Vichekesho nchi hii, kwanza tujiulize serikali ilitaka kuachieve kitu gani kwa kukamata meli ile na shehena yake. Meli imeshikwa haifanyi kazi na inaharibika bandarini shauri ya sea corrosion, samaki wapo sehemu ambapo storage charges ni kubwa kuliko kawaida mabaharia wako ndani muda wote toka meli iliposhikwa.
Mpaka hapo utaona serikali yetu ina liabilities tatu meli kuharibika kwa kutotumika, samaki kuhifadhiwa kwa gharama kubwa na kuwanyima uhuru mabaharia wa meli hiyo.
Chukua scenario hii upande wa mashtaka unashindwa kuthibitisha kesi na mabaharia wanachiwa, mwenye meli atafungua kesi dhidi ya serikali kudai fidia ya loss of business, kuharibika meli, kuharibika bidhaa zake. Mabaria nao wanaweza kufungua madai kwa kufunguliwa kesi isivyo halali. In that situation serikali italipa kiasi kikubwa sana, na hatutaachive kitu apart from international reputation.
Walipa kodi tusiombee hiyo scenaio itokee we will pay through our noses.