivomuubua mwenekiti yule mhagama alipomtaka kufuta maneno ktk hotuba ya upinzani eti kwa kuwa AG hajayapenda, alimwambia mhagama ivi , 'mwenyekiti ktk suala la kanuni tutagombana sana, kiti chako hakifuati kanuni za bunge na uyo AG wako hafuati kanuni izi' Hapo akamsomea kifungu kwa kifungu mpaka mhagama akasikia kizunguzungu bila kuelewa kinachoendelea akadai suala ilo analipeleka kwenye kamati .....mh Lissu ana hoja kali sana na ccm hakuna kama yeye....buneni hakuna aliyewai kumjibu labda kejeli tu za viongozi wa serikali bungeniiiiii!
 
Viongozi wa kitaifa ni janga tena vilaza hata majukum yao wameyaweka pembeni kama sio kuyasahau kabisa.

Rais anaongoza kwa kuvizia wala hana final say nor decision making on critical matters. Mr president keeps comlaining and to some extent uses intimancy approach where psychological or logics is needed.

the ruling part will never ever provide critically the answers as quested by Lisu.

Lisu has been dealing with the realities, is very hard and actually incrindible to fight the fact because you'll be dipicted as a deminter by citizens.

Surely not easy for kikwete nor other ccm kada's to defend the truth blown out by Tundu's findings. Infact they can play with lies, cheating and propaganda to weaken Lisu's quests, yet trueth will exist and one day will be validated and proved beyond doubt and Lisu will emerge the hero.
 
wanamuogopa sanaa,dreva aliwahi kuuambia uma kuliko lisu awe mbunge nibora wamnyime unahodha,chezea lisu wewee,magambaa hua tunawachabo kwenye runinga wanavyo palangana hawanaga hoja.mmoja wa cdm ni magamba 30.
 
Jaman ukweli huwezi kuupinga, Lisu anapita njia ya kuuleza uma upuuzi na madudu wayafanyao watawala na ccm yao bila kufuata sheria, taratibu, kanuni wala miiko.

Watadanganya lakin ukweli utadum tu na wataumbuka siku moja.
 
mheshimiwa Tundu Lissu amekuwa akichachafya serikali kwa hoja moja mbali mbali hasa zinazohusiana na katiba na mambo ya sheria,yafuatayo ni mifano michache
1.serikali ya zanzibar kuanzisha majeshi kinyume cha katiba
2.serikali ya Zanzibar kujitangazia uhuru bila kutaja neno uhuru
3.Muungano sio halali kwa kuwa bunge la zanzibar wakati wa kuungana halikutunga sheria ya kuridhia muungano
4. Mambo yaliyoongezwa kwenye article 11 za muungano ni batili kwa kuwa hayakufata sheria ya muungano
5.wakuu wa mikoa na wilaya ni watumishi wa umma hivo kuwa wabunge ni kinyume na katiba
6. Wanajeshi ambao sio wastaafu kuwa wakuu wa wilaya ni kinyume cha katiba
7. Mahakama ya Rufani iliingizwa kuwa jambo la muungano kinyemela
8.Rais wa muungano kukaa kimya wakati kuna uvunjifu mkubwa wa katiba hasa upande wa Zanzibar ni kosa na anatakiwa kushitakiwa bungeni kwa kushindwa kulinda katiba aliyoapa kuilinda?

Hayo ni machache sana ila serikali ya ccm imekuwa inataoa majibu ya jumla au kumshambulia Lissu binafsi na sio hoja zake! Swali langu ni lini serikali hii itapitia kifungu hadi kifungu hoja za kamanda Lissu na kuzitolea majibu ya kisheria na sui ya kisiasa, huu ni wajibu mkubwa sana wa mwanasheria mkuu(AG) na waziri wa sheria na katiba!!Kuna mkanganyiko mkubwa sana wa kikatiba i.e katiba ya zanzibar, katiba ya JMT NA Sheria ya muungano! tupeni majibu sio porojo na siasa!

Mkuu hayo maswali ya lissu next level dont expect vichwa panzi like Ag na chikawe watajibu.nilimsikiliza chikawe jana wakati akijiumauma kuhusu uteuzi wa wakuu wa wilaya
 
Hata wakikataa! Serekali ya jk ipo ipo tu haijielewi dawa ni kuongeza kina Tundu lissu,mdee,Mbowe,dogo janja,Mnyika,Zitto,Slaa wengine bungeni wafike 180 hivi pengine serekali itawajibika kwetu.
 
Back
Top Bottom